Kuelekea Mechi ya Simba SC dhidi ya AS Vita Club, hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika 'Hatoki Mtu'


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
18,452
Likes
54,036
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
18,452 54,036 280
Kuelekea mechi ya Simba SC dhidi AS Vita Club kutoka Kongo, hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, mchezo utakaovurumishwa Jumamosi Machi 16, 2019 kunako Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Hatoki Mtu.

Kocha wa Simba SC, Mbelgiji Patrick Aussems amesema na kusisitiza kuwa wanaelekeza nguvu na akili katika mechi hii ya mwisho huku akiongeza kuwa anajua anapambana na wapinzani wa namna gani kwenye ligi hii Mabingwa Afrika.

••Kulipewa Mwana.....Kulitaka Mwana

AS Vita Club haitoki salama, itapigwa vibaya kutokana na uwezo wa Simba SC kutumia vema Uwanja wa Taifa, MKAPA STADIUM, kwa kuwachinja wapinzani wao hatua ya makundi kila aliyetia mguu Kimataifa.

Vilevile kumbuka na fahamu kwamba kwenye kundi D hakuna timu ambayo imeshinda ugenini, wala kupoteza mchezo (kufungwa) nyumbani, kila timu imeshinda nyumbani kwake.

Yatasemwa mengi na uchambuzi wa kila aina kutoka pande zote zenye kufuatilia soka, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hakuna timu imeshinda nje ya mji wake kwenye kundi D, hivyo tunatarajia Simba SC itaigaragara vilivyo AS Vita Club na Washirika wake hivyo kuweza kufuzu katika hatua ya robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu ushindi JF Simba SC, sembo OKW BOBAN SUNZU Shunie King Ngwaba Sapta Sapta Tui barafuyamoto toxic9 Jaby'z Mshuza2 nyakubonga Twende sasa hapa Ubaoni..Na uwanja wa Taifa.

This Is Simba SC...SimbaNguvuMoja.

img_20190313_074329_311-jpeg.1044481
tapatalk_1552456545196-jpeg.1044483
 

Forum statistics

Threads 1,272,373
Members 489,924
Posts 30,449,207