Kuelekea Makongamano ya kudai Katiba Mpya, Haki za Msingi ziheshimiwe

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,223
35,149
Kudai haki za msingi za yeyote ni masuala yasiyo hitaji ridhaa za asiyehusika na hasa mlalamikiwa.

Haki za msingi kwa mlalamikaji haziwezi kutegemea ukubali wa mlalamikiwa.

Mlalamikaji na ategemee machungu kamili kutoka kwa mlalamikiwa, ujira wa kutokuchoka kwake ni kupatikana kwa haki husika.



Huku ni kuchezana shere ambako ni muhimu mlalamikiwa akafahamu kuwa hakukubaliki.

Kama wewe si mlalamikiwa na unadhani hauhusiki kwenye madai ya haki husika, mambo ya pilipili usizozila ndipo yanapoingia hapo!

Ni sahihi kuombana kutowashwa washwa enyi mnaodhani kuwa hamhusiki kwenye agenda hii yenye maslahi makubwa kwa nchi yetu.

Nakazia: Kuelekea Makongamano ya kudai katiba mpya, haki za msingi za watu na ziheshimiwe kwani haki huinua taifa.

Amandla!
 
The economic vision is always directed by the political organization structure (constitution - Katiba). Short of that results to economic illusions.

It is known that, all sort of excuses will be hatched to avoid getting to the real cause of our economic and social problems.

Relenting is not an option anymore.

The beneficiaries of the status quo should know we are demanding (not asking) for a new Constitution.
 
Matatizo yetu ya uchumi yanatokana na katiba mbovu tuliyo nayo:

1. Wizi kiasi gani umekuwa ukifanyika kwa miaka nenda rudi serikalini na hatua zipi zimewahi kuchukuliwa?
2. Pesa kiasi gani zimekuwa zikitumika kwenye chaguzi viini macho zisizokuwa na tija nchini?
3. Kwanini vigogo hawalipi kodi na mzigo wa tozo na kodi ni kwetu?
4. Vipi majumba na magari ya mabilioni wanayopeana wao kama zawadi walipaji tukiwa sisi?
5. Vipi pesa zinazotumika kununulia wapinzani na kuandaa chaguzi mpya?
6. Vipi pesa za kulipa wabunge wasiokuwa na sifa?
7. Vipi mzigo wa serikali 2 zilizopo?
8. Vipi sintofahamu ya Dar es Salaam, Dodoma na Chatto kama miji mikuu?
9. Vipi mashirika yanayozalisha hasara kila uchao?
10. Vipi kukosekana kwa mpango mkakati kuhusiana na ugonjwa na athari za Corona?
11. Nk nk

Katiba mpya si kizingiti cha kukuza uchumi bali kichocheo sahihi sasa kwa ajili ya kukuza uchumi na kwa haraka zaidi.
 
Kupata Katiba Mpya Tusipigane Kipumbavu (Tupeane Makavu):

Makamanda watukuka agenda ya kudai katiba mpya ni ya msingi mno. Hii ni kwa maslahi yetu leo na hata kwa watoto wa wajukuu zetu.



Agenda hii haipaswi kufanyiwa mzaha hata kidogo. Ikibidi hata kutiana bakora wenyewe kwa wenyewe ili kuifanikisha itakuwa ni sehemu ya wajibu uliotukuka katika kuipigania.

Katika agenda hii, ni muhimu tukaelewana:

1. Hatuwezi kuwa na adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu kwenye harakati hizi.
2. Lazima tuwe na mkakati unaoeleweka wa mapambano usioshindwa na usiojali nani anatuongoza kwa wakati gani.
3. Lazima tuwe na mkakati kamili wa kuwahami wahanga kama mashujaa wetu mstari wa mbele, magerezani au hata wakiwa wafu.
4. Lazima tuwe na mpango mkakati wa kuwahusisha washirika wengi kwa kadri inavyowezekana, shughuli ni watu.
5. Lazima wigo wa ushiriki upanuliwe kuhakikisha wote walio tayari kujihusisha kwa namna yoyote wanahusishwa kikamilifu katika harakati hizi.
6. Jitihada zote zifanyike kujenga maelewano mema na wengine hata ambao wanaweza kuwa ni mahasimu wetu leo.
7. Tuwekeze zaidi kwenye vinavyotuweka pamoja kuliko kwenye vinavyo tutenganisha.
8. Tuwakemee na kuwadhibiti wajumbe wetu wenye kutenda kupalilia matengano na mitafaruku isiyokuwa na tija.
9. Harakati hizi ziwe kwa manufaa ya umma na si binafsi katika mali, pesa au kisiasa.

Ni wazi kuwa anayepinga jitihada za kupata katiba mpya sasa anaweka kizingiti si kwetu tu, bali hata kwa watoto wa wajukuu zake mwenyewe.

Hapa tuna walalamikaji, wadaiwa (walalamikiwa) na wasiohusika. Kila mmoja na aijue au ajuzwe nafasi yake akapate kujitambua anaposimama.

Kwani pilipili mtu asizozila zimuwashe yeye namna gani?

Angalizo: Mwana mpotevu aliporudi nyumbani kwa baba yake, aliyekuwa mwana mwema alichukizwa kiasi cha kuondoka nyumbani moja kwa moja!

Makamanda tusipigane kijinga. Bila kuyajaza magereza haipo katiba mpya hapa!

Cc: Cannabis
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom