Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Wadau,Niko hapa maeneo ya mbagala mwanamtoti natoka kwenye pilika zangu,mpaka saa hizi naandika huu uzi ,saa moja na dakika hamsini na sita,Bado Kuna watu wamejazana katika vituo vya kusajilia laini za simu.
Mida mchache ujao tutasikiliza taarifa ya habari sijui,E-1 ataongeza muda Tena au ndo imetoka.
Hebu tuendelee kula mtori ,nyama tutazikuta chini.
Wenye updates za usajili watuletee kuitia uzi huu.
Cc,ziro iq.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani muda ukiisha kuna tatizo lipi? Si unanunuwa SIM card mpya na kuisajili hapo hapo?
 
*Laini yangu ya Vodacom*

*BALANCE*

1. Salio la kawaida Tsh 0.00
2. Salio la M-PESA Tsh 0.00
3. Salio la M-PAWA Tsh 0.00

*MADENI*

1. Nipige tafu deni Tsh 3000/=
2. M-Pawa deni Tsh 58000/=
3. SONGESHA deni Tsh 76500/=

_Laini haijasajiriwa kwa alama za vidole, Sina namba ya NIDA nasubiri maamuzi ya TCRA, nipo tayari kwa lolote_

Sent using Jamii Forums mobile app
 
By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.


Kesho Jumatatu Januari 20, 2020 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitazimwa. Ili uweze kusajili laini ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho.
Mnazima kesho au keshokutwa? Mlisema mwisho tarehe 20/1/2020, sasa kwa nini mzime kesho badala ya keshokutwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9914CB36-FCBA-4657-B2AB-B4D9E69CD4F9.jpeg


Ujumbe huu umenisikitisha kutoka kwa mmoja wa waumini wenzangu ambae anawakilisha mamilioni ya watanzania wengi watakaofungiwa laini zao siku ya 20/01/2020.

My Take:
Kwa kua watakaozimiwa wote ni kwa sababu wamekosa namba za Nida ndani ya muda uliopangwa, ili wawasiliane na ndugu zao watalazimika kusajili laini kwa namba za watu waliopata. Hii pia nimeishuhudia sehem nyingi za kusajilia watu wakisajili kwa vitambulisho vya watu wengine.

Wahusika hawakujipanga vizuri. Waliosajili kwa namba zao halali ni wachache sana, wengi wamenunua namba zilizokua zimeandaliwa na mawakala, wengine wamesajili kwa vitambulisho vya ndugu, marafiki au jamaa tu. Acha tuweke akiba ya maneno, muda utaongea!
 
Mbona mnafanya kama janga au msiba wakati mambo ya kawaida tu... Copy contacts, toa pesa zako zilizomo basi... Kama utasajili nyingine kopa halafu tupa.
 
Back
Top Bottom