Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

NIDA kumekuwa na folen ya kufa mtu sio kwa kuwa watu wanataka vitambulisho vya Taifa bali kwa kuwa wanapigania namba zao za simu zisizimwe

Yaan watu hawana mpango na vitambulisho sema tu inabidi wawe nacho kukamilisha usajili

I.e line ya simu ni muhimu kuliko kitambulisho
ikitangazwa kuwa usajili wa line sio muhimu kitambulisho cha NIDA basi folen inaisha fasta
ukienda airtel wanakwambia netwok ipo down njoo kesho... ukifika kesho wanakwambia ipo pending njoo kesho
aliyetoa siku 20 haja calculate haya ya njoo kesho sijui mtandao uansumbua. dah mashaka haya mpaka lini sijui
 
Kuthibitisha kama laini yako ya simu imesajiliwa kwa alama za vidole piga *106# chagua 1


Kwanza niwape pole wale wote ambao wanashinda ofisi za NIDA bila kufanikiwa.

Ukweli process ya vitambulisho ni ndefu sana.

Kwa wale ambao hawana vitambulisho vya NIDA unaweza tafuta ndugu yako ukasajili kwa kutumia kitambulisho chake, kitambulisho kimoja kinaruhusiwa kusajili laini 10.

Kwa wale ambao hawajasajili hakikisha fedha zote umezitoa na kama umezoea kutumia mobile banking hakikisha kadi yako ya ATM ipo valid otherwise utapata usumbusu mkubwa sana kupanga foleni bank na kupata ATM mpya inachukua more than one week.

Kwa NIDA nashauri watume majina na namba za wananchi ambao wameshajaza form na hawajapata namba zao ili mitandao ya simu (MNO) wasiwafungie kwa sababu hawana hatia.

Nawatakia weekend njema.

------
Waziri Nditiye asema hekima itatumika usajili wa laini kwa wasio na vitambulisho vya Taifa


Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.

Chanzo: Mwananchi

 
Naona mnadanganyana hahahaha mlikuwa wapi siku zote? NIDA kuna shida lakini watanzania tuna shida zaidi,,,,, kuna namba nyingi sana zimeshatoka lakini hadi leo hazijasajiliwa ,,,,,,,,
Hata pale mwananchi anaponyanyaswa na serikali yake bila hatia kazi yako ww nikujikomba kwa jiwe ili upate mlo!
Nani kalalamika hapa kwamba ana namba ya NIDA na ameshindwa kusajiri?

Hata hivyo, wakati wewe unasifu na kuabudu watawala walio kosa hekima, ukidhani mnawakomoa wapinzani,
ndg zako huko kijijini wanasota na NIDA na hawajafanikiwa kupata hata namba na ni miongoni mwa watakaofungiwa line zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina line 2. Moja nimesajili kwa kitambulisho cha jamaa (ili nijihadhari na kutokuwepo kwenye mawasiliano)... Nyingine (ya kwangu ya siku zote) sijasajili. Hii ya kwangu ikifungiwa haina shida coz watu wangu hawatonikosa hewani kwa hii nyingine na JF nitaendelea kuenjoy :D :D :D

HIVI NDIVYO NILIVYOJIANDAA KISAIKOLOJIA.
 
Kisaikolojia fanya haya. Kama una smartphone utaendelea na internet kwa wi fi ya mtu mwingine karib. Utaacha aina zote za mikopo ya mitandaon. Utafanya mawasiliano ya kupiga kwa internet tu bila line kwenye whasapp, viber etc. Utarudia mifumo ya kibenk kuhusu pesa hasa huduma ya cardless. Mwisho wa yote utaambulia usumbuf kias lakin kampun zitapoteza makato meng yanayokuhusu na serkali itapoteza mapato ya kodi.
Bonge la point...pia tutajipunguzia usumbufu wa matangazo yao kwa njia ya sms
 
Yaani nimecheka kwa sauti ya juu hapo kwenye kupatia maisha ... Mkuu bado sema mimi kipindi kile cha kujiandikisha NIDA sikuukataa wito nilifanya hivyo kwa siku tatu mfululizo mpk kuja kufikia sehemu ya kupiga picha nakumbuka nikaenda halafu nikachana na hiyo biashara nikaja kutumiwa msg sijui baada ya miezi zaidi ya minne nikafuata kitambulisho.


Mimi huwa sina tabia ya kupuuzia mambo huwa nasema ngoja nifanye ikae hapo huwezi jua....
Huo muda unao.
Sisi waajiliwa tusio na off na tunaingia asubuhi kutoka usiku ndo wenye kimbembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom