Kuelekea Klabu Bingwa Afrika | Simba SC na Al Ahly SC, Mechi ya Kibabe kwa Wababe wa Soka

Status
Not open for further replies.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Jambo TANZANIA na Duniani Kote..!

Naaaam..!

Jumanne ya February 23, 2021 muda wa saa 10:00 Alasiri, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, kutakuwa mchezo wa kundi A' wa Klabu Bingwa Barani Afrika ambapo Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni Simba SC, anakwaruzana na Mabingwa Watetezi Al Ahly SC kutoka nchini Misri.

Patashika hii ya aina yake inatarajiwa kuwa kali mno, na ya kusisimua kwa wote wa muda wote dakika 90 kwa kila timu kuhitaji ushindi na kujikusanyia alama tatu muhimu.

Timu zote mbili katika michezo yao ya kwanza waliweza kushinda, ambapo Simba SC waliweza kuibuka na ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club na Al Ahly SC wakiwachapa Al Merrikh kwa mabao 3-0 nchini Misri.

Kutoka Simba SC "Ni jukumu la kuteta heshima ya soka TANZANIA na Afrika Mashariki lipo kwetu hivyo maandalizi ya kuleta heshima tutakapowakabili Mabingwa namba tatu wa dunia inaendelea.

Mechi ya Kibabe, mechi ya wanaume wa shoka, wababe wa soka Afrika, siyo ya kukosa, vita ndani ya uwanja kuhakikisha tunabeba alama zote tatu za mchezo"
taarifa ya Simba SC imeeleza.

Jambo kubwa kwetu kama Watanzania, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC pamoja na Wadau wa soka ni kuwaombea dua wanajeshi wetu.

Si mchezo mwepesi lakini kuna jambo tunakwenda kulifanya kuelekea mchezo huo, hivi ni vita zaidi ya vita vya Kimbari, hivyo kunahitaji jitihada na nguvu ya pamoja kuweza kushinda vita. Hivyo tujipange na tuweze kushinda na kuipeperusha vema bendera yetu..Mungu Ibariki Simba, Mungu Ibariki TANZANIA.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Utapata yanayojiri kuanzia leo mpaka siku ya mchezo kutoka kwa Jopo la WanaJF sembo, OKW BOBAN SUNZU, Shunie, NAWATAFUNA, Mwifwa, Dam55, mjingamimi, Root, rodrick alexander, mmteule, Payrol Saint Ivuga, King Ngwaba, Scars na wengine chini ya Nahodha...Ghazwat
FB_IMG_1613892508851.jpg
FB_IMG_1613892472973.jpg


Update;

Wachezaji wa Simba SC wamefanya mazoezi leo jioni ya February 21 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Tayari kabisa kuwakabili Al AhlyView attachment 1708571

..MO Dewji

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC na Mwenyekiti Murtaza Mangugu pamoja na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, wamehudhuria mazoezi leo kuona namna timu inavyojiandaa kuwakabili Al Ahly.

..Kocha Msaidizi Suleiman Matola

"Si rahisi ni mechi ngumu ikichukulia kwamba tulipata matokeo katika mchezo uliopita, na ukiangalia ligi ya mabingwa Afrika hakuna mtu rahisi.

Lakini tumejipanga pamoja kwa kwamba tunakutana timu ambayo iko nzuri na bora zaidi, lakini lazima tuhakikishe tunapata matokeo katika mchezo wetu wa nyumbani".

..Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane

"Tupo tayari kwa mchezo hakuna la kuhofia na muda wa mechi sio sababu ya kubadili kikosi, tupo tayari kwa mapambano.

Simba ilicheza Kinshasa na kushinda dhidi ya As Vita na hicho ndo kitu ambacho kinatufanya tuwe makini zaidi dhidi ya Simba.

Walicheza vizuri sana hiyo inaashiria benchi la ufundi linafanya kasi nzuri.

Ina wachezaji wazuri wa kigeni, Luis ni mchezaji mzuri nilimsajili kutoka Msumbiji wakati nikiwa Mamelodi na tukamtoa kwa mkopo kuja Simba, ni mchezaji muhimu

Claotus ni mchezaji anayependa kucheza mpira, tulikutana naye wakati anachezea Zesco, ni mchezaji mzuri

Washambuliaji ni wazuri, mchezaji namba 7 [Mugalu] halafu wana mchezaji mkongwe namba 14 [Kagere] ni top player na kuna kiungo mwingine wa Zambia [Bwalya]".
 
hebu toa bange zako, Simba haiwakilishi Taifa, inajiwakilisha yenyewe, Taifa linawakilishwa na timu ya Taifa tu.
Wawakilishi wa TANZANIA michuano ya Kimataifa ni Simba SC na Namungo FC

Simba michuano ya kombe la Mabingwa Afrika na Namungo ni kombe la Shirikisho Afrika hivyo kama timu yako haipo kimataifa basi Timu yako ni tia maji tia maji.
 
Acha nitoe utabiri wangu bado mapema wa kikosi Cha Simba Vs Al Ahly:

1. Aishi Manula
2. Shomary Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Paschal Wawa
5. Joash Onyango
6. Peter Muduhwa/Erasto Nyoni
7. Luis Miquissone
8. Thadeo Lwanga
9. Chriss Mugalu
10. Lary Bwalya
11. Clotas Chama

Formation 3:4:2:1

Huu mfumo ni mzuri wa kuwa na mabeki watatu nyuma Timu inakuwa na uwiano mzuri wa kushambulia na kuzuia rejea mechi ya Simba Vs Platinum pale kwa Mkaba...
 
WanaSimba wote tulioko Tanga, Morogoro, Pwani na Daaaslam pls pls Jumanne inakrbia na Kiingilio ni Elfu 3 tu. Tujitokeze kwa Wingi kabisaaa, tujitahidi pia tuvae MASK ili kujikinga na maambukizi ya Magonjwa ya Mfumo wa Hewa.

Siku ya Jumanne tuliamshe Shangwe kama lote, tuwape Hamasa Vijana wetu.

SIMBA NGUVU MOJA DAIMA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom