Kuelekea Klabu Bingwa Afrika | Simba SC dhidi ya As Vita Club Tunaendelea Tulipoishia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mabingwa wa Nchi, Mnyama Mkali, Simba SC, imepania kuendelea ilipoishia kwa kuendeleza ushindi dhidi AS Vita Club katika hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, mchezo ambao utapigwa Jumamosi ya Machi 3, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Hakuna namna, Simba SC inahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kuweza kujihakikishia kufuzu hatua ya robo fainali katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amesema kuwa timu ipo tayari kusaka alama tatu katika mchezo huo.

"Kesho lazima tupate matokeo ya ushindi ili tuweze kusonga mbele, tumejipanga kupata matokeo.

Tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa, wote wapo kambini na hilo linatupa mwanga kuwa tunaweza kufanya vizuri". Amsema Matola.

Naye Nahodha wa Simba SC John Bocco amesema wamefanya maandalizi mazuri kuwakabili AS Vita Club

"Kwa upande wetu kama wachezaji tupo vizuri, tuna ari nzuri kuweza kupambana ili kufikia malengo ya timu yetu

Tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini Mungu atatusaidia na tutafuzu hatua ya robo fainali. Tuna wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaoelewa kwanini wapo kwenye klabu. Tupo tayari". Amesema Bocco.

Nini maoni yako kuhusu kauli ya Kocha Msaidizi Matola wa Simba SC na vile vile Nahodha John Bocco.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Kumbuka Mdau mtanange huu wa Wababe wa soka Afrika ni kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose Ukasimuliwa.

FB_IMG_1617384804385.jpg
 
Hii mechi nimeiota.. Simba tutatanguliwa goli moja. Tutakuja kuchomoka dakika za mwisho mwisho na kuongeza lingine dakika za lala majeruhi..
Umeota kama ilivyotokea kwa Nkana FC na As Vita michuano iliyopita kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
 
Hii mechi nimeiota.. Simba tutatanguliwa goli moja. Tutakuja kuchomoka dakika za mwisho mwisho na kuongeza lingine dakika za lala majeruhi..
Mimi nimeota Simba kapigwa moja,baadae Simba wakarudisha mechi ikaisha draw ya moja moja.
 
Back
Top Bottom