Kuelekea katiba mpya, ni vema tukajikumbusha sababu zilizokwamisha mchakato huo awamu ya 4

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
Wakuu
Kwa Tanzania ya sasa, uhitaji wa kufanya mabadiliko kwa katiba ya Tanzania hayaepukiki

Mchakato wa katiba mpya ulianzishwa na Kikwete tangu 2011 lakini ulikuja kufail hatua za mwisho

Ni vema sie Watanzania tukajikumbusha na kutambua changamoto na vikwazo vilivyofelisha mabadiliko ya katiba mpya

Nakumbuka moja ya sababu za kufeli kwa mabadiliko hayo ni toauti za kiitikadi zilizotofautikiana kutokana na vyama vya kisiasa tanzania hadi kupelekea wabunge wa upinzani kususia mchakato

Pili ni tofauti za kimtazamo juu ya Serikali ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar
Hii nahisi ndio kilikuwa kiini cha kuvunjika kwa mchakato mzima

Ni rai yangu kwa watazania sasa tujitafakari dhidi ya zile sbabu zilizokwamisha mabadiliko ya katibzma, je yumekomaa vilivyo kuweza kuhimili vikwazo hivyo?

Unaweza share sababu kinzani hapa zinazokwamisha katiba mpya tuzitathimini
 
Kitendo cha ukawa kujitoa kwenye mjadala wa katiba mpya kilikwamisha mchakato. Kwa maoni yangu kujitoa kwenye majadiliano muhimu kama ya katiba haikua njia mzuri. Swali, je mjadala wa katiba mpya ukianza upya ukawa hawatajitoa au kujiziba midomo kwa vitambaa/karatasi mbele ya makamera ya wanahabari?
 
Mkuu inatakiwa tujiulize nini chanzo cha UKAWA kususia mjadala wa katiba mpya?

Ukilijua hilo utakua umepata sababu za kufeli katiba mpya na sio ukawa kususia
 
UKAWA tuje na hii slogan:

Pigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa tupate tume huru bila kuandamana, virungu wala mabomu ya machozi mengine tutarekebisha tukiwa madarakani.

Kwa slogan kama hiyo najua watatukejeli lakini 2020 watagundua tuliona mbali.

Advantages:

1.Tutakuwa na tume huru

2.Matokeo ya uraisi kupingwa mahakamani.

3.Sheria ya uchaguzi kubadilishwa

4.Mshindi wa uraisi kupata asilimia zaidi ya 50(kipengele hiki sina uhakika sana kama kilipitishwa na kuweka katika katiba inayopendekezwa)

Narudia watatubeza sana ila sisi tusijali bali tukumbuke huu msemo wa kingereza:

"the end justifies the means".

Tukiingia madarakani au kupata wabunge wengi katiba halisi ya mzee Warioba itapatikana.

Tuwe flexible katika hili na zaidi tuwe na foresight.

Tukijidai wabishi huku tumeshindwa kushinikiza tume huru wala kupata katiba ya mzee Warioba na huku hatuko tayari kuandamana kudai Tume huru basi tujiandae kulalamika kuibiwa kura 2020.
 
Kitendo cha ukawa kujitoa kwenye mjadala wa katiba mpya kilikwamisha mchakato. Kwa maoni yangu kujitoa kwenye majadiliano muhimu kama ya katiba haikua njia mzuri. Swali, je mjadala wa katiba mpya ukianza upya ukawa hawatajitoa au kujiziba midomo kwa vitambaa/karatasi mbele ya makamera ya wanahabari?
Mkiti: Kuilaumu UKAWA pekee bila kukumbuka matukio halisi yaliyosababisha hata hao UKAWA kujitoa itakuwa sawa na kujificha kwenye usemi wa "mbuni kufukia kichwa chake mchangani huku kiwili-wili chote kikiwa wazi!" Hapo tayari utakuwa umejiweka kwenye upande moja wa itikadi za siasa za Tanzania. Mapendekezo halisi ya Katiba Mpya ni yale yaliyofanywa na Tume iliyoongozwa na Jaji Warioba. Ukweli upo hapo. Baadhi ya mapendekezo ya Tume yalikuwa yanaathiri nafasi ya wajumbe wengi tu wa Bunge la Katiba hivyo zoezi zima likavurugika. Katika moja ya mambo mazuri sana aliyoyafanya Raisi wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Kikwete (Raisi Mstaafu), ni kuteua Tume makini sana. Tungeisikiliza Tume hiyo, tukaipa mapendekezo machache tu ya kufanya kwenye Rasimu ya Pili, ingetosha kabisa kutupatia Katiba ambayo ni nzuri. Ikumbukwe kuwa haitakuja kutokea tukapata "a perfect Cosntitution" (Katiba sahihi sana) na ya kumridhisha kila Matanzania. Mimi siammini hivyo, hayo ndiyo maoni yangu.
 
1. Sheria ya Manailiko ya Katiba ndio kikwazo!!!!
3. Kazi ile ilipaswa kyfanywa na time huri tu!! Ambayo haitokani na chachu ya siasa, na wajumbe wake ealipaswa kuapa, wao na familia zao, kutoihisisha na siasa kwa kipindi kisichopungua miaka kumi.
3. Siasa za maji taka zoizopo Bongo hszituhusu maendeleo y kueleweka.
 
Wakuu
Kwa Tanzania ya sasa, uhitaji wa kufanya mabadiliko kwa katiba ya Tanzania hayaepukiki

Mchakato wa katiba mpya ulianzishwa na Kikwete tangu 2011 lakini ulikuja kufail hatua za mwisho

Ni vema sie Watanzania tukajikumbusha na kutambua changamoto na vikwazo vilivyofelisha mabadiliko ya katiba mpya

Nakumbuka moja ya sababu za kufeli kwa mabadiliko hayo ni toauti za kiitikadi zilizotofautikiana kutokana na vyama vya kisiasa tanzania hadi kupelekea wabunge wa upinzani kususia mchakato

Pili ni tofauti za kimtazamo juu ya Serikali ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar
Hii nahisi ndio kilikuwa kiini cha kuvunjika kwa mchakato mzima

Ni rai yangu kwa watazania sasa tujitafakari dhidi ya zile sbabu zilizokwamisha mabadiliko ya katibzma, je yumekomaa vilivyo kuweza kuhimili vikwazo hivyo?

Unaweza share sababu kinzani hapa zinazokwamisha katiba mpya tuzitathimini
  • Mchakato wa katiba umekwama baada ya kukosekana kwa maridhiano baina ya wanasiasa kuhusu muundo wa muungano
  • CCM wanataka Serikari mbili, UKAWA wanataka Serikari tatu
  • Miundo ambayo haina hata tija ukilinganisha na muundo wa Serikari moja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom