Kuelekea hatua Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC dhidi ya Al Ahly SC 'Hatushindwi'

FlashBack Klabu Bingwa Afrika 1984/1985; Simba SC waliwachapa National Al Ahly mabao 2-1 kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ukiwa ni mchezo wa kwanza.

Magoli ya Simba yaliwekwa kimiani na Streika Matata Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' akipokea pasi safi kutoka kwa Malota Soma Ball Juggler na bao la pili lilifungwa na Mtemi Ramadhan akipokea pasi safi ya Zamoyoni Mogella


Kila la heri Mnyama Mkali..Ushindi ndo lengo letu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ni kweli Zamoyoni Mogera na Malota soma walicheza zile enzi za 80’s sio 90’s kama nijuavyo mimi
 
Kutoka moyoni kabisa sina chochote nachotegemea kwenye hii mechi.

Namwomba tu Mungu iwe kama impendezavyo, maana nikimwomba eti tushinde ni kama namshinikiza.

Daaah! Kwa huo mstari wacha tuishie hapo. Maana nimejikuta nayavaa haya maneno kama nimeyaandika mie. 👏👏👏👏

Ila niseme yawapasa muwe na mawazo haya kwenye kila mechi na hata ile ya Jumamosi Feb 16. Teh teh. 😀😀
 
Daaah! Kwa huo mstari wacha tuishie hapo. Maana nimejikuta nayavaa haya maneno kama nimeyaandika mie. 👏👏👏👏

Ila niseme yawapasa muwe na mawazo haya kwenye kila mechi na hata ile ya Jumamosi Feb 16. Teh teh. 😀😀

Mungu wetu ni wa ajabu, anawezesha mahali ambapo kwa akili zetu tunaona haiwezekani.

Hiyo ya Jumamosi Feb 16 hayo mawazo yatakuwa yenu, sisi siku hiyo ni kurudisha heshima nyumbani.
 
Vyura wanajifariji kubishana na club kubwa Tanzania, juzi niliangalia mechi ya omba omba na JKT aisee yanga sio timu kabisa ina wabutuaji tu

Ukibisha sana, tukutane 16 na kilaza wenu kindoki mtakula 10
 
Uuwiiii. Hivyo anaweza akawezesha mkamfunga mwarabu. Duuuh. 😀😀😀

Haya bana. Ila jiandae kiasikolojia hasa ifikapo 16:00Hrs.

Katika matukio ya kimpira yaliyokuwa ya kimaajabu ni pamoja na Yanga kutoka 0 - 0 na Simba, maana alitegemewa kuchakazwa.

Kwa hiyo kwake Mungu kila kitu kinawezekana.
 
Hahahahah
IMG-20190212-WA0000.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo ndio leo jamaani. Wale Waarabu Koko wenzangu tujumuikeni kwa pamoja kuwapa Support Waarabu wenzetu kwa Mchina.

Nifah uko wapi Mwarabu Koko mwenzangu.
Hapa Cairo tumechinja ngamia ndio tunachoma tunasubiri saa kumi tule pamoja na mvinyo ambao umekaa wiki mbili

Sent from my TECNO K7 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom