Kuelekea harakati za ukombozi,dini ni adui wa mwisho anayepaswa kuangamizwa haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea harakati za ukombozi,dini ni adui wa mwisho anayepaswa kuangamizwa haraka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by only83, Jan 23, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Katika karne ya 15-19 wakati wakoloni wanaingia barani afrika mbinu mbalimbali zilitumika ili kufanikisha mbinu zao chafu za kutawala Afrika na makoloni yao mengine.Mbinu kama elimu,dini,lugha,malI nk vilitumika kama mbinu ya kuwagawa waafrika na kwa kweli walifanikiwa sana.

  Katika karne ya 18 baada ya Berlin Conference mbinu zilizopangwa na kila mkoloni kupewa malengo ya kutimiza ni kuhakikisha unatawala kweli kweli.Kwa kweli dini ilitumika sana,baada ya kuingiza dini ya ukristo na uislamu wale waumini waliambiwa "msishirikiane na wale makafiri maana ni mashetani" Oh!!

  Na kweli wakristo kwa waislamu wakawatenga wenzao na mzungu akawatawala kweli kweli tena kwa mateso makali,na wale wakristo mfano walipewa vi-biskuti na vi-nguo toka ulaya ili kuweza kubakia kuwa ndani ya ukristo.

  Elimu pia ilitumika sana,mfano baada ya watoto wa machifu na wale wa koo za machifu kupewa vi-elimu vya kizungu wakawa wanaongea kiingereza na hapo wakaambiwa msichangamane na wale maana ni watu wasiostaarabika lol!! Kwa kweli kwa haya mawili nawapa hongera wazungu na wakoloni kwa ujumla maana walifanikiwa sana na hata harakati za ukombozi ziliafifishwa kwasababu ya hili.

  Ki ukweli dini na elimu,hasa dini ni vitu vizuri sana,maana vinatuagiza kumtambua Mungu muumbaji,na kuishi kwa umoja na undugu…mfano Biblia inasema "Mtu akisema anampenda Mungu wakati anamchukia ndugu yake,huyo mtu kweli haimo ndani yake"

  Kwanini nimeandika haya;

  Katika miaka ya karibuni hasa kuanzia miaka ya 2000 kumekuwa na kuibuka kwa hoja kama ile ya wakoloni kuwa mtu ukiwa na elimu na dini na hasa dini tofauti na mwenzako hupaswi kushirikiana nae.Na mbaya zaidi siasa za Tanzania kwasasa zimetawaliwa na dini na udini,si ajabu kusikia shehe mmoja akisema hii nchi inatawaliwa na wakristo au kusikia Mchungaji au askofu mmoja anasema JK kajaza waislamu wengi kwenye safu za juu za wasaidizi wake.Au si ajabu kusikia mtu anasema mwaka 2015 ni zamu ya wakristo kutoa raisi.Au si ajabu kusikia mtu anasema CDM ni chama cha wakristo au CUF ni chama cha waislamu nk…

  Ndugu zangu tunapoendelea na michakato ya harakati zaukombozi tunapaswa kujua kuwa dini ni adui wa mwisho anayepaswa kuangamizwa.Mwalimu Nyerere aliwai sema "Kuingelea na kuutukuza udini na ukabila ni kujichimbia kaburi na mwanasiasa au mtu anayeongelea mambo haya ni dalili ya kufilisika kwa hoja"

  Na wanasiasa wetu baada ya kutambua nguvu ya dini kwenye hisia za binadamu wameanza kutumia kama silaha ya kusambaratisha umoja wa watanzania ili wasidai haki zao za msingi..

  Muislamu akidai haki yake anaambiwa ni kwasababu ya wakristo ndio maana hupati haki hii, vile vile kwa wakristo.Dhana hii imeanza kumong'onyoa nguvu na umoja wa watanzania,si ajabu kumsikia muislamu akisema bora aendelea JK kuwa raisi japo maisha ni magumu..kuna viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanaambiwa kuwa wasihitishe migomo na maandamano maana mambo haya ni mpango wa wakristo kuuangusha utawala wa JK.

  Hii dhana inatumaliza watanzania, nawahasa kama kweli tunataka ushindi dhidi ya dhuluma na mateso toka kwa watawala wetu wa sasa,DINI NI ADUI WA MWISHO ANAYEPASWA KUANGAMIZWA….
   
 2. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mkuu;hapo kwenye red sijakuelewa...kuangamiza dini au udini;ufafanuzi please;then tuendelee
   
 3. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Ndeeeefu kwelikweli but finally nimemaliza kuisoma ila ndugu yangu hapo ni sawa na kushauri kuwa katika harakati za kusafisha shamba tun`goe mpaka mti unaotambulisha mipaka ya shamba letu? No man no. Kwa nionavyo mimi kama sio sisi nikuwa kama kuna mtu wa kumheshimu ni huyo aliyeleta DINI hebu fikiri haraka haraka ulimwengu bila dini
   
 4. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hata YESU hakuanzisha dini alifundisha upendo.
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Dini hazina shida;bali kutumia udini kama silaha ya kupendelea watu na kutetea uongozi mbovu!
   
 6. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Fikra mgando!
   
Loading...