Kuelekea eid el fitr, jeshi la polisi latoa tahadhari kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea eid el fitr, jeshi la polisi latoa tahadhari kwa wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gudboy, Sep 17, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jeshi la polisi nchini limewatahadharisha wananchi katika maeneo mbalimbali kujihadhari na vitendo vya kihalifu na wahalifu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye siku kuu ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

  Tahadhari hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi
  Abdallah Mssika, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.

  Kamanda Mssika amesema kuwa uzoefu umeonyesha kuwa mara nyingi wananchi wa dini zote wamekuwa wakisherehekea siku hii kwa shamra shamra mbalimbali ukiwemo unywaji wa pombe kupita kiasi na wengine kuthubutu kuendesha magari kwa mwendo kasi na kupelekea ajali.


  Amesema kuwa kutokana na uzoefu huo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi mbalimbali wakiwemo walezi na wazazi, kutowaacha watoto wadogo pasipo na uwangalizi wa watu wazima ili kuepuka kugongwa na magari ama kuzama majini wakati kwenye fukwe za bahari na maziwa ama mabwawa.
  Aidha wazazi na walezi wasiache nyumba zao bila uangalizi wa kutosha na pia kuepuka kuwaruhusu watoto wadogo kwenda kujazana kwenye kumbi za starehe kwa kuhofia kukosa hewa na kufariki dunia.


  Kamanda Mssika amewatoa hofu wananchi na kusema kuwa watakuwa salama mwanzo hadi mwisho wa siku kuu hiyo na kwamba Jeshi hilo kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi wataimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mijini na sehemu za kufanyia ibada na burudani na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu..


  Amesema kuwa Jeshi hilo litatumia askari wake wa miguu, magari, Mbwa na Farasi katika kufanya doria kwenye maeneo korofi kwa lengo la kuwahakikishia wananchi usalama wao pamoja na mali.


  Hata hivyo Jeshi la Polisi linawakumbusha wafanyabiashara kuepuka kusafirisha fedha nyingi kwa wakati mmoja kutoka eneo moja hadi lingine lakini ikiwa ni lazima kufanya hivyo wanashauriwa kutoa taarifa kwa wakuu wa Polisi ili kupatiwa askari wa kuwasindikiza ili fedha zao ziwe salama.


  Kwa upande wa Walinzi wa majengo ya viwanda, ofisi na maghala ya kuhifadhia mali na bidhaa mbalimbali zikiwemo za madukani wametakiwa kujiepusha na vishawishi vya kufadhiliwa vyakula na vinywaji kutoka kwa watu wasiowafahamu wawapo kwenye malindo yao ili kuepuka kupewa sumu ama madawa ya kulevya na kuibiwa.


  Amewataka pia Madereva wa magari ya abiria na madereva wa Taxi kujiepushe na mambo ya ulevi na kwenda mwendo wa kasi ambao unaweza kusababisha ajali za barabarani. Pia abiria wa magari hayo a wanatakiwa kutoa taarifa kwa askari wa usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili kwa kukiuka mashariti ya udereva.


  Aidha amewakumbusha pia wamiliki na madereva wa magari madogo waepuke kutoa lifti kwa watu wasiowafahamu ili kuepuka kuporwa magari na kusababisha hasara kwa wamiliki wake.


  Amesema kuwa pamoja na uchache wa skari wa Jeshi hili hapa nchini, Jeshi hilo limejipanga kuwashirikisha wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuimarisha doria na kufanya kwa pamoja katika kuwahakikishia wananchi usalama wao.

   
 2. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa tahadhari hiyo sawa ila je wananchi wakitaka kupiga simu ya Emergency 112 inapatikana? Mara nyingi inaita tu bila kupokelewa. Anasemaje afande Msika kuhusu hilo?
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  .

  Hivi ni kweli siku hizi watu wanalewa sana siku ya eid?. na vipi viwanja vya watoto kucheza sikikuu vipo huko Bara? na vipi Znz viwanja vya baraza la wawakilishi na Foro vipo?
   
 4. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kuhusu hilo watu wasiwe na wasi wasi zitakuwa hwani na pia kuna zile ambazo makanda walitoa pia, kwa hiyo zote zitafanya kazi sio siku hiyo tu bali ni kila siku, kama una taarifa zozote tafadhali zitumie kufanya mawasiliano
   
Loading...