Kuelekea CC ya CCM mpaka NEC, nani kumrithi Kinana, Nape na sekretarieti kwa ujumla?

amina ngalo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
309
170
Mpaka sasa wapo ambao walishatajwa au kuhisiwa kwenye bàadhi ya nafasi

1.Nafasi ya Katibu Kkuu wanaotajwa ni
RC Anthony Mtaka
Abdallah Bulembo
RC Aggrey Mwanry

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu
Alhaj Kundya
Anna Kilango
Halima Mamuya

Nafasi ya mwenezi wa taifa
Livingston Lusinde
Haji Manara
Jerry Muro
Mary Piusi Chatanda

Mchumi wa Taifa
Egla Mwamoto
Enosi Mafuru
Lazaro Nyalandu

Katibu wa itikadi na mambo ya nje
Bernard k.Membe
Said Mwambungu
Suleimani Serera

Kuelekea kamati kuu ya chama tawala kwenye pita pita zangu nimeyasikia hayo.
 
Mabadiliko makubwa yanakuja CCM ambapo Dr. Bashiru Ally anatarajiwa kumrithi Kinana. Pamoja na Dr. Bashiru mwingine anayetajwa ni Mwigulu Nchemba.

Hatua hii inakuja baada ya Kinana kuandika barua ya kupumnzika. Na baadhi ya vigogo wa chama hicho kuteuliwa kuwa mabalozi.

Vile vile wanaotajwa ni Humphrey Polepole katika nafasi ya Uenezi. Makonda katika nafasi ya uenezi. Makongoro Nyerere katika nafasi ya Naibu katibu mkuu Bara. Na Zahoro katika nafasi ya naibu katibu mkuu Zanzibar..
 
Mbona nasikia Makonda alikuwa kwenye oral intavyuu juzi hapo Dar es salaam ili apate uenezi wa chama Taifa?

Hivi mnadhani alikuwa anatembea hivihivi?
kuna watu walikuwa wamekaa wanatoa maksi,sasa sijui kama atafaulu
 
Nimeipenda ya Bashir Ally, pole pole na Makongo ro Nyerere pia Kibajaj na wakubali sana hawa watu kupambana na chadomoo iliyoshindwa.
 
Polepole apewe Uenezi, ataitendea haki.
Hichi chama kiwe makini waombe busara za ziada kutoka kwa Comrade A. Kinana. Huyu bwana alitufaa sana kichama. Ukimteua mtu kama Mkama, Bulembo au Nchemba ni kukaribisha matatizo mengine kwenye chama. Anayetufaa pengine January Makamba na Lukuvi. Makamba ni kijana msomi. Lukuvi ......

Kunahitajika watu wa aina ya Kinana kinachofanyika sasa ndani ya chama ni kuweka watu wangu wakunijenga na siyo kutujenga sisi kama taasisi. Chama ni sisi, sisi ndiyo Chama.

Itakavyokuwa tutegemee kurudi nyuma kiutendaji kama chama tusipowekeza kwa watu makini. Ikitokea kuwa hivyo tutegemee kupanda mlima mrefu kweli. Tuhakikishe pia kwamba uchumi unakuwa kwa kasi na kuwahakikishia wananchi maisha bora, isipokuwa hivyo tutegemee kupanda mlima mkali zaidi tutao jasho jingi lisipotoka tutegemee kukukwama.
 
Change,Karamagi,Diallo, wanatoka kanda yetu lazima tuwape nafasi za juu kaskazini,Pwani na Kusini mtaisoma namba.
 
NANI MR BULE MHH MSINIKUMBUSHE KAMPENI ZILIZOPITA KWANZA AANZE KUTUBU KWA MOLA WAKE.MANENO YAKE YALIJAA KASHFA.
 
Bavicha naona mnapiga ramli tu hapa, mnajifariji na mambo yenu yaliyowashinda!
 
Kwa mabadiliko yanayotarajiwa kufanyika ndani CCM.
Kunauwezekano mkubwa Nape Nauye kuvaa viatu vya Abdrahman Kinana, huyu kada wa chama anakila aina ya sifa kuchukua nafasi hiyo.
Nape amefanya kazi kwa karibu na Katibu mkuu Kinana kwa muda wa miaka zaidi ya mitatu. Nape anasifa ya kupambana na ufisadi ndani ya CCM haswa alipokuwa umoja wa vijana alipambana vikali kuhusu ule mradi wa jengo la umoja wa vijana.
Mwenyekiti wa CCM John Magufuli anataka kuleta mabadiliko makubwa ndani ya chama kwa Kuwaondoa wazee na nafasi hizo kujazwa na vijana ili chama kiende na wakati.
 
Back
Top Bottom