Kuelekea 2020, maandalizi duni ya vyama vya upinzani, fursa nzuri kwa CCM kuchukua dola

Dankbar

Member
Jul 11, 2015
98
113
Ni mwaka wa pili sasa tangu uchaguzi ufanyika na katika kuelekea 2020. Baada ya uchaguzi 2015 ambao ulikuwa na hamasa kubwa, chama cha ccm kupitia mgombea wake Magu kilishinda hali kadhalika viti vingi vya ubunge na udiwani. Tofauti na chaguzi zingine, upinzani ulionekana kukubalika sana mijini hasa katika majiji na kushuhudia viti vingi vya ubunge na udiwani kuchukuliwa na upinzani.

Baadhi ya Sababu za upinzani kushindwa kuchukua dola kwa Kadiri ya maoni na mtanzamo wa upande wa wapinzani:

1. Kura ziliibibiwa: Tulishinda ila kura ziliibiwa
2. Kutokuwa na tume huru ya uchaguzi
3. uchaguzi kutawaliwa na rushwa na hujuma
4. Wapiga kura kutishwa na vyombo vya dola (polisi)
Kama upo upande huu ongeza sababu unazozifahamu

Upande wa ccm:

1. Wananchi bado wana imani na ccm
2. ccm inatekeleza ahadi zake
3. hazina kubwa ya wanachama
4. Imani kubwa waliyokuwa nayo wananchi kwa Magufuli
ongeza sababu unazozifahamu

Wasio wanachama wa chama chochote:

1. ccm kuwa na hazina kubwa ya wapiga kura hasa vijijini, upande mwingine upinzani kutokuwa ushawishi na wanachma vijijini ambako ndiko wapiga kura ni wengi.

2. upinzani kuto kuwa na sera mbadala ambazo ziligusa mojakwamoja hujuma na mateso kwa wananchi zilizosababishwa na ccm baada ya ajenga ya ufisadi kuyeyuka

3. kutokuwa na tume huru ya uchaguzi

4. Kupokelewa kwa Lowasa licha ya tuhuma zake, kuondoka kwa Dr. Slaa na iman ya wananchi kwa Magufuli
ongeza sababu zingine unazozifahamu

Nini kinafanyika kuelekea 2019/2020
1. Upinzani ulianza kwa kutafuta namna ya kugomea matokea lakini kwa vile matokeo yalikuwa yanalindwa na katiba mbovu, nguvu na jitihada hazikuzaa matunda

2. Baadaye ilikuja hatua ya kutaka kuzunguka nchi nzima kwa ajenda ya kushukuru lakini nyuma kukiwa na lengo kuwasadikisha watanzania kuwa upinzani ulishinda hata hivyo utawala wenye Kila dalili ya udikiteta ukapiga marufuku bila kujali ni kinyume cha katiba.

3. Sasa imekuja hatua ya kupinga na kutafuta kasoro kwa chochote kinachofanywa na utawala huu, ukiambatana na matamko yasiyotekelezeka ikiwamo UKUTA na KATAFUNUA

Mbinu inayotumiwa na utawala sasa:

1. Kuzuia jitihada yoyote inayofanywa na upinzani ili kujitangaza kwa watanzania hasa wanyonge na waishio vijijini ambao ndiyo wapiga kura wengi
2. Kutekeleza baadhi ya ahadi na kuweka jitihada kubwa katika kuweka matangazo sambamba na utekelezaji wa ahadi hizo lakini pia kwa vile wafanyakati wengi na wasomi wameonesha kuchoshwa na ccm, utawala huu unaweka akiba ya kutekeleza baadhi ya ahadi kuelekea uchaguzi ili ziwaguse kweli wananchi, ikiwamo mil 50 vijijini na hivyo kumaliza kabisa nguvu ya upinzani.
3. Kutengeneza matukio ambayo wapinzani wanatumia muda mwingi kujadili na kupingana nayo badala ya kujenga chama na kutengeneza sera mbadala.

Maoni yangu, ili kuleta hamasa na kuwa na upinzani imara, ushauri wa Lowasa kuhusu sifa ya chama cha Siasa na chama cha Kiharakati sio ya kupuuzwa.

1. Vikao vya vyama vya upinzani vilenge kutengeneza sera zitakazokuwa mbadala wa sera mbovu za ccm badala ya kuwa vikao vya kutengeneza matamko ya kupinga
Kuwa na sera ambazo zitagusa watu kama ilivyokuwa Ufisadi ambayo sio ajenda tena. Mfano utaratibu wa huduma ya afya hususani bima ya afya kwa wananchi wa kawaida n.k

2. Kwa vile asilimia kubwa wanaamini pasipo tume huru ya uchaguzi hakuna ushindi kwa upinzani, sasa ingekuwa kitu cha kukipigania kupitia wabunge waliopo, hata kama sio kupata Katiba mpya, walao kurekebisha vipengele muhimu vikiwemo: Tume huru ya uchaguzi na kuruhusu matokeo kuhojiwa baada ya kutazwa

3. Kuelekeza nguvu kubwa kwenye matawi badala ya kuelekeza katika kutetea viongozi na vikao vya juu ambavyo vinakuwa kwa ajili ya matamko.

4. Kudai haki ya Kikatiba mahakamani kufanya mikutano ya siasa kwavile hakuna aliye juu ya katiba

5. Kujenga demokrasia katika vyama kuelekea uchaguzi hasa namana ya kuwapata wagombea badala ya mtu mmoja kujihakikishia atashinda kwa kuwa alishinda ila matokeo yaliibiwa, kauli ambayo kwa wananchi wa kawaida ambao ni wengi haiieleweki.

Ongeza maoni
 
Pole sana mkuu, mchukue dola kutoka wapi labda?
Si mmekataa mikutano ya hadhara? wenzenu wanafanyia chumbani...... the game is tough than ever..... its about time...
 
Back
Top Bottom