Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Kwa sasa ninaamini asilimia kubwa ya watanzania wanapata habari za kina za nini kinaendelea katika nchi hii kupitia mitandao na si vyombo rasimi vya habari kama magazeti na television hasa juu ya yale mambo ambayo si mazuri kusikia au kuonekana machoni mwa watu.
Vile vile,ni kupitia mitandao hii, watu wanasikia kupitia clip zinazosambazwa mitandaoni matamshi ya baadhi ya wanasiasa, matamshi ambayo media ama zinakwepa kuyaandika au kuandika huku wakiacha baadhi ya maneno(wakichuja) lakini mitandaoni clip zinasambaa kama zilivyo bila kujali uliongea au kuropoka nini(hakuna kinachofichwa).
Pia,ni kupitia mitandao hii, propaganda zote za wanasiasa wa awamu hii zinajibiwa,kuchambuliwa na kutolewa ufafanuzi unaosaidia watu kuelewa/kuchambua pumba na mchele.
Kwa kifupi,mitandao kwa sasa ndio inasaidia watanzania kujua yale yanayofichwa pamoja na yale yanayopotoshwa hivyo nina kila sababu ya kuamini asilimia kubwa ya watu wenye access na internet mpaka kufikia 2020, watakuwa na ufahamu na uelewa wa kutosha juu ya namna mambo yanavyokwenda katika nchi yao kwa sasa na iwapo mambo haya(utekaji,unyanyasaji wa raia,watu kupotea,kauli za viburi na kejeli za baadhi ya wanasiasa,utendaji wa wabunge na Bunge lenyewe ,n.k) yataendelea kutokea kila siku,binafsi sioni uwezekana wa wagombea wengi wa CCM kupigiwa kura za ndio na watanzania walioa na access na internet kupitia simu zao za mikononi,kompyuta mpakato(laptop,n.k).
Nasema haya kwasababu,ukiacha matendo na kauli za wanasiasa mmoja mmoja,CCM ndio chama tawala kinachounda serikali hivyo wao na chama chao na wagombea wao ndio watakaobeba lawama na kuwajibishwa na wapiga kura kupitia sanduku la kura.
Naelewa tume si huru, ila maamuzi ya wananchi watayaona kupitia kura zao bila kujali nani anatangazwa mshindi(ukweli watauona kwenye ballot papers na wataelezeana).