Kuelekea 2015 CHADEMA wana kazi kubwa ya kufanya kuliko wapinzani wao CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea 2015 CHADEMA wana kazi kubwa ya kufanya kuliko wapinzani wao CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Oct 23, 2012.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunaelekea 2015 kwa matumani lakini pia tukiwa katika lindi la kukata tamaa. Mambo haya mawili yako katika mioyo ya Watanzania vijana, wazee, akinamama, watoto na marafiki zetu wa n'gambo.

  Watanzania wana matumaini kwa sababu wanahisi kuzidi kujikaanga kwa CCM katika matukio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na pengine hata the vacuum in leadership we witness today ni matakwa yake Mola ili wananchi waichukie na hatimae waamue kupigia kura za chuki za kuikataa hata kama chaguo mbadala halipo.

  Tunatofauti katika mitizamo na hakuna asemaye mtizamo moja ni sahihi kuliko mwingine ingawa matendo ya msimamo mmoja na tabia/personalities za exponent huleta tofauti tunayoitaka. Kuna watu wanasema ukisikia mzigo mzito bila kujali uzuri wa mzigo huu utuwe haraka kwani madhara yakekama utaendelea kuuweka kichwani ni makubwa ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutwaa uhai wako. Kwa msingi huu mawazo ya shule hii ni kwamba tuipigie CCM kura ya kuikataa ili tuweke mazingira ya kuleta mabadiliko tunayoyahitaji ikiwa ni pamoja na kukibadili chama chenyewe kitakachoidadili CCM na kwamba hoja yoyote kinyume na mtizamo huu ni kurudisha juhudi za umma nyuma. Mtizamo mwingine wanaona hii ni sawa na kujiandalia ghasia, kwao wanaona kwanza tujiandae kimuundo, kisera na kimawazo ili tuonyeshe umma pasi na shaka kuwa tunatosha kuwa mbadala. Nakubaliana na mfumo huu wa mawazo kwani kama huwezi kuonyesha kuwa unatosha katika ngazi ya chama utawezaji kupewa dhamana ya kuongoza taasisi ambayo muundo wake ni complex kama serikali.

  Kimsingi Mungu yupo upande wa Watanzania wa kawaida na amesikia kilio chao anajua wanapambana na Goliati lakini amewawekea mikono yake na inavyoonekana mwanga wa mabadiliko unakuja. Ndugu zangu Watanzania nataka kuwaasa kuwa CDM ni tumaini la watanzania katika hali ya wakati mgumu waliyonayo sasa ambapo uongozi katika nchi yetu ni biashara na wapiga kura maskini wanasema nipe changu mapema kwani hata ukipata uongozi ni kwa manufaa ya familia yako na si kwake maskini. Matajiri wanasema kwa kuwa umeniuzia kura usiniulize juu ya maisha yako.


  Matatizo yanayoikabili nchi yetu ni makubwa na yanatosha kujinadi yenyewe mbele ya watu ili mabadiliko yawezekane. Matatizo yetu ya msingi yapo mengi lakini yote yamezalishwa na tatizo moja kuu la Utupu/vacuum katika uongozi na matokeo yake ni nchi kukosa ivpaumbele na usimamizi wa rasilimali zetu ili tujitegemee kwa maendeleo yetu. Chadema wako kimya juu ya urejeshwaji wa maadili ya uongozi katika nchi hii ambayo ndiyo kinga kuu ya uwajibikaji na uadilifu.

  Watu wengine watanipinga kuwa nchii hii inavyovipaumbele na watadiriki kuvitaja kama elimu, Kilimo, afya nk yalaaaaa! vipaumbele vya nchi si kwa kutaja bali vinaonekana katika mipango na mikati na utekelezaji. Ipi ni mikakati ya elimu bora katika Tanzania, ipi ni mikakati ya kilimo bora na chenye tija Tanzania, ipi ni mikakati ya afya bora, kupeleka wagonjwa wengi india, viongozi kupeleka watoto wao kusoma ng'ambo. Mpishi gani anatamba yeye ni mpishi bora wakati chakula akipikacho hali yeye na familia yake. Anapika akimaliza anaoga nakujikwatua yeye na familia yake anaenda kula Serena. CDM lazima kila anayekubali kupika chakula kwa ajili ya watanzania awe na shuruti ya kukila kwanza yeye na katiba iseme hivyo kuwa ukiomba kuwa mbuge watoto wako na mkeo watasoma na kutibiwa Tanzania ili kwa kufanya hivyo walazimike kuisimamia serikali ipasavyo

  Nini CDM wafanye sasa mpaka 2014, kwanza waainishe vipaumbele vyao halafu wawatafute dreamers and pactitioners waandae concept papaers halafu waitishe kongamano la kitaifa kujadili "hatima ya nchi yetu na uongozi mpya" waalikeni mabingwa wa ndoto (dream team) ili wafanye uchokozi uchokozi katika maeneo ya umaskini na ajira, uongozi, elimu, afya, maji, miundo mbinu na uchumi, wanawake na makundi maalum katika maendeleon.k. Wafanye hivyo wakilenga kipindi cha miaka kumi ijayo ili kutokana na kongamano hilo tukazalishe dira ya Chama kwa maendeleo ya nchi na hii ndio ikazalishe ilani ya chama kwa elfu 2015 kama hatua ya awali ya kujitofautisha na watu wengine.


  Nahisi kuwachukia CDM si kwa sababu hawafanyi vizuri bali wanabweteka sana kwani vitendo vyao haviendi sambamba na kazi nzuri ya uhamasishaji wanayofanya sasa, wananchi wakawaida wanataka kuwaona mkiwa active as you do now, and the brainy human wants to see you in paper works and link that to your field actions

  Iknow this may not be everybody's cup of tea but learn to hear much on your weaknesses rather than the praise.

  VIVA CDM

  ALUTA CONTNUA AND REMAIN ASSURED THE GENUINE FREEDOM OF OUR COUNTRY IS SOON IN OUR REACH, WE NEED YOUR LEADEARSHIP

  Wengi tunamawazo ya kuona Nyerere mpya anazaliwa Tanzania ili asahihishe mabaya ya awamu zote lakini ajenge nchi yetu upya
   
 2. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nini CDM wafanye sasa mpaka 2014, kwanza waainishe vipaumbele vyao halafu wawatafute dreamers and pactitioners waandae concept papaers halafu waitishe kongamano la kitaifa kujadili "hatima ya nchi yetu na uongozi mpya" waalikeni mabingwa wa ndoto (dream team) ili wafanye uchokozi uchokozi katika maeneo ya umaskini na ajira, uongozi, elimu, afya, maji, miundo mbinu na uchumi, wanawake na makundi maalum katika maendeleon.k. Wafanye hivyo wakilenga kipindi cha miaka kumi ijayo ili kutokana na kongamano hilo tukazalishe dira ya Chama kwa maendeleo ya nchi na hii ndio ikazalishe ilani ya chama kwa elfu 2015 kama hatua ya awali ya kujitofautisha na watu wengine

  Nimesikitika sana wanajamii mnaoitakia CDM mema mumejikita kwenye hoja za udaku na kuacha kuchambua hoja hii ambayo inatuhimiza kufanya zaidi kwa matokeo zaidi na kukidhi kiu ya mabadiliko ya Watanzania
   
 3. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Binafsi huwa napenda ushauri chanya kama huu. Ninaamini viongozi wetu makini na sikivu wataufanyia kazi. Tuko pamoja kamanda.
   
 4. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ondoa shaka kamanda kama umeamin cdm ni chaguo la wanyonge unaweza ukaanza wewe kwenye kata yako!
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  elimu ya wapiga kura wengi kwa bahati mbaya ni ndogo sana ukilinganisha na theory unazozimwaga jamvini, chadema inachohitaji ni kuungwa mkono kwa kura kutoka kwa mpiga kura yeyote na kokote alipo, kama kura za vijijini zimeiwezesha nchi kuwa mikononi mwa ccm kwa kipindi kirefu namna hii, itakuwa ni kosa la milenia kusubiri hawa wanakiji wakawa na uelewa/elimu unayoikusudia ndipo waweze kutambua unayotaka chadema wayafanye, ndipo wawaamini na kuwaunga mkono.

  Kwa mazingira ya mbinyo wa kiuchumi, kielimu na kidemokrasia tuliyonayo, naamini wanachofanya chadema ni chanya kabisa. kwanza kabisa chadema wanawajengea uwezo wa kifikra wananchi wa kukataa kudanganywa, kukataa kupuuzwa, kukataa kudharauliwa na pia kukataa kunyanyaswa. kwa kuwa uwezo huu haulengi kuikataa ccm pekee bali mtawala yeyote including chadema ikiboronga baada ya kukabidhiwa nchi, hii inanipa tumaini kubwa sana.

  better must come, and chadema is the wagon to bring, at least for now.
   
Loading...