Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,567
- Thread starter
- #21
Mkuu zimmerman, kwanza nakushukuru sana kwa sababu mpaka sasa, hii thread imeshamkomboa kifkra mtu angalau mmoja ambaye ni wewe!. Kitendo tuu cha kukubali kuwa "Dhana kwamba adui mkubwa wa watanzania si CCM bali ni sisi wenyewe siyo sahihi sana" hii kauli peke yake imenifariji kuwa dhana hii siyo sahihi sana inamaanisha ni sahihi kidogo!, kwangu uelewa kidogo tuu unatosha kuleta ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania.Pasco, unajua mada zako unazipanga vizuri, unaziandika vizuri na unazifafanua vizuri kwa lugha rahisi kiasi kwamba hata kama kimantiki si kweli watu wengi wanaweza kukubaliana na hoja zako? Ndivyo ilivyo hata kwa hoja yako hii ya leo.
Kiukweli kulekea elfu mbili na kumi na tano adui mkubwa wa Chadema ni ..CCM.
Dhana kwamba adui mkubwa wa watanzania si CCM bali ni sisi wenyewe siyo sahihi sana. Ni kweli kwamba kuna vi element fulani vya utamaduni wa kitanzania vinavyotubakisha sana nyuma lakini adui mkubwa ni yule anayecapitalize kwenye udhaifu wetu ili kuendelea kutunyonya na kutukandamiza. CCM haina huruma, haina tofauti na mkoloni wa kiarabu au kijerumani aliyetumia ukarimu wetu, upole wetu na kukosa elimu kwetu ili kujinufaisha juu ya migongo yetu. Ni kweli, hata hivyo, kwamba njia ya kumshinda adui wa namna hii ni kusambaza elimu ya uraia. Hii inatusaidia sana kuongeza ukali kidogo tunapodai haki zetu za kikatiba na kumpinga hasa pale anapoleta uhuni na ndicho Chadema wanachofanya.
Wewe mkuu Zimme, jifikirie kama wewe ni mlenga shabaha, umemaliza risasi zako zote ila umebakisha risasi moja tuu ya mwisho iliyosalia ndani ya bunduki yako na mbele yako unawaona adui wawili, mmoja ni lile lidubwana kubwa linalotisha linaloitwa CCM ambalo limebebwa na adiu wa pili anayeitwa watu!. Jee utaitumia hiyo risasi yako kulitarget hili dubwana CCM ulilenge, ulishoot au life, au lijeruhiwe na kuanguka chini na kuanza kugalagala au ndipo life, au lisalimike!.
Adui wa pili ni wale watu waliolibeba lile dubwana CCM, ambapo ukimlenga tuu mmoja, wate wataliachia hilo dubwana CCM liporomoke, na bila hao watu, lidubwana CCM, haliwezi kusimama lenyewe!, jee wewe utamtarget adui yupi kati ya hao?!.
Opposition siku zote wanalitarget hilo dubwana, as a result wanalijeruhi, lakini kwa vile wale wanaolibeba wako intact, no matter lijeruhiwe vipi, ikifika uchaguzi, hulibeba tena na kuliwezesha kuendelea kuwakalia hao waliolibeba hivyo kuendelea kupeta uchaguzi hadi uchaguzi!.
Lakini ukiitumia hiyo risasi yako moja ya ngama, kutarget ule mhimili hilo dubwana liliposhikilia na kusimamia, hutaligusa hilo dubwana, bali utaisambaratisha nguzo yake dubwana linaloitegemea, hivyo kupelekea nguzo kukatika na dubwana kuporomoka, na bila hiyo nguzo, dubwana haliwezi kusimama peke yake, litaishia kujifia natural death!.
Kwani CCM ni nini?, inategemea nini ili kuendelea kuwa madarakani?, hutumia mbvinu gani ili kuendelea kuchaguliwa, na jee wanaichagua hiyo CCM ni kina nani?, nikimaanisha determinant factor ya CCM kuchaguliwa ni nani kama sio watu?!.
Nachukua baadhi ya mistari yako "aliyetumia ukarimu wetu, upole wetu na kukosa elimu kwetu ili kujinufaisha juu ya migongo yetu. Ni kweli, hata hivyo, kwamba njia ya kumshinda adui wa namna hii ni kusambaza elimu ya uraia. Hii inatusaidia sana kuongeza ukali kidogo tunapodai haki zetu" mwisho wa kunukuu. Hayo maneno niliyobold, wetu, wetu, kwetu, yetu ​na zetu, ni kinanani!?, jibu hao ni sisi, ni sisi ndio tunaiweka CCM madarakani kwa kura zetu!. Kama tutaendelea kuitarget CCM badala ya kuwa target watu, we will be doing the same mistake again and again, na CCM itaendelea kupeta kwa ku capitalize on people!.
Kinachoipa CCM ushindi ni kipi?, lets deal na kinachoipa CCM ushindi na sio ku deal na CCM!.
Pasco.