Kuelekea 16/6/2016 " siku ya kuzima simu feki"

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,463
SHAIRI LA KUWAAGA BAADHI YA WADAU WA JAMII FORAM

Twahuzunika kwakweli,
Makamanda wa ukweli,
Kwa kuwaaga kwaheli,
Nunua nyingine rudi.

Hiyo ni kama ajali,
Simu yako si halali,
Kuwa nayo si kibali,
Nunua nyingine rudi.

Inaumiza ni kweli, gharama kuikabili,
Simu yako kubadili,
Nunua nyingine rudi.

Hii ndyo serikali,
Meamua kukatili,
Simu ziso na kibali,
Nunua nyingine rudi.

Twakuhitaji kwakweli,
Kwenye kundi letu hili,
Twaliona pengo hili,
Nunua nyingine rudi.

Ndg wala usijali,
Simu yako kubadili,
Mana si la kujadili,
Nunua nyingine rudi.

Huwezi kupinga hili,
Ni lazima ukubali,
Mana meshika makali,
Nunua nyingine rudi.

Mpendwa kila lakheri,
Kwa ya dukani safari,
Simu feki ni hatari,
UNAWEZA KUZIMIA...
 
Back
Top Bottom