Kudos to Hon. Pinda kwa kuanza kuwekeza Nchini: Wawekezaji si Lazima watoke Nje

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Wakuu

Its has been so long toka nianzishe thread hapa ila nafurahi kuona JF ikizidi kukua na kupata wanachama wengi...Hongereni sana

Kilichonikuna leo ni auli ya Hon. Pinda kuwa na yeye ni mwekezaji na kutoa kauli kuwa wawekezaji siyo lazima watoke nje. Zaidi ya yote kaongea kauli hii bila kumumunya maneno.tunaweza kujifunza kutokana na uwekezaji wa Hon. Pinda.

WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amesema suala la uwekezaji hapa nchini haliwalengi watu wa nje tu bali hata wa ndani wanaweza kuwekeza hata kama ni kwa kiwango kidogo.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumatatu, Novemba 29, 2011) wakati akizungumza na wakazi wa mikoa ya Rukwa, Ruvuma na mkoa tarajiwa wa Katavi katika chakula cha jioni ambacho aliwaandalia kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Wakazi hao zaidi ya 100 walikuwa wamealikwa kuja jijini Dar es Salaam kushiriki tamasha la Utamaduni la mikoa ya Rukwa na mkoa tarajiwa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tamasha hilo lilifanyika Novemba 25-27, 2011, katika kijiji cha Makumbusho jiini Dar es Salaam.

Akifafanua kuhusu uwekezaji Waziri Mkuu alisema yeye alipochukua mkopo waliopatiwa wabunge wa sh. milioni 90, hakuona haja ya kununua gari bali aliamua kuwekeza katika ujenzi wa nyumba ya kulala wageni kijijini kwao, Kibaoni wilayani Mpanda.

"Nilichukua mkopo mwingine benki ya NMB na kuamua kujenga vyumba 24 pale kijijini kwetu. Kama ningetaka ningechukua mafundi wazuri kutoka Kariakoo, (Dar es Salaam) lakini niliamua kutumia mafundi wa kijijini ili kutokana na zile fedha nao pia waweze kununua bati na kuezeka katika nyumba zao, jambo ambalo limewezekana," alisema.

"Ujenzi wa vyumba 24 karibu unakamilika, … kiasi kingine cha fedha nililima shamba la mahindi na nikafanikiwa kuvuna magunia 380," aliongeza.

Waziri Mkuu anasema aliamua kuuza magunia 300 kati ya hayo aliyovuna na kupata sh. milioni 11 ambazo aliziwekeza tena katika mradi wa ufugaji nyuki kijijini kwao na Dodoma.

"Nina mizinga 250 kule Dodoma na Kibaoni (kijijini kwao) nina mizinga 600, kila mzinga unauzwa sh. 50,000/- na kila mmoja una uwezo wa kutoa lita 10 za asali. Bei ya asali hapa mjini ni sh. 10,000/- kwa hiyo katika kila mzinga unaweza kupata sh. 100,000/-," alisema.

Alisema suala la uwekezaji ni muhimu na haliepukiki na kumtaja Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi ambaye alikuwepo katika hafla hiyo kwamba ni miongoni mwa wawekezaji wadogo kwani ana ekari 200 za mahindi na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Kanali Antonio Mzurikwao kuwa naye ana ekari 100 za mahindi. "Hawa nao ni wawekezaji lakini tunawaita wawekezaji wadogo," alisema.

Akifafanua kuhusu uwekezaji, Waziri Mkuu alisema nchi zote zilizoendelea zilifaulu kufiki hatua hiyo kwa kupunguza idadi ya wakulima wadogo na kuongeza idadi wa wakulima wakubwa. "Mkiona wakulima wadogo ni wengi mjue kuwa bado hamjapunguza umaskini," aliongeza.

Alisema Taifa bado linakabiliwa na changamoto ya kupunguza umaskini kwa kuhahakikisha kwamba kuna uzalishaji wa chakula cha kutosha ili watu kwanza washibe lakini pia akaongeza kusema kwamba inabidi uzalishaji uwe na tija ili wakulima wapate mazao mengi na kujiongezea kipato.

Akitoa shukrani katika hafla hiyo, Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi aliwashukuru wajumbe wa Kamati za maandalizi katika mikoa ya Dar es Salaam na Rukwa kwa maandalizi mazuri hadi wakafanikisha tamasha la utamaduni wa mikoa hiyo miwili.

Mkuu Pinda,naomba kutoa ushauri mdogo tu, Serikali ianze pia kutengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani ambao ni watanzania kwa kutoa masharti nafuu yanayofanana na yale ambayo tunayowapa wawekezaji wa nje. Kama tukiwapa hawa wa ndani, tena Watanzania wanawezakukuza biashara zao. Nina imani kabisa kama tukiwasaidia kuanzisha biashara ndogondogo tatizo la ajira kwa vijana haliwezi kuwa bomu


With all respect, Mkuu PM Pinda Nakupongeza na uendelee na uwekezaji sehemu zingine za Tanzania!
 
Safi sana mkuu, ila yeye ndie ana role ya kupromote mazingira sawa na mazuri ya kuwekeza.

Tatizo langu kwa Mh Pinda ni kuwa naye analia lia kama sisi tusio na vyeo serikalini, wakati yeye ni mtendaji.
 
Mkuu karibu tena!

Ndoto yangu mimi kama mwananchi ni kuona watanzania wengi tunamiliki njia kuu za uchumi. Kama wanasiasa wanaonyesha kwa vitendo, bila kutumia hela za kuiba then that is a positive move.

Tuhamasishe wengine wengi tuwe wajasiriamali na kuacha kutegemea kuajiriwa na watu wengine bila sababu.
 
Safi sana mkuu, ila yeye ndie ana role ya kupromote mazingira sawa na mazuri ya kuwekeza.
Tatizo langu kwa Mh Pinda ni kuwa naye analia lia kama sisi tusio na vyeo serikalini, wakati yeye ni mtendaji.


Mkuu Fair Player,Tatizo la Pinda siyo kulia lia,what i see ni yeye kama PM hana madaraka makubwa hivyo zaidi ya kushauri tu,?Tatizo hata hao mawaziri ambao wamemzunguka hatujawahi kuona wakizungumzia ni jinsi gani wanawasupport vijana na wajasiliamali wa ndani zaidi ya kuwaandalia semina..

Semina sawa,ila serikali inatakiwa iende mbali zaidi na kuwawezesha hawa wawekezaji.Je wizara ya vijana imewasidiaje vijana katika kutengeneza ajira?wana mpango gani kwa miaka 10,15 20 ijayo?tatizo mawaziri waliopo nao wananchangia katika kuchelewesha maendeleo.Mie nina uhakika kabisa ,sisi kama taifa tukijipanga na kuweka taifa mbele na kushirikiana bila kujali itikadi za vyama vyetu tatizo la Ajira litapungua sana.

kuwa na waziri ambaye yeye kama yeye hana vision ni tatizo.Kama Mdogo wangu Nchimbi ananisikia basi aanze sasa kuandaa sera ya kutengeneza ajira na kusimamia biashara za vijana.Hapa tuanweza kutrack ni biashara zipi zimeweza kutengeneza ajira,wanaendeleaje na wanahitaji vitu gani ili waongeze uzalishaji wao.Hili ni suala la kitaalam na hatuhitaji bodi yenye watu wa zee ili kupanga mikakati hii

Mkuu Nahani,Pinda kawa muwazi kuwa anafanya biashara na kaelezea vyanzo vyake vya biashara ambavyo hauwezi kuvidoubt..siyo wale mawaziri wanaomiliki vitega uchumi ila havijulikani vimepatikana wapi..!


Pinda amenigusa sana kwenye swala la asali na tuendelee kukata issue..
 
Miaka 50 ya uhuru ndio leo anazungumza hili? Kweli ujinga ni laana...

Inaonyesha hajawahi kuwekeza kabla ya kuwa PM pengine ni kwa sababu hakuwa na mtaji, sasa ana access ya fedha mfano kukopa NMB na mkopo kuokana na ubunge; ana mkakati gani kwa mtu wa kawaida kupata mtaji kama yeye?
 
huyo ndo pinda! Mzee wa mortgage, mzee wa nyuki, mzee wa nafaka. Shit kabisa. Waziri mzima unavuna magunia 300? Unafuga nyuki? Angesema hobi tungemwelewa
 
Siasa na biashara!!! Hii ndiyo Bongo. Je wewe ungeweza kupata mkopo kama huo ungeshindwa kufanya kama yeye? Suala hapa si kusifia kwa sababu kwa cheo chake fursa hizo kwake zipo tele. Je asingekuwa ktk nafasi hiyo angeweza kuupata huo mkopo? Je ni lazima sote tuwe wabunge au Mawaziri Wakuu ili tuwe wawekezaji? Haiwezekani. Je ni mkulima gani mdogo wa Tz anayeweza kumilikishwa ekari 50 au 100 au 200? na hata akifanikiwa kuzipata atazilimaje?Mkuu, samahani sioni cha kupongeza hapo.
 
..amepata MKOPO wa sh mil 90 wa masharti nafuu kupitia BUNGE.

..juu ya hiyo mikopo kuna posho zisizokuwa na uhalali wala maelezo, mishahara minono, marupurupu etc etc.

..ndiyo maana wataalamu wanaacha kazi zao na kukimbilia kugombea ubunge.
 
Back
Top Bottom