Kudorora mapokezi ya Rais Samia kutoka Marekani Tatizo limeanzia hapa...

Sote ni mashahidi tangu juzi kuna kakikundi ambako sidhani kama ni watanzania kweli au wachumia tumbo tu wanaolipwa kushibisha nafsi zao au la!

Tangu juzi tumeshuhudua kukurukakara za hapa na pale za kutaka kuaminisha watanzania wachache kuwa Rais Samia Suluhu alitoa hotuba ya kihistoria. Ile ni hotuba ya kawaida sana.

Kwanza niwajulishe tu walioona na kusoma hotuba ya Rais ni watanzania wachache tena wanasiasa ambao wana access ya Mitandao ya kijamii. Huko vijijini na mikoani wala hawama habari na kinachoendelea. Wengi ktk mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi hiki ni kipindi cha kuandaa mashamba ya kilimo ktk msimu wa mvua ujao.

Hata hivyo kumekuwa na jitihada za kutaka kulikuza jambo hili kwa kile kilichoandaliwa kama mapokezi ya Rais kutoka Marekani.

Mbali na vijitangazo vidogo vidogo sijaona tukio lolote mahali popote likishangiliwa na watanzania. Sijaona Tv wala mtandao wa social media hata ule wa vijigazeti la chama.

Watanzania wamesusa. Wamesusa kwa sababu hawafurahishwi na kinachoendelea nchini

Matukio ya kubambikiza watu kesi za ugaidi yamewachukiza sana watanzania wapenda amani, haki na maendeleo. Watanzania wamekatishwa tamaa na namna nchi inavyoendeshwa kupitia Tozo na kodi lufufu.

Watanzania hawawezi kufurahia tukio la Mtu na kikundi cha watu wachache kwenda marekani huku wakiacha uvunjifu mkubwa wa haki za kikatiba kama uhuru wa vyombo vya habari, haki za kukusanyika na kufanya shughuli za kisiasa na uchumi.

Nimuombe Mama Rais Samia Suluhu hajachelewa. Arekebishe mienendo yake ya utawala. Ajikite kulinda haki za wananchi makundi yote wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, watumishi wa umma na wanasiasa.

Akifanya hivyo hatahitaji nguvu kubwa kusherehesha watanzania. Wakiwa na Furaha watampokea mgeni bila kutumwa.

Si Whatsapp, twitter, facebook, youtube wala instagram huoni shamra shamra. Wikendi imepoa sana kama hakuna kitu.
Kwanza lugha aliyotumia ya Malkia kuhutumia huko UNGA, haikulenga Watanzania. Na Je Kwa nini hakutumia Kiswahili wakati kuna Nchi zimetoa hotuba kwa lugha zao? Pili, ukiisoma ile hotuba imejaa taarifa nyingi za WHO na hasa kuhusu Covid 19...

Watu leo wanaenda zao kwa Mkapa ingalau wakafurahi....sio kwenda kumpokea mtu Airport..
 
Tuliambiwa alikuwa na ujumbe mzito wa wawekezaji wa ndani kukutana na wawekezaji wa nje - kima Mange.

Kuchanganya madesa ni kipaji.

Wa Burundi alikwenda na mke na watoto wake wote.

Mkutano huu ni wa kuuza sera za nje na kuweka wazi misimamo ya nchi wala si vinginevyo.
Ndio unaitwa UNGA
 
Mkuu sahau ya nyuma! Twende na Mama yetu kwani tunakoelekea ni mbali kuliko tulikotoka.
Tushikamane na Mama yetu,tumpe support tutafika tu.
Hata hivyo Asante kwa mawazo Yako!
"Mawazo hayapingwi rungu" ushauri wako utafanyiwa kazi.
 
Kudorola mapokezi! Inamaana wanaotakiwa kumpokea hawakuenda?
Au unamaanisha kuwepo na sherehe ya kumpokea?
Ninavyojua kuna utaratibu wa kumpokea rais na wahusika wapo lakini hakuna sherehe inayotakiwa kufanywa kama vile Simba wanavyotokaga kuwapiga mabao ya kutosha waarabu huko Misri.

Cha muhimu arudi salama aendelee kuchapa kazi zake. Walakini hakika bado anaupiga mwingi.

Hongera SSH na kazi inaendelea
 
Apokelewe kwani ni Mgeni au hajui anapoenda?. Wazee wetu walimchangia Nyerere alipoenda kuhutubia huko mambele na Dunia ikatisika SASA huyu kubwa aliyofanya ni kupiga picha na Mange.
Hahhaa Diaspora tunayohubiliwa kila siku ndio ile ya Mange kweli??
 
Mkuu sahau ya nyuma! Twende na Mama yetu kwani tunakoelekea ni mbali kuliko tulikotoka.
Tushikamane na Mama yetu,tumpe support tutafika tu.
Hata hivyo Asante kwa mawazo Yako!
"Mawazo hayapingwi rungu" ushauri wako utafanyiwa kazi.
Asante kwa kuupokea. Watu wema wataukubali na kuufanyia kazi.
 
Kudorola mapokezi! Inamaana wanaotakiwa kumpokea hawakuenda?
Au unamaanisha kuwepo na sherehe ya kumpokea?
Ninavyojua kuna utaratibu wa kumpokea rais na wahusika wapo lakini hakuna sherehe inayotakiwa kufanywa kama vile Simba wanavyotokaga kuwapiga mabao ya kutosha waarabu huko Misri.

Cha muhimu arudi salama aendelee kuchapa kazi zake. Walakini hakika bado anaupiga mwingi.

Hongera SSH na kazi inaendelea
Shamra shamra maana Rais sio wa kikundi maalum. Ni wa wananchi wote.
 
Kwanza lugha aliyotumia ya Malkia kuhutumia huko UNGA, haikulenga Watanzania. Na Je Kwa nini hakutumia Kiswahili wakati kuna Nchi zimetoa hotuba kwa lugha zao? Pili, ukiisoma ile hotuba imejaa taarifa nyingi za WHO na hasa kuhusu Covid 19...

Watu leo wanaenda zao kwa Mkapa ingalau wakafurahi....sio kwenda kumpokea mtu Airport..
Alijikita zaidi kwenye Corona kutafutia kiki😅
 
hahahaha yeye ndio chief boss kwahio haina mjadala

Heri angeenda kuuza nyungu au bupeji au hata NIMRICAF.

Value ipi kaongeza kwenye mkutano ule?

Ajabu eti anaongelea dilemma ya kulinda maisha dhidi ya uchumi.

Kuna dilemma hapo? Awaulize wanaume wa shoka kina Museveni na kina PaKa kama kuna dilemma hapo.

Tumekuwa kituko!
 
Tuliambiwa alikuwa na ujumbe mzito wa wawekezaji wa ndani kukutana na wawekezaji wa nje - kina Mange.

Kuchanganya madesa ni kipaji.

Wa Burundi alikwenda na mke na watoto wake wote.

Mkutano huu ni wa kuuza sera za nje na kuweka wazi misimamo ya nchi wala si vinginevyo.
wa Burundi ametish🤣🤣
 
Eti 'Watanzania wamejasirishwa kukamatwa kwa mbowe!'. Mdugu, HV unaishi Tanzania au?!!! Maana tz hii kwa sasa hakuna kabisa anayemzungumzia mbowe zaidi ya mbowe mwenyewe na misukule yake. Ukisikia sana basi ni habari ya kesi yake kupitia baadhi ya vyombo via habari
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom