Kudondoka kwa uchumi wa Tanzania: Tatizo si la wanasiasa bali ni Wananchi wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kudondoka kwa uchumi wa Tanzania: Tatizo si la wanasiasa bali ni Wananchi wenyewe

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Godwine, Jan 22, 2012.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Miaka ya nyuma uchumi wa nchi ulikuwa ukitawaliwa na taifa kupitia udhibiti wa njia za uchumi chini ya umma, lakini kwasasa wakati nyakati hizo zimepita na serikali imebaki ni watunga sera na kusimamia utekelezaji na kuwa refa wa mechi ya uchumi.

  Tatizo kubwa la Tanzania ni nchi kugeuka soko la mataifa mengine ili linasababishwa na Wananchi kutowekeza kwenye viwanda na kukimbilia kwenye matumizi mengine . pia ata wanapotaka kuwekeza kwenye biashara basi wanakimbilia biashara za uchuuzi na majengo badala ya viwanda ambavyo vingesababisha kukua vema kwa uchumi na kupunguza uagizaji wa bidhaa toka nje ambao unadidimiza uimara wa fedha yetu na uchumi wetu.


   
 2. k

  king11 JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiona serikali inakopa kwenye bank za kibiashara ujue wananchi wametunza fedha nyingi badala ya kuziwekeza kwenye biashara. pia wawekezaji wa tanzania wanaona ni vema kuweka bil 10 kwenye ujenzi wa jengo na kuacha kuwekeza kwenye kiwanda au karakana ambayo ingechangia kukua kwa uchumi zaidi ya jengo
   
 3. d

  dada jane JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni somo zuri ninaomba shule zaidi ili niielimishe jamii inayonizunguka. Maana mwananchi wa kawaida itasaidia. Kwani wengi wa pesa nyingi zinakaa tu bank.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wanaoweka vipaumbele ni wananchi ama wanasiasa? Sera na ilani huandaliwa na nani? Itikadi ya nchi huamuliwa na nani? Sera za viwanda, kilimo ama uwekezaji zinasemaje? Hapa huwezi mlaumu mwananchi ikiwa wanasiasa (serikali) katika sera yake ya manunuzi wanapendelea kuagiza nje. Vipaumbele huwekwa na serikali kisha ikatoa muelekezo wa jinsi ya kufikia malengo. Wanasiasa wana nafasi kubwa sana katika kuhakikisha wananchi wanaenda katika mistari sahihi ya kimaendeleo
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Godwin umekosea sana na leo bahati nzuri nitakuelimisha vizuri!. Tatizo la Tanzania ni serikali.

  Tanzania ingekua imeendelea sana kama serikali ingekuwa inatunga sheria tu hapa chini nitakupa kitu kimoja kimoja kwa undani

  1. Viwanja: Nimeanza na viwanja kwasababu kwa uchumi kuendea unakiwa kuwa na "Land". Kwanza viwanja vya Tanzania si vya wananchi bali ni vya serikali! hivyo wananchi wa Tanzania wana pangisha viwanja vyao. Tatizo ni kwamba serikali si mtu hivyo kiongozi yeyote anaweza kuweka sheria zake na kubadilisha kwa manufaa yake binafsi wakati wowote. Pili vibadi vya viwanja vya Tanzania hata kama unahaki zote za kumiliki ni gharama na usumbufu wa hali ya juu kipewa kibali cha kiwanja kama unataka kujenga. Kuna wakati inachukua hadi miaka minne kupata kibadi nwakati una kila karatasi linalotakiwa. Ujenzi mfano ni muhimu sana kwa maendeleo kwani ukijenga unatumia mafuta, una nunua smenti, misumari, mbao, plastics, mabomba, wiya, unavuta umeme, makokoto, unaajiri wapimaji wa viwanja, unaajiri wajenzi, na mengineyo mengi. Hii yote inasadia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi lakini serikali inazungusha watanzania kucha kutwa kwenye vibali bila kuwa na sababu ya msingi. Pamoja na serikali kuzungusha watu Watanzania wamejitahidi kujenga bila msaada wowote wa serikali.
  2. Umeme: Umeme ni mfano mwingine wa serikali kuwa na Tatizo. Serikali ingeachia kampuni binafsi zihusike kwenye umeme tatizo la umeme lisingekuwapo Tanzania. Ngoja ni kupe mfano wa state nyingine za hapa USA zinavyofanya. Step 1: Kunakuwa na kampuni kama ya Tanesco na inakuwa na lengo moja tu kusambaza umeme na kutengeneza. Step 2: Kampuni ya Tanesco inakuwa inanunua umeme kwa makubaliano fulani na kampuni ya tofauti zingine za majenereta, zingine za umeme wa jua, zingine za umeme wa upepo, gas n.k. mtu yeyote anayeweza kuuzia umeme Tanesco kwa kiwango fulani ambacho ni cha kimataifa aruhusiwe. Step 3: Tanesco inajitoa kwenye biashara ya wateja kama kutuma bill na kukusanya pesa na ziruhusiwe kampuni tofauti kufanya biashara hizo. Hii itapunguza mzigo mkubwa kwa Tanesco. Mfano mtu akiwa na bill naomba nitumie dollars ya $50 kwa mwezi basi ($20 ya Tanesco, $20 ya muuzaji wa umeme na $10 ya kampuni inayoshughulikia utumaji na upokeaji wa mapato kutoka kwa wateja). Ushindani huu utapunguza gharama na kuongeza umeme Tanzania. Tanzania inakuwa imetatua tatizo lililopo sasa la kununua majenereta!. Hili ni tatizo la serikali, mikataba mibaya ni tatizo la serikali. Umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.
  Mikopo: Je kwa nini Tanzania mikopo ya bank ni zaidi ya 10%? ni kwasababu ya vitu vifuatavyo (1) Hatuna ID hivyo watu wa bank hawajui watu (2) Viwanja ni vya serikali hivyo huwezi kuweka rehani kwa muda mrefu kwani serikali wakati wowote inaweza kuchukua kiwanja cha mtu yeyote (3) Serikali-Serikali ili kukithi mahitaji inauza T-BILLS na Goverment Bonds. Serikali ya Tanzania rate inayotoa kwa hizi ni zaidi ya 7% na kawaida bank haziwezi kutoa mikopo kwa rate chini ya hapo kwani kama mwekezaji anaweza kuwekeza kwa serikali kwa 7% na ana uhakika wa kulipwa ni kwa nini anawekeze kwa mtu wa kawaida kwa kiwango hicho hicho wakati hana uhakika wa kulipwa!!! hivyo ukweli ni kwamba bank ni lazima zitoe kiwango cha juu zaidi. Hapa tena Tatizo ni serikali!
  Miradi ya Uwekezaji: Uwekezaji wa Tanzania ni kichekesho serikali ikipata mwekezaji wa madini, mafuta, gas au hata mashamba wanawatoa watu kwenye maeneo ili kumpisha mwekezaji. Serikali bila kuhusisha wananchi inaingia mikataba ya siri eti kwa manufaa ya nchi. Wawekezaji wanawalipa wafanyakazi au wizara Dar. Watanzania ambao wamefukuzwa na kuchukuliwa viwanja hawapati chochote, jamii zao zinadidimia sana barabara hazijengwi, hakuna shule, hakuna maji n.k sana hapo serikali imewasadia vipi wananchi? Je si bora serikali ingewasaidia wananchi kuingia mkataba na hizo pesa zibaki pale.Sasa hapa tena serikali ni Tatizo ingetakiwa kuwasaidia watu badala ya kufanya mashamba ya watu kuwa mitaji ya mawaziri.
  Kuna mifano mingi na sitanii nafikiria kuandika kitabu kwani nimeona watu wengi hawaelewi ubaya wa kuwa na serikali kubwa.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kushuka kwa uchumi wa nchi hii ni kutokana na serikali kukosa uongozi wa utawala bora. Inawezekana kabisa kwamba wananchi walikuwa na nia ya kuwekeza kwenye viwanda, lakini kwa makusudi na kwa hila wakanyimwa na viongozi wetu kwa maslahi binafsi. Haiingii akilini kuona karibu viwanda vyote vinamilikiwa na watu wanaotokea bara la asia. Hatuna viongozi wenye dhamira ya kweli kuwaandaa wananchi kuwekeza kwenye sekta ya viwanda. Ni jambo la kushangaza kuona ngozi inasafirishwa nje ya nchi, badala ya kutengeneza kiwanda cha ngozi hapa hapa nchini. Ni jambo la kushangaza dhahabu yetu inasafirishwa kwenda nje badala ya kufanyiwa sorting hapa hapa nchini na kuiuza kama bidhaa badala ya mali ghafi. Bila kuwa na viongozi wenye fikra chanya na wenye uthubutu tutabaki kulalama tu.
   
 7. d

  dada jane JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante wakuu leo nimepata jibu kwa nini nchi ni maskini.
   
 8. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,452
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  Andikeni kwa mcharazo wasiwaelewe ...maana wanadai uchumi umekua haujashuka sasa nyie mnaosema umeshuka.........!!!
   
 9. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tatizo la uchumi wa Tanzania linaanza na kuwa na Rais aliyesomea uchumi lakini hajui kuapply alichosomea. Rais ambaye hajui kwanini Tanzania ni maskini.
   
 10. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,452
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  sidhani kama kwa sera za sasa ukitaka kuwekeza kwenye kiwanda zinakukataza kwani kwa kutumia mfano hai wa mfanyabiashara (BAKHRESSA) ameweza kuwekeza katika viwanda na amefanikiwa kwa sera hizi hizi sasa wakati mwingine visingizio vya watu vinakuwa kwa viongozi wa kisiasa badala ya wao kujaribu. kuna watu wametunza mabilioni ya fedha bank badala ya kuwekeza , tatizo kubwa ni la wananchi wenye uwezo wa kuwekeza hawafanyi hivyo
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo lazima tuweke sawa uchumi na uongozi, natambua wazi wazi kuwa serikali ya sasa imeshindwa kufanya yanayostahili na hii ni kutokana na kubomoka kwa chama tawala na makundi. hii inaweza kupelekea kutoweza kuratibu sera vyema , lakini hiki kisiwe kisingizio kikubwa cha kushindwa kuwekeza katika viwanda na kutawala uchumi wetu na kuleta maendeleo. kwa mfano somalia mbali na kuwa na machafuko lakini bado uchumi wao unakuwa na wako juu yetu.Sasa kama kisingizio cha sera pekee unaweza kusema Somalia wana sera gani kutushinda sisi?.

  Tatizo kubwa ninaloliona mimi ni la wananchi hasa wafanyabiashara kushindwa kuwekeza kwenye viwanda na wakati mwingine kuachia wageni kutawala uchumi wetu. Inawezekana mtanzania akawa na shs mil 300 akakimbilia kununua V8 na kushindwa kujua mtaji huu unaweza kuanzisha karakana ndogo, baadae wakija wachina kuwekeza kwenye karakana analalamika kwamba hana mtaji wa kuwekeza kwenye karakana. Wapi wabunifu wa kuweza kukuza sekta ya viwanda pasipo kulalamika kila kitu? lazima tuige kwa watu kama SSB akizalisha bidhaa zinazopunguzia taifa kuagiza ata juisi Afrika kusini na kuokoa matumizi ya fedha za kigeni yasiyo na lazima
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  You have a gist dude!!!
   
 14. G

  Godwine JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sababu ya kutokupewa kiwanda kilichokuwa kinamilikiwa na serikali kwa wazawa ni nzuri lakini haiwezi kukunyima uwezo wa wewe kuagiza mitambo yako nje na kuanzisha kiwanda kipya. kwa mfano unaweza kukuta mtu anajenga ghorofa posta lenye thamani ya zaidi bil 20 kwani alinunua ghorofa kwanza na kulivunja na kisha kujenga analolipenda yeye, mtu huyu angeweza kujenga kiwanda cha kuchakata ngozi, na iwe inatumika nchini kwetu na si kuuzwa kabla ya kuongezwa thamani.

  Kabla ya kuanza kuilaumu serikali kwa sera mbovu lazima tuanze kufanya kitu fulani pale tunapokwama ndio tupige kelele na tatizo la sera mbovu. Bado kuna fulsa nyingi lakini watu awazitumii na wanawekeza kwenye sehemu isiyo na tija kubwa. watu wanatumia fedha nyingi kuwekeza kwenye anasa kuliko viwanda
   
 15. k

  king11 JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1. kuhusu viwanja mkuu nadhani Tanzania hatujafika wakati wa kusema tumekosa ardhi ya kuweza kuwekeza viwanda vyetu labda utake kuwekeza kariakoo au posta.

  2.Umeme ni moja ya sababu za kukwamisha viwanda lakini kwa nchi yetu imetoa ruhusa ya kampuni za binafsi kuweza kuwekeza kwenye sekta hii hivyo ni sehemu tunayodhani watu wanaweza kuwekeza.

  3.Mkopo wa bank lazima utakuwa na riba zaidi ya 10% kwasababu ya mfumuko wa bei kwani banki lazima zihakikishe kiwango utachokilipa kitaendana na thamani ya fedha zao kwa wakati huo sasa mfumuko wa bei umefika 19.8%
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  we unaona tatizo ni viwanda tu. Fungua akili na uwasome wenzako. Yaani wewe unaaply kitu kinaitwa ceteris peribus. Other things constant ukabaki na viwanda. Unaweza kuwa na viwanda na usiwe na economies of scale. Nimezungumzia kuhusu sera. GDP and consequently per capita income sio zao la exportation of industrial goods pekee. Kuna utalii, uwekezaji, kodi, remittance, n.k. Sasa ukishikilia viwanda pekee unajidanganya. You are talking about holding other variables in an economy which sounds more theoretical rather than empirical
   
 17. G

  Godwine JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Kodi ni matokeo ya uchumi lakini si kitu cha kukuza uchumi, kuna kitu lazima utambue utaongelea yote lakini ni nadharia kwa nchi kuendelea bila viwanda na tena viwanda . hisi porojo za wazungu kuandika vitabu jinsi ya kuendele bila viwanda ni namna ya kukugeuza wewe kuwa soko lao ndio maana wanaweza kukudanganya ili usifikirie viwanda. pia umeongelea uwekezaji sentensi uwekezaji bado aujakamilika kwani ukisema uwekezaji bila kusema unawekeza wapi utakuwa unajichanganya tuu.

  ok shukrani kwa mchango wako lakini taifa bila Viwanda maendeleo ni ndoto kwani kila mmoja atageuka mchuuzi wa bidhaa za kigeni na nchi itageuka soko lao tu tena la bidhaa za mtumba toka kwao
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa wananchi wengi sana tena wanasiasa ndio wanaongoza kwa ku-invest kwenye mambo ambayo hayakuzi uchumi

  a. Watu wangapi Tanzania wana nyumba ya Mil 300 mbezi lakini yeye anafanya kazi kwenye kampuni? by any standard mil.300 si pesa ndogo hadi kuweka kwenye nyumba ambayo ni residential haileti uchumi wowote badala ya kujenga kiwanda?? hesabu nyumba za kuishi watu ufukweni mwa dar ndio utajua priority za wananchi wetu; middle class citizen

  b. Kila tatizo ni opportunity katika uchumi wa soko huria; mathali ukosefu wa umeme ingekuwa ndio opportunity ya wanachi kuandika write na kufanya biashara ya umeme; kukopa benki kufanya hivyo; wananchi wetu wanasubiri wazungu na serikali inasubiri wazungu na pesa wanachukua hapa hapa kwenye benki zenu (savings zetu) ikiwemo ppf..

  c. Kilimo na ufagaji wa kibiashara unafanywa na watu ambao hawana eliu, wenye degree wanatafuta kazi viwandani na maofisini ; hii altitude inaharibu uchumi wa nchi, na hawa ni wananchi

  d. Kila mwenye pesa ame invest kwenye bar, saloon na duka; traditional businesses hakuna anayetaka kujaribu mambo mapya ku-solve problems; yote haya ni matatizo ya wananchi wetu..

  empawerment and capacity is needed
   
 19. G

  Godwine JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Na kama watu wengi wangewekeza kwenye viwanda pia tatizo la ajira katika taifa letu lingepungua kwani kiwanda kimoja kinatoa ajira nyingi kuliko kujenga ghaorofa la makazi au nyumba ya makazi
   
 20. RaiaMbishi

  RaiaMbishi JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 252
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mchambuzi alifafanua vizuri sana suala hili kwenye uzi wake wa: Mkullo, Ndullu na Uchumi Uchwara.
   
Loading...