Kudodosha bomu Octoba 31 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kudodosha bomu Octoba 31 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mathias, Oct 28, 2010.

 1. Mathias

  Mathias Senior Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu habari kwenu
  Napenda tu kuwashirikisha katika furaha yangu ya leo.
  Nilienda katika kituo changu cha kupigia kura kuangalia kama jina langu limerudi au la? Bahati nzuri namshukuru Mungu kuwa jina limerudi na ntakuwapo kati ya watu watakao piga kura hapo October 31. Kwa kweli ni furaha ya ajabu niliyo nayo kuona sasa nina rungu kamili la kuwakataa mafisadi na ufisadi wao. Nimeangalia kadi yangu ya mpiga kura mara mbili mbili nikaisi inafanana na bomu kali ambalo halina masihala pindi kipini kitakapochomolewa na kuachwa lilipuke. Naifafanisha pia na kombora la maangamizi ambapo hapo Octoba 31 ntalilipua mwenyewe, natumani kwa kuungana na watanzania wenzangu Nov 2 majibu ya milipuko yatajibu. Tutafurahia ushindi wetu na moshi wa milipuko utakuwa kila pahala, na mwisho wa siku Jemedari wetu atatangaza kuisha kwa vita. Nimejipanga panako majaliwa ya mwenyezi Mungu iyo Jumapili nifike katika kituo cha kupiga kura saa moja kamili asubuhi ili pasiwe na kisingizio cha kukosa iyo fulsa muhimu. Nimewaomba Ndugu na jamaa walikuwa na mipango ya kuja kunisalimia na shughuli nyingine za kijamii, waniwe radhi kwa siku iyo kwa sababu shughuli za kitaifa zitakuwa muhimu zaidi ya shughuli zangu binafsi. Wengi wanasema kura yako ni siri yako, lakini napenda kuwashirikisha ya kuwa mie ntampigia kura ya NDIO Dr Slaa na Mbunge wetu wa Kawe Halima Mdee, na Diwani wake (japo sikupata nafasi ya kumsikiliza diwani katika kampeni zake, lakini naamini ni mtu makini) nafanya hivi kwa sababu siridhishwi na kasi ya utendaji wa Serikali ya ccm, roho yangu inanatuma kwamba kama ntawapigia kura watu hawa ntakuwa sijatenda haki kwa mamilioni ya wananchi wanao ishi kwenye dimbwi la umasikini, na vile vile ntakuwa mnafiki wa dhamira yangu ya haki sawa kwa kila raia. Natambua kama Raia huru sifurahishwi na Serikali yetu na utendaji wake na njia pekee ya kuonyesha masikitiko yangu ni kupitia kisanduku cha kupigia kura ndo maana nasisima mstari wa mbele kutekeleza wajibu wangu ili siku ya siku niseme kwawanangu nakwa mungu wangu kuwa nilitekeleza wajibu wangu kwa uwezo na maarifa yangu.

  Ndugu zangu nimewaandikia kwa sababu nina faraja moyoni na nimependa kuwashikirikisha katika ili.
  Mungu ibariki Tanzania na wananchi wake, twende sote tukapige kura tulete mabadiliko tuyatakayo.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  mi sijaenda huko, nimecheki kwenye mtandao wa nec.go.tz kila kitu swadakta nipo tayari kuweka kura yangu kwa mara ya kwanza.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Elnino nenda kaprove physically unaweza kuta mwana si wako ukaambulia kushika kichwa
   
Loading...