Kudisco Chuo kuskieni tu, ni maumivu yasio na mfano

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Huku tukiwa na mapumziko ya siku chache ya sikukuu hii tukufu kabisa ya Iddi,basi ningependa leo niwakumbushie mawili matatu tu hawa wadogo zetu ambao bado wako ma vyuoni humu nchini, na ambao sasa hivi uenda wakawa wako kwenye kipindi cha mitihani yao ya kumaliza mwaka (UE), au ndo wako wanajiandaa, tunakumbushana tu.

Hakika hakuna kitu kibaya kama kuona ndoto yako inakatishwa mchana kweupe na watu wachache tu, vuta picha ni maumivu kiasi gani kupewa taarifa kua "bhana kuanzia siku hii wewe sio mwanachuo tena, ndoto zako mwisho leo, na mkopo ndio baibai hivyo, ume disco mzee rudi kwenu mwaka mzima bure mzee" sasa mbaya zaidi anayoambiwa haya ni kijana mdogo tu asie na ukomavu wa kimaisha tena walio wengi ndio hawa fresh from school wanaamini chuo ndio maisha yao ndio kila kitu kwao.

Sasa bila kusahau ku disco ni jambo dogo tu na uenda isiwe kaazi kiviile, maana kunatakiwa mtu ajichanganye kidogo tu na apate sare Supplimentary 4 tu kwa mwaka kwa baadhi ya vyuo, au Sup. 5 basi ambazo ni mitihan tu mwanafunzi anaweza kuamka vibaya akabaka maswali akaenda na maji ghafla discontinue hio hapo.

Sasa nyakati hizi ni vyema basi wadogo zetu mkawa bize na mambo ya kimasomo, pigeni discussion za maana, someni sana hata kama hamuelewi ivyo ivyo kazeni tu, salini sanaa na punguzeni mizaha zaha hio, ila kikubwa mjifunze kujituliza wenyewe kama kufanya meditation ya numbers ili mjifunze kutokupanic uko mbeleni, mengine mnayajua wenyewe yazingatieni haya.

sasa binafsi nimeyashuudia haya kwa watu tofauti tofauti ila moja toka kwa ndugu yangu mpendwa na ningependa ni share kidogo kwenu kipi kilitokea, kwa ajili ya mfano ata kwa wale wanaotarajia kujiunga vyuoni mwezi wa 9 mwaka huu.

Nikiwa nimemaliza mwaka wa pili chuo niko nyumbani napiga field, Gafla akaja mdogo angu mtoto wa mama angu mdogo ndio amekuja kufanya masuala yao haya kujiunga chuo, kuangaika na habari za TCU na bodi ya mikopo nk.

Alikua kamaliza form six na kapata Two yake safi kabisaa, kwaio ktk kufanya harakati kama kaka na mzoefu kwa kipindi icho nikamchagulia baadhi ya shahada ambazo anapaswa kusomea na tukashauriana pale nk. Muda ukapita akachaguliwa UDOM.

Siku zikapita dogo kaenda chuo na mie nikaendelea na mambo yangu, sasa tukawa tunawasiliana na huyu mdogo angu, dogo anacheka sanaa et kaenda chuo cha kata ila kwakua kapata boom yaani kila kitu fresh tu na kozi anayosomea yeye ndo kwanza ilikua imeanza haina muda mrefu ni hii "Environmental Engineer", mwenyewe nikastuka nkasema ndio kitu gani iki mdogo angu? Uinjinia wa mazingira mbona hii kali? akasema tu alivyofika chuo alibadilisha kozi na sio ile nnayoifaham.

Dogo akadai ooho kashauriwa na wenzake kua hio course ni nzuri sana ukimaliza chuo wee fasta tu unatoka, wenyewe wanaitana "wana wamenishauri" sikua na hofu nae dogo ni smart sanaa ata four alipigaga one nzuri tu.

Sasa dogo nae akawa haeleweki anakiponda chuo chake icho icho na anajisifia tu "bro mie hatari nimekutana na super mbururaz madebe matupu humu class mie ndo mwalimu wao na nini" miezi minane ya chuo ikafika dogo akafanya final examination akamaliza chuo.

Siku zikapita matokeo yao yakatoka dogo kaenda na maji, kapata automatic discontinue, GPA poor sanaa, sasa hapa hakuna aliejua wa nyumbani wala wale "wana", mie nimepanga chumba kimoja wakati ule dogo kaja kuishi kwa kaka, ila sasa nikaanza kustuka dogo hayuko kawaida, akawa anapenda sana pombe muda mwingine anakuja usiku kalewa sanaa mie nachukia sanaa, asubuhi namkanya anaona aibu sana hayuko sawa kabisaa.

Akipigiwa simu hapokei, akiwa ana chat whatsap unaona ka alama ka ku Mute chats za ma group, na mie ni mtu wa machale machale sanaa kama Jack Bauer nkajua huyu dogo ana tatizo la ki academic na sio vingine kabisaa.

Hizi stress ni either kapata ma sup ya kutosha au ana ma carry ata matatu huyu iki kitu kinamuumiza, sasa kila usiku tumelala hiv nastuka dogo hayupo kalala chini ya kitanda na kama ana lia hivi ukimsemesha wew vp bwanaa anadai alikua anakoroma tu mara sijui kafikaje hapo chini labda wachawi wamemtoa kitandani wakamlaza hapo.

Sasa kila nikimwambia mdogo angu sie wote wanaume kaka ako nimekaa chuo kikuu miaka mingi nnajua matukio karibu yote, niambie bhana nini tatizo, dogo "oooh bro its nothing".
,
Siku moja kaenda kuoga kaiacha simu yake hapo nikaichukua fasta nikazama mtandao "operamin" nkakuta kijana haku log out kwenye akaunt zao za chuo za matokeo, daaah nlichokiona asee sikuamini macho yangu, dogo kwa pale juu kaandikiwa DISCONTINUE nkasema baasi ni iki ndio kinacho mtesa, daaah hatari hii.

kufupisha tu stori ilimchukua muda sana dogo kurejea hali yake, haikua rahisi kueleweka hata kwa familia tu, poteza repitition aliyoijenga kwa miaka miaka mingi ndani ya siku moja tu,,, ila kuna maisha baada ya matatizo, dogo yuko chuo tena, ni dhambi kubwa kukata tamaa.


Muwe makini tu vijana, na samahani kwa gazeti hili
 
Kwa utafiti wako mkuu nini kilisababisha dogo ku Disco ni vile kuwa anakidharau chuo sijui cha kata ama alikutana na maisha yapi yakambadili hapo chuo ?
 
dogo aliingia kichwa kichwa na kozi yake ya uinginia wa mazingira... dooh! hii tanzania sijui inaenda vipi! sasa huo uinginia wa mazingira ndio upoje? wadau..
 
Kwa utafiti wako mkuu nini kilisababisha dogo ku Disco ni vile kuwa anakidharau chuo sijui cha kata ama alikutana na maisha yapi yakambadili hapo chuo ?

Ndugu yangu nlishindwa kujua nini tatizo, maana dogo hakua mtu wa starehe hizi, ni smart na ana uelewa mzuri tu, ila nlichomsoma labda overthinking ndio ilimfelisha, hakuwai kusema nini kisa hasa nae alikua na wakati mgumu sana.
 
dogo aliingia kichwa kichwa na kozi yake ya uinginia wa mazingira... dooh! hii tanzania sijui inaenda vipi! sasa huo uinginia wa mazingira ndio upoje? wadau..

Inaitwa Environmental Engineering, ni mpya hii, hahahaahahahah
 
uli ingilia privay ya mtu, kwani alikuruhusu uangalie info zake? ni kosa hilo

Kasome kesi ambayo wale FBI waliwapeleka Apple mahakamani waruhusu kudukuliwa kwa taarifa za watu ambao ni suspect, na usome kwnin mahakama iliruhusu.
 
Alienda kusoma kama sekondari akavikuta vshawishi vya mitungi na mikasi chezea chuo? Lakin kwa mwanaume ambae umeenda ukijitambua unaenda wp no cary no disco ukikoxea ka sup nako co kila mwaka.wanaokwenda na tu one ndo wanaongoza Kusup meen
 
Npo hapa wadau namalizaa mwez ujao kiukweli UDOM sio chuo cha mchezo - shule yangu yaa advance tulikuja hapa kadhaa had leo 6 wapo nyumban .KWA WANAODANGANYIKA KWAMBA UDOM CHUO CHA KATA wanapotea sana tumeaza kuwashaur madogo kama ww n mtt wa mama nenda private report ya vyuo mwaka huu kitu kama mwezi 3 ilisema UDOM inaongoza wanafunz kudsco ndo wale wanaojua chuo bata .. mm na wagum tunadum tunaiaga chimwaga soon .HABARI NDO HIYO.
 
Alienda kusoma kama sekondari akavikuta vshawishi vya mitungi na mikasi chezea chuo? Lakin kwa mwanaume ambae umeenda ukijitambua unaenda wp no cary no disco ukikoxea ka sup nako co kila mwaka.wanaokwenda na tu one ndo wanaongoza Kusup meen


hahahahaah vijana nyie wa siku hizi mna mabalaa sana.
 
Kasome kesi ambayo wale FBI waliwapeleka Apple mahakamani waruhusu kudukuliwa kwa taarifa za watu ambao ni suspect, na usome kwnin mahakama iliruhusu.
braza hukufuatilia kesi
FBI waligaragarazwa kote, baadaye wali drop case kwa kuwa wanadai walipata njia yao ya ku unlock ile simu ya Farouk. ambayo ndio ulikuwa msingi wa kesi nzima. so its like Apple still won kwa kuwa yenyewe haikutoa taarifa yyte ya wateja wake ambayo ilikuwa ni haki yao ya privacy.
halaf wewe hukuwa FBI uli ingilia personal info za mtu ambazo hazikuwa zikihatarisha usalama wako wala wa taifa. you are still wrong
 
Npo hapa wadau namalizaa mwez ujao kiukweli UDOM sio chuo cha mchezo - shule yangu yaa advance tulikuja hapa kadhaa had leo 6 wapo nyumban .KWA WANAODANGANYIKA KWAMBA UDOM CHUO CHA KATA wanapotea sana tumeaza kuwashaur madogo kama ww n mtt wa mama nenda private report ya vyuo mwaka huu kitu kama mwezi 3 ilisema UDOM inaongoza wanafunz kudsco ndo wale wanaojua chuo bata .. mm na wagum tunadum tunaiaga chimwaga soon .HABARI NDO HIYO.


Hongera mkuu, kazeni.
 
braza hukufuatilia kesi
FBI waligaragarazwa kote, baadaye wali drop case kwa kuwa wanadai walipata njia yao ya ku unlock ile simu ya Farouk. ambayo ndio ulikuwa msingi wa kesi nzima. so its like Apple still won kwa kuwa yenyewe haikutoa taarifa yyte ya wateja wake ambayo ilikuwa ni haki yao ya privacy.
halaf wewe hukuwa FBI uli ingilia personal info za mtu ambazo hazikuwa zikihatarisha usalama wako wala wa taifa. you are still wrong

United States Magistrate Judge Sheri
Pym has asked Apple to provide
“reasonable technical assistance” to
investigators — which means help
bypass an auto-erase function that gets
activated when the wrong pin or
password is entered for a fixed number
of times; allow FBI to submit unlimited
passcodes via a computer, a programme
or whatever protocol they determine;
and ensure that the Apple software
doesn’t purposely add any additional
delay between password attempts to
unlock the device. Apple is also required
to load a specific iOS recovery file on to
the device so that FBI can recover the
passcode. This version of iOS will
ensure that the auto-erase function
doesn’t get enabled. FBI basically wants
to ensure that it doesn’t spend an
indefinite length of time trying to
unlock this iPhone.

New York Times hili la 21 march 2016.

na vile vile FBI waliichunguza hii simu vizuri tu, na Kesi ya pili ya Apple dhidi ya serikali walilipinga hili swala ambalo hao FBI walitaka liwe endelevu, ndipo walishinda hio kesi.

Sasa na mim nlikua ni lazima nifanye kila namna kujua nini tatizo la mdogo angu, sikua na njia nyingine zaidi ya hio.
 
United States Magistrate Judge Sheri
Pym has asked Apple to provide
“reasonable technical assistance” to
investigators —
sasa wewe ulifuatilia kesi nusu, niulizr mie madau wa hiyo kesi
soma hapa

The FBI has unlocked Farook’s iPhone 5c involved in the San Bernardino shooting using an alternative method that didn’t involve Apple. Given this new development, the Department of Justice is dropping the case. The government has been evasive about this alternative method and didn’t provide additional details.
The filing is very succinct. “The government has now successfully accessed the data stored on Farook’s iPhone and therefore no longer requires the assistance from Apple Inc. mandated by Court’s Order Compelling Apple Inc. to Assist Agents in Search dated February 16, 2016,” U.S. attorney Eileen M. Decker and assistant U.S. attorney Tracy L. Wilkison wrote.
The technical Crunch 28 March 2016

au kaingia kwenya Archive ya attorney Wilkson ya twitter ujionee.

hiyo kesi iliisha April 2 ambapo FBI walitangaza wameweza ku unlock sim baada ya kununua software ya ku unlock code ya iphone 5c tuu na walinunua kwa Usd milion1.3, Apple mpaka mwisho hawa ku wa assist hao jamaa.
na James Comey alithibitisha later in April 7 2016. kuwa apple hawaku wa assist jamaa ku pata passcode. na later on kuna jaji wa Brklyn Magistrate alisema FBI haiez tumia writ act ku walazimasha apple watoe info, by Aprill 22 kesi zoote za FBI zilifungwa kwakuwa walikuwa washapata pass code kwa namna yao wenyewe tena kwa sabab za ki usalama.

wewe mdogo wako hakuwa ana pose threat yoyote kwako zaid zaid ni wewe ndio ulikuwa curious kujua kwa nn kabadilisha stail ya maisha ambayo si sababu ya kukufanya wewe uingilie privacy yake labda ungeenda na wewe kwenye vyombo vya dola kudai akuoneshe ni nin anaficha kwa sim yake kwa hiyo hata wewe writ act isinge apply kwako mzeiya, kwanza hata mahakamani ungeshindwa vibaya sana
ulokosea tu.
 
Back
Top Bottom