666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,688
- 3,816
Huku tukiwa na mapumziko ya siku chache ya sikukuu hii tukufu kabisa ya Iddi,basi ningependa leo niwakumbushie mawili matatu tu hawa wadogo zetu ambao bado wako ma vyuoni humu nchini, na ambao sasa hivi uenda wakawa wako kwenye kipindi cha mitihani yao ya kumaliza mwaka (UE), au ndo wako wanajiandaa, tunakumbushana tu.
Hakika hakuna kitu kibaya kama kuona ndoto yako inakatishwa mchana kweupe na watu wachache tu, vuta picha ni maumivu kiasi gani kupewa taarifa kua "bhana kuanzia siku hii wewe sio mwanachuo tena, ndoto zako mwisho leo, na mkopo ndio baibai hivyo, ume disco mzee rudi kwenu mwaka mzima bure mzee" sasa mbaya zaidi anayoambiwa haya ni kijana mdogo tu asie na ukomavu wa kimaisha tena walio wengi ndio hawa fresh from school wanaamini chuo ndio maisha yao ndio kila kitu kwao.
Sasa bila kusahau ku disco ni jambo dogo tu na uenda isiwe kaazi kiviile, maana kunatakiwa mtu ajichanganye kidogo tu na apate sare Supplimentary 4 tu kwa mwaka kwa baadhi ya vyuo, au Sup. 5 basi ambazo ni mitihan tu mwanafunzi anaweza kuamka vibaya akabaka maswali akaenda na maji ghafla discontinue hio hapo.
Sasa nyakati hizi ni vyema basi wadogo zetu mkawa bize na mambo ya kimasomo, pigeni discussion za maana, someni sana hata kama hamuelewi ivyo ivyo kazeni tu, salini sanaa na punguzeni mizaha zaha hio, ila kikubwa mjifunze kujituliza wenyewe kama kufanya meditation ya numbers ili mjifunze kutokupanic uko mbeleni, mengine mnayajua wenyewe yazingatieni haya.
sasa binafsi nimeyashuudia haya kwa watu tofauti tofauti ila moja toka kwa ndugu yangu mpendwa na ningependa ni share kidogo kwenu kipi kilitokea, kwa ajili ya mfano ata kwa wale wanaotarajia kujiunga vyuoni mwezi wa 9 mwaka huu.
Nikiwa nimemaliza mwaka wa pili chuo niko nyumbani napiga field, Gafla akaja mdogo angu mtoto wa mama angu mdogo ndio amekuja kufanya masuala yao haya kujiunga chuo, kuangaika na habari za TCU na bodi ya mikopo nk.
Alikua kamaliza form six na kapata Two yake safi kabisaa, kwaio ktk kufanya harakati kama kaka na mzoefu kwa kipindi icho nikamchagulia baadhi ya shahada ambazo anapaswa kusomea na tukashauriana pale nk. Muda ukapita akachaguliwa UDOM.
Siku zikapita dogo kaenda chuo na mie nikaendelea na mambo yangu, sasa tukawa tunawasiliana na huyu mdogo angu, dogo anacheka sanaa et kaenda chuo cha kata ila kwakua kapata boom yaani kila kitu fresh tu na kozi anayosomea yeye ndo kwanza ilikua imeanza haina muda mrefu ni hii "Environmental Engineer", mwenyewe nikastuka nkasema ndio kitu gani iki mdogo angu? Uinjinia wa mazingira mbona hii kali? akasema tu alivyofika chuo alibadilisha kozi na sio ile nnayoifaham.
Dogo akadai ooho kashauriwa na wenzake kua hio course ni nzuri sana ukimaliza chuo wee fasta tu unatoka, wenyewe wanaitana "wana wamenishauri" sikua na hofu nae dogo ni smart sanaa ata four alipigaga one nzuri tu.
Sasa dogo nae akawa haeleweki anakiponda chuo chake icho icho na anajisifia tu "bro mie hatari nimekutana na super mbururaz madebe matupu humu class mie ndo mwalimu wao na nini" miezi minane ya chuo ikafika dogo akafanya final examination akamaliza chuo.
Siku zikapita matokeo yao yakatoka dogo kaenda na maji, kapata automatic discontinue, GPA poor sanaa, sasa hapa hakuna aliejua wa nyumbani wala wale "wana", mie nimepanga chumba kimoja wakati ule dogo kaja kuishi kwa kaka, ila sasa nikaanza kustuka dogo hayuko kawaida, akawa anapenda sana pombe muda mwingine anakuja usiku kalewa sanaa mie nachukia sanaa, asubuhi namkanya anaona aibu sana hayuko sawa kabisaa.
Akipigiwa simu hapokei, akiwa ana chat whatsap unaona ka alama ka ku Mute chats za ma group, na mie ni mtu wa machale machale sanaa kama Jack Bauer nkajua huyu dogo ana tatizo la ki academic na sio vingine kabisaa.
Hizi stress ni either kapata ma sup ya kutosha au ana ma carry ata matatu huyu iki kitu kinamuumiza, sasa kila usiku tumelala hiv nastuka dogo hayupo kalala chini ya kitanda na kama ana lia hivi ukimsemesha wew vp bwanaa anadai alikua anakoroma tu mara sijui kafikaje hapo chini labda wachawi wamemtoa kitandani wakamlaza hapo.
Sasa kila nikimwambia mdogo angu sie wote wanaume kaka ako nimekaa chuo kikuu miaka mingi nnajua matukio karibu yote, niambie bhana nini tatizo, dogo "oooh bro its nothing".
,
Siku moja kaenda kuoga kaiacha simu yake hapo nikaichukua fasta nikazama mtandao "operamin" nkakuta kijana haku log out kwenye akaunt zao za chuo za matokeo, daaah nlichokiona asee sikuamini macho yangu, dogo kwa pale juu kaandikiwa DISCONTINUE nkasema baasi ni iki ndio kinacho mtesa, daaah hatari hii.
kufupisha tu stori ilimchukua muda sana dogo kurejea hali yake, haikua rahisi kueleweka hata kwa familia tu, poteza repitition aliyoijenga kwa miaka miaka mingi ndani ya siku moja tu,,, ila kuna maisha baada ya matatizo, dogo yuko chuo tena, ni dhambi kubwa kukata tamaa.
Muwe makini tu vijana, na samahani kwa gazeti hili