#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
(Reuters) - Britain is banning all arrivals from Tanzania and Democratic Republic of Congo from Friday to stop the spread of the South Africa COVID-19 variant, transport secretary Grant Shapps said in a tweet on Thursday.

"All passengers from these countries except British & Irish Nationals and third country nationals with residents rights will be denied entry," Shapps wrote in his tweet.

==========

Wasafiri kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watazuiwa kuingia Uingereza kwenye harakati za kujaribu kuzuia kirusi kipya cha Covid-19 kutoka Afrika ya Kusini.

Lakini marufuku hiyo itakayoanza Ijumaa saa 10 usiku haitawahusu raia wa Uingereza na Irish na wote wenye haki za makazi nchini Uingereza wanaorudi nchini humo, alisema katibu mkuu wa usafiri, Grant Shapps.

Hii imekuja baada ya mshauri mkuu wa kisayansi nchini Uingereza, Sir Patrick Vallance kuonya chanjo ambayo kwa sasa inatolewa inaweza kuwa haina nguvu sana dhini ya kirusi kutoka Afrika ya Kusini.

Kirusi tofauti cha Covid kinachojulikana kama 501Y.V2 kina uwezekano wa kusambaa haraka zaidi kwa asilimia 50 zaidi ya mwanzo.

Soma > UK bans passengers from Tanzania, Democratic Republic of Congo to control spread of COVID variant
 
Sasa Hivi tujikite kutengeneza fedha, baadaye dawa rasmi ikipatikana tutaenda. Waache waje tupate pesa, sie tujifukize tusife ili siku za usoni waone kuwa wao walikosea

Unasema je kama tuliokosea ni sisi? Ama kweli "nyani haoni kundule."

Eti tuendelee kujifukiza tusife hadi dawa rasmi ipatikane. Kwa nini kujifukiza kusiwe ndiyo dawa rasmi basi?

Eti tuendelee kutengeneza pesa!

Hii inaitwa, "tamaa mbele, mauti nyuma."

Mawazo duni kabisa.
 
Unasema je kama tuliokosea ni sisi? Ama kweli "nyani haoni kundule."...
Kwa mawazo finyu unaweza kufikiri lockdown ni solution. Mbona haijesha huko Ulaya na Marekani? Hivi unajua kuwa wengi tumeipata na tumevuka? Siamini kupigana na zimwi lisiloonekana bali kujizatiti tu.

Najua wewe ni mpinzani ila kumbuka kwa suala hili njia tuitumiayo ndiyo njia sahihi kwa hali ya covid ilivyo. Nakuacha na rejea ya Gazeti lenu linalosema wanatibu.

A medical doctor at Aga Khan Hospital, in the city centre – who prefers not to be mentioned, without giving the exact number of those infected by Covid-19, said the number has been growing but most of them do recover after three to four days. He did not disclose the prescriptions.

Aga Khan hospital has reportedly developed a special formula for the treatment of Covid-19.

He said most of the patient comes with respiratory complications, high fever and sometimes headache, are clinically plaid and when diagnosed with Covid-19 are admitted with special supervisions – and starts treatments.

Full story Fresh Corona fears hit "Covid-free" Tanzania - Sauti Kubwa
 
Lakini hii sirikali yetu inachekesha sana, ni kweli maambukizi ya korona sio makubwa nchini. Kuna ubaya gani wa kutoa data za hao wagonjwa?

Nchi yetu sio kisiwa ina muingiliano na mataifa mengine yaliyoathirika sana na wala ugonjwa huu sio wa aibu haujaanzia kwetu...kuna tatizo gani kusema hali yetu nchini kuhusu korona ikoje.

Yaani li sirikali lipo kimya japo hata kuendelea kuhamasisha raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa ambao dhahiri bado ni tishio duniani.
 
Ilitosha tukakubaliana corona ipo, lakini tunaidhibiti ipasavyo.

Hivyo hatuna maambukizi mengi kama wenzetu.

Nadhani ingetupa heshima zaidi kuwa ni taifa linalojitambua.
 
"Wengi tumeipata na tumevuka." Hayo ni maneno yako.

Sina hakika kama waliotangulia au jamaa zao wanaweza kuwa na kauli fyongo kama hiyo. Wako wapi wale wabunge, yule mstaafu na wengi wengine achilia mbali wasiokuwa na majina makubwa makubwa nao kuwa habari?

Aliyesema "usipoziba ufa utajenga ukuta" hakuwa mjinga kihivyo.

Kwamba Agha Khan wana tiba? Kwani hawazijui medical journal zinazoshughulika na taarifa nyeti kwa afya ya dunia na kwenye dharura kama hii?

Warundi wahead nyie. Msitake kutufanya sote tu mazuzu wa kumshabikia Mrundi mwenzenu kijinga jinga tu hata kama tunaopukitika ni sisi.

Hata hivyo mola wetu ni mkubwa na tulipo yetu macho. Wako wapi kina Nkurinziza?

Eeh mola wetu na ukatudhihirishie ukuu wako dhidi ya miungu watu hawa wanaojitanua na kutelekezea watu wako gonjwa linaowapukutisha hali lingeweza kuepukika. Na ikawe fundisho kuwa kwa hakika hayupo aliye mkuu Ila wewe.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom