Kudhibiti COVID-19 na kuepuka kulishana uchafu, tuweke sheria ya kupiga faini yeyote atayepiga chafya hadharani bila kuziba pua na mdomo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,994
144,329
Hata kabila ya ujio wa Covid, hakuna tabia ambayo huwa naichukia kama mtu kupigya chafya mbele za watu bila kuziba pua na mdomo kwani mbali na kusambaza magonjwa, lakini pia inachangia sana kulishana uchafu(makamasi).

Kutokana na ujio wa Covid, ugonjwa unaosambaa kwa njia kadhaa ikiwemo mtu mwenye virusi vya Covid kupiga chafya hadharani bila kufunika pua na mdomo, napendekezat tuweke utaratibu wa kisheria wa kutoa adhabu ya mtu kulipa faini kwa kupiga chafya hadharani bila kuziba pua na mdomo.

Kwakuwa hoja si tu kuziba pua na mdomo,bali ni kufanya hivyo kwa kutumia kiwiko na si kiganja cha mkono, iwe pia ni kosa kuziba pua na mdomo kwa kutumia kiganja wakati wa kupiga chafya au kukohoa.

Hii tabia licha ya kusambaza magonjwa, lakini kiukweli inakera sana.Mfano, mko ofisini na mna-share kifaa kama computer, ghafla unaona mwenzako anapiga chafya na anaziba pua na mdomo au asizibe kabisa na akiziba anaziba kwa kutumia kiganja cha mkono wake.

Inafika hatua unatamani uondoke ofisini au ikiwezekana utumie laptop yako kama hilo linawezekana kwasababu licha ya kusambaza uchafu, anakuondolea amani ya kufanya kazi kwa hofu ya kuambukiza mariachi (Covid).

Hata tabia ya kukohoa na kuziba mdomo kwa kwa kiganja cha mkono nayo haina tofauti na kupiga chafya na kuziba mdomo kwa kiganja cha mkono au kutoziba kabisa.

Naelewa kabisa utekelezaji wa sheria kama hii utakuwa mgumu sana( kwa mfano jinsi ya kumkamata watu,n.k) ila kwa kitendo tu cha kuweka sheria au utaratibu kama huu na kuutangaza, binafsi naamini itasaidia sana kupunguza hii tabia kwani watu wataogopa kupiga chafya au kukohoa bila kukinga wengine maana atakuwa hajui nani anaweza kumkamata.

Kama tumewahi kuwa na sheria inayosema ni kosa kumkonyeza mwanamke(niliwahi sikia kuhusu hii sheria), iweje iwe ni ajabu kuwa na sheria kama hii itayolinda afya zetu?

Binafsi naamini tukiwa na utaratibu kama huu na tukautangaza sana katika media, hatua hii itasaidia sana ku- create awareness mbali na kuwafanya watu wawe waoga kupiga chafya au kokohoa hadharani pasipo kuchukua tahadhari za kulinda wengine.

Ningekuwa na kampuni yangu na nimeajiri watu,ningeweka utaratibu Katika ofisi yangu wa kumrudisha nyumbani na kumkata malipo ya kiwango fulani (tutachokubaliana) mtumishi ataepiga chafya au kukoa bila kuchukua tahadhari akiwa ofisini.

Vyuoni na Katika mashule, utaratibu unaweza kuwa ni mwanafunzi ataepiga chafya au kukohoa bila kukinga wengine adhabu yake ni kutolewa nje ya kipindi au kutohudhuria vipind vyote kwa siku usika. Aibu hii itatosha kupunguza hii tabia ingawa inaweza tumiwa vibaya na wanafunzi wasiopenda kuingia darasani (watoro).

Mnaweza kuona nimeleta mada ya kushangaza na isiyotekelezeka, lakini ukweli ni kwamba, hivi vitu tunavyovipuza ndio vinavyotugharimu.

Watu tunakosa ustaarabu kupita kiasi.
 
Kwanini Kirusi cha Korona kinabadilika kila wakati na sio kile cha UKIMWI?

Wametengeneza chanjo wa Korona ndani ya Mwaka Mmoja ila ya UKIMWI wameshindwa ndani ya miaka zaidi ya 20?
 
Hata kabila ya ujio wa Covid, hakuna tabia ambayo huwa naichukia kama mtu kupigya chafya mbele za watu bila kuziba pua na mdomo kwani mbali na kusambaza magonjwa, lakini pia inachangia sana kulishana uchafu(makamasi).
Wafundishe watoto wako kupiga chafya kwa staha wakiwa home.

Tabia njema kwa mtoto huanza kufundishwa nyumbani pamoja na katika taasisi za dini (kanisani/msikitini/madrasa) tena angali akiwa bado mdogo sana.

Wazazi pamoja na viongozi wa dini wakitimiza wajibu wao ipasavyo wanakuwa wanapunguza mzigo mkubwa sana kwa dola/serikali.
 
Kwanini Kirusi cha Korona kinabadilika kila wakati na sio kile cha UKIMWI?

Wametengeneza chanjo wa Korona ndani ya Mwaka Mmoja ila ya UKIMWI wameshindwa ndani ya miaka zaidi ya 20?
Covid inapona tofauti na HIV, sasa unapomuwekea mtu live virus wa HIV maana yake umempa maambukizi ya maisha. Nani atakubali jaribio hilo wakati jaribio la Covid una uhakika unaweza kupona.
 
Zamani kupiga chafya hadharani ilikuwa ni kitu cha kawaida tu na watu wanakwambia “bless you” siku hizi watu wanahofia na kuzibana chafya au ukipiga wanakukata jicho 🤣🤣🤣🤣 utadhani umetenda kosa kubwa sana ukipiga mbili wanaanza kusogea mbali nawe 🤣🤣🤣
 
Covid inapona tofauti na HIV,
jaribio la Covid una uhakika unaweza kupona.
Wakati nipo secondary mwalimu wangu wa Biology alinifundisha kuwa virusi vyote havina dawa. Ndio maana hata mafua pia ni virus lakini hayana dawa bali yanapotea kwa muda lakini baadae yanarudi.

Sasa sijui ni nani yupo sahihi hapa dada yangu.
 
Zamani kupiga chafya hadharani ilikuwa ni kitu cha kawaida tu na watu wanakwambia “bless you” siku hizi watu wanahofia na kuzibana chafya au ukipiga wanakukata jicho 🤣🤣🤣🤣 utadhani umetenda kosa kubwa sana ukipiga mbili wanaanza kusogea mbali nawe 🤣🤣🤣🥰🥰🥰
Tunaoneana aibu na hiki ndio kitu kinachotugharimu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwanini Kirusi cha Korona kinabadilika kila wakati na sio kile cha UKIMWI?

Wametengeneza chanjo wa Korona ndani ya Mwaka Mmoja ila ya UKIMWI wameshindwa ndani ya miaka zaidi ya 20?
Kama una muda soma hii makala utajibiwa maswali yako.
 
Back
Top Bottom