Mzalendo39
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 882
- 1,029
Watanzania wengi wanasahau walipotokea na kuziita Imani zao za kale kuwa za kishirikina. Katika historia Dini tunazoabudu hivi sasa zilikuja kwa meli (Wazungu) na kabla ya hapo tulikuwa na imani zetu zilizotuongoza kabla ya Wazungu na Waarabu.
Imani zetu hazina tofauti na lugha zetu za asili pamoja na kiswahili ambacho hivi sasa kinazidi kudumazwa na lugha za kigeni (Kingereza) kupewa chapuo hadi kufundishia mashuleni.
Kwa sasa imani zetu Watanzania na asili zetu zimeendeleatupiliwa Mbali hadi kufikia kuitwa Imani za kishirikina. Ni vyema serikali ikatoa uhuru kwa imani zote tulizonazo kama wanavyopigia chapuo Imani za wazungu na Waarabu.
Mimi nimezaliwa bila dini yoyote ya Wazungu nitaendelea kuwa na imani nilizozikuta toka kwa babu zangu.