Kudharau Lugha Zetu Za Asili Ni Kumdharau Mungu.


Jacobus

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Messages
3,900
Points
2,000
Jacobus

Jacobus

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2011
3,900 2,000
Huwa najiuliza hivi lugha zote hapa duniani zina aliyezianzisha? Kama pana mtu ajuaye kuwa labda Kinyamwezi kaanzisha mtu fulani naomba kufahamishwa.
Nimeonelea kulisema hili maana pana juhudi za kuziua lugha zetu za ASILI na kudandia za nje. Wizara yetu ya Utamaduni ingejitahidi lau kuchukuwa maneno ya lugha zetu za asili kukijenga kiswahili lakini hawafanyi hivo. Angalia neno shikamoo kufanywa ni salamu hii haina maana kabisa, neno hili halina uhusiano wowote na kusalimiana maana nijuavo salamu ni kujuliana hali.
Naomba sana sana wadau tuwaeleze waliopo wizarani wasikae tuu na kungoja mshahara bali wachukue maneno toka katika lugha zetu za asili na kukijenga kiswahili pia pawe na vitabu kwa lugha zetu za asili ili tuwe tunajifunza. Kwa nini iwe rahisi kujifunza kiingereza, kifaransa, kichina n.k. na kuwa mwiko kujifunza KINYAMWEZI, KIGOGO, KIHEHE n.k.?
Tusimkufuru Mola kwa hili. Mungu aepushe mbali.
 

Forum statistics

Threads 1,295,830
Members 498,404
Posts 31,224,572
Top