Kudhani kuwa Lowassa kawazidi Lipumba, Slaa kura za urais ni uwendawazimu

gwamaka aswile

Senior Member
Mar 26, 2015
186
195
Kuna mjadala unaendelea sehemu mbalimbali, mitandaoni, mitaani na barabarani. Kuna watu ambao wanafuatilia siasa kishabiki zaidi wanadai kuwa lowassa amewazidi Dkt.Slaa na Lipumba kwa kura za urais na kwamba kama ukawa ungewasimamisha wao wangeshindwa zaidi. Huku ni kujidanganya na kukejeli jitihada za dhati za ujengaji wa demokrasia zilizofanywa na Slaa na Lipumba kwa muda mrefu. Hili hitaji la kudai 'mabadiliko' la sasa haliwezi kusheherekewa bila ya kumtaja Slaa na Lipumba watu ambao wameweka rehani maisha yao kwa nyakati tofauti na kuibua hoja na mijadala iliyowafanya watanzania wakaamka na kuwa macho. Kuna tofauti kubwa sana kati ya uchaguzi wa 2015 na zilizopita.

Uchaguzi huu upinzani ulisimamisha mgombea mmoja katika urais, miaka ya nyuma kila chama kilisimamisha mgombea wake, aidha mwaka 2015 maeneo mengi UKAWA wamesimamisha mgombea moja mmoja, wakati miaka ya nyuma kila chama na mgombea wake. Mwaka huu UKAWA imepata msaada wa kifedha toka kwa wadau wengi tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu CCM ilikuwa na mpasuko mkubwa tofauti na miaka ya nyuma. Halafu mtu anasema eti Lowassa ni zaidi ya Slaa au Lipumba huu ni uwendawazimu! Na ni muendelezo wa ushabiki na ufuasi wa watu wenye akili fupi ambao hadi sasa hawajajua sababu ya upinzani kushindwa badala yake wanaendelea kusambaza propaganda za kuibiwa kura.

Kama tunataka kuwalinganisha wagombea Lowassa anakuja kuwa mtu wa mwisho kwa wagombea wote wawili lipumba na slaa. Kwanini? Kwanza, lowassa si mwanasiasa, ni msanii na mtu anayependa kutumia fursa (opportunist) ni mtu ambaye amekulia kwenye raha na ni wazi hata dhumuni lake la kuingia katika siasa halikulenga kubadilisha maisha (alijiunga na CCM baada ya kumaliza chuo kikuu) ni mtu aliyejiunga na chama kiulaini akiwa bado na akili za kishule shule bila kuwa na uchungu wala vission yoyote na huko akapanda vyeo na kupata fursa mbalimbali zilizomfanya afikie hadi cheo cha uwaziri mkuu. Mwenendo wake hadi kufikia uwaziri mkuu unatuonyesha kuwa ni mtu wa kutengeneza mitandao ambayo ina malengo ya kumjenga binafsi zaidi kuliko chama au taasisi anayoitumikia.

Tulishuhudia mwaka 1995 alivyotengeneza timu ya kuimba jina lake kwenye vikao vya CCM ili apitishwe kirahisi, hali hii imejirudia 2015 kila mtu kaona. Pili, Lowassa hana uwezo wa kujenga hoja hajawahi kuanzisha mjadala wowote bungeni wenye maslahi ya kitaifa kupinga ufisadi au chochote. Zaidi ni mmoja wa wabunge bubu. Tangu atoke uwaziri mkuu hadi juzi bunge limeisha Lowassa hajashiriki mjadala wowote wenye mlengo wa kitaifa. Bila shaka Lowassa nguvu yake ya kuongea huendana na nafasi aliyopo. Akiwa na cheo mathalani waziri mkuu hivi, basi ndipo tunamuona akitoa amri na maagizo.

Lowassa ni kiongozi aina ya nyapara, aina ya mtu anayependa kutoa maagizo na kutaka watu watekeleze na wakati mwingine bila kupima kama maagizo hayo yanatekelezeka. Hii ni kinyume na slaa na Lipumba, viongozi hawa ni wachambuzi ambao wameshiriki mijadala mbalimbali wakaibua hoja ambazo kiuhalisia zimelisaidia taifa. Wamepinga waziwazi wasichokiamini na kusimama katika misimamo yao.

(Lipumba alitoka ktk bunge la katiba, slaa alipumzika siasa baada ya Lowassa kubaka demokrasia UKAWA). Kitu pekee kinachomtofautisha Lowassa na Slaa na Lipumba ni uwezo wake mkubwa wa kifedha ambazo nazo hazijulikani alivyozipata. Ni fedha hizo ambzo zimekuwa zikimjengea umaarufu na kumfanya watu hata viongozi wakubwa wa CCM na upinzani wamfuate. Lakini kisiasa, nooo! Lowassa yuko chini sana chini sana hata Mnyika, Zitto, Makamba Januari. Hawafikii hata kidogo. Kumfananisha Lowassa na Slaa, Lipumba, Kikwete na hata Hashimu Rungwe ni kuitukana demokrasia!
 

Africa one

JF-Expert Member
May 6, 2013
240
250
Uchambuzi wako umetumia sanaa zaidi badala ya sayansi(namba) ni mawazo yako lkn.
 

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,402
1,500
Mzima wa lowasa kumnyika haki utawaandama sana. Mkilala mnamuota mnawai huku justify utapeli wenu ila bado mnakwama!
 

rofejo

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
516
250
Sio kawapita kina Slaa na Lipumba bali kampita hata magu kwa kura nyingi sana!! hata magu anajua kamchezo kalikofanyika,na lazma nafsi inamsuta!
 

Ngoshanyi

JF-Expert Member
Jun 14, 2013
2,460
1,500
Hawa jamaa ni vichaa,malofa na mapumbavu. Lowassa kaingia kugombea Chadema@Ukawa na kukuta kazi kubwa ya uhamasishaji wa kujiandikisha umesharatibiwa na kufanywa na Dr Slaa na Pr. Lipumba. Kwa sababu ya ulofa na upumbavu wao wa kumsikiliza Dj Mbowe kuwa Lowassa anakuja na mamilioni ya watu na viongozi wamemuamini. Mimi naona hata wabunge kumi waliongezeka Chadema ni wale wa Masaini na Uchagani. Otherwise Workdone ni 0%
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
12,709
2,000
Ungetulia, huu uzi wako ungeuandika kwa angalau sio chini ya aya nne.
 

Mkomamanga

JF-Expert Member
Dec 9, 2011
816
225
Aliyezidi au kuzidiwa ni hoja gani kwa sasa? Demokrasia imekua au imerudi nyuma kwa uchaguzi wa mwaka huu? Kwangu ni mjadala huu unapaswa kutupeleka katika uchaguzi wa 2020 na kuiacha Tz ikiwa makini na ikikua kiuchumi na maendeleo ya watu....vinginevyo yote ni siasa za vijiweni hazileti tija
 

Mtingaji

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
1,209
1,225
Kwenye heading nilifikiri mtoa hoja anashusha data za kutetea heading yake, kumbe ulojo tu!!-Kakuna hata idadi yoyote ya kura iliyotajwa!!

Eti Eddo ni Bubu bungeni hakuweza kukemea Rushwa na Ufisadi Bungeni!! Hivi mtu akiwa CCM anaruhusiwa na chama chake kukemea ufisadi na wizi, huyo si kesho yake tu ana anzishiwa zengwe mpaka ataufyata na kufuta kauli zake za kukemea uozo!!

Kama hujui idadi ya kura alizopata Eddo, subiri uone idadi ya wabunge wa upinzani ilivyo ongezeka Bungeni pamoja na kuwadhulumu wagombea wa upinzani ushindi.
 

Faru Kabula

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
12,548
2,000
. Zaidi ni mmoja wa wabunge bubu. Tangu atoke uwaziri mkuu hadi juzi bunge limeisha Lowassa hajashiriki mjadala wowote wenye mlengo wa kitaifa. Bila shaka Lowassa nguvu yake ya kuongea huendana na nafasi aliyopo. Akiwa na cheo mathalani waziri mkuu hivi, basi ndipo tunamuona akitoa amri na maagizo.
-----------------------------------------
-----------------------------------------
Lowassa ni kiongozi aina ya nyapara, aina ya mtu anayependa kutoa maagizo na kutaka watu watekeleze
Unajichanganya mazee. Umesema EL ni bubu, halafu ukaja kusema anapenda kutoa maagizo. Hivi bubu anawezaje kutoa maagizo?
UTAFITI WA TWAWEZA: 67% ya wana CCM ni ...
 

Addict

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
703
500
sawa sasa.shangilieni.sasa mmeshinda hofu ya nini kwa lowasa tena.
 
Top Bottom