Kudandia Life-Cycle ya wazungu ndo kosa letu, tutakoma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kudandia Life-Cycle ya wazungu ndo kosa letu, tutakoma!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nimie, Dec 8, 2011.

 1. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hawa wazungu kufika hapa walipo wametoka mbali na kupitia changamoto kibao. Maendeleo yako yametokana na jitihada katika kutafuta majibu ya shida zao katika mazingira yao. Juhudi hizo zimewasaidia kugundua mambo kibao ambayo leo tunayaita maendeleo. Na mapambano yao hayo yamepita katika vipindi/nyakati mbali mbali. Solultions zingine hazikupatikana kirahisi bali kwa kupitia hatua mbali mbali.


  Tatizo letu Afrika na hasa bongo, matatizo yetu yaliyo katika mazingira yetu hatutaki kusumbua bongo zetu kutafuta majibu ya haja zetu. Kinachofanyika ni kwenda kuchukua solution za matatizo ya Ulaya na kuja ku-apply kwa matatizo yetu Afrika. Tukumbuke matatizo ya ulaya si yote yana kiini na majawabu ya shida za afrika kwa kuwa kuna mazingira tofauti.

  Wakati mwingine wanaweza kuwa na solution ya kutufaa hata sie. lakini wenzetu kufikia solution iliyopatikana wamepitia changamoto na vipindi tofauti. Hivyo basi ili kutumia hizo solution zao inabidi kuwa na background ya hatua za upatikanaji wa solution husika. Hivyo basi solution zingine zinatushinda kuzitumia ipasavyo kwa kuwa hatuna background yake, mara nyingi tunakwama njiani!

  Nadhani tungetumia mbinu zetu wenyewe hata kama kwa taratibu kupata majibu ya matatizo yetu kwa kutumia mazingira yetu na malighafi zetu, watu wetu na akili zetu wenyewe. Sasa hivi tumebaki kuiga kila cha wazungu, hatuwezi tena kuwa na cha kwetu, na ni ngumu mno kutoka katika life cycle ya wazungu. Hatujui mwanzo wao kwa kuwa tumedandia katikati. Hii imetufanya kuwa watumwa na wasindikizaji wa mambo ya wazungu. Kwa msingi huu hatuchomoki na hawa jamaa watatutawala tu.

  Kuna jamaa Iringa miaka ya 80 hivi alianzisha mradi wa kutengeneza mabomba ya maji kwa kutumia mianzi, sijui sana ilikuweje, wazungu wakajiingiza hapo na leo ule mradi haupo tena. Nahisi wameuua tu, ili tubaki kwenye life cycle yao. Wao ndo watubadilishe kutoka kwenye mabomba ya chuma hadi aluminium, aluminium hadi plastics nk. hawa jamaa hawataki tuwe na kitu chetu, kila kitu kikigunguliwa wao ndo wakisajili why! Na kila mkipeleka kitu mnaambiwa kilishagunduliwa na wao!

  Ni lini Afrika tutakuwa na maisha yetu, ugunduzi wetu, solutions zetu na mambo yetu wenyewe kwa mazingira yetu? Fikiria bajeti zetu wanatu-support wao, chaguzi zetu wenyewe tunawaita waje watusimamie, hata nyanya tunazo lakini bado tunaletewa za kutoka kwao kwa kisingizio cha biashara huria. Aibu gani hii?

  Bado nadhani tulikosea kudandia life-cycle ya wazungu, naam tutakoma!

  Ni mtazamo wangu tu, sijui mwenzangu unasemaje.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huyo jamaa anaitwa Nd. Lipangile, wazo lake lilitokana na upungufu mkubwa wa mabomba ya maji ya metal. Na kwa ugunduzi wake huyo ilimfanya akanshinda zawadi ya kitaifa ya ugunduzi. Hata hivyo sababu kubwa ya kufa kwa project yake haitokani kamwe na wazungu kama unavyodai.

  Kipindi cha ugunduzi wa mabomba ya miazi, uchumi wa nchi ulikuwa ni mbaya, hivyo kuja kwa mabomba hayo kulileta matumaini fulani, katika uzambazaji wa maji vijijini. Kabla ya kuanza kutumika kwa mabomba hayo kikazi zaidi, wizara husika iliona ni vema kuyachunguza zaidi mabomba hayo. Hatua hii ni ndefu, na haikufikia mwisho wake kwani uchumi uliimarika na hakuna taasisi ama mtu binafsi aliyeonyesha nia ya kuyatumia mabomba hayo. Hivyo project hii ilikufa yenyewe bila mkono wa mzungu.
   
Loading...