Kudai katiba mpya sasa hivi ni sawa na kuchenji buku kwa njaa ya usiku mmoja wakati haujui kesho yako itakuwaje?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wanabodi!

Nilikuwa nashauri kwamba kwa sasa tumpe nafasi mama akuze uchumi maana uchumi wetu kiukweli ulipo si pazuri ukilinganisha na huko nyuma tulipotoka kabla ya hili janga la uviko.

Taifa kama taifa linapitia katika kipindi kigumu sana, na hii katiba tunayolilia ni kama njaa ya usiku mmoja tujaribu kuvumilia tu tusichenji buku kwa njaa ya usiku mmoja, kukikucha panapo majaliwa ndio tuje na hoja ya kudai katiba mpya.

Nasikia mama ameomba repoti ya BOT huko ili ajiridhishe mzigo upo wa watoto wake kula mwaka mzima, maana kutokea na usambaaji wa kirusi hichi cha delta wimbi la tatu lolote linaweza kutokea japo hatuombei mabaya lakini ni vyema tukawa na akiba tusichenji buku kwa vitu ambavyo havina msingi kwa sasa.

Ningeshauri vijana tuachane na hoja ya katiba mpya kwa sasa, tujikite katika kumuombea na kumtia moyo mama yetu ili akuze uchumi siku 100 ni chache sana anaitaji mda zaidi kupanga mipango yake.

Hata hivyo katiba mpya ni matumizi mabaya tu ya pesa kwa sasa, kama katiba itaitaji kupelekwa bungeni haitokuwa ya wananchi maana hata hao wapinzani hawana muwakilishi zaidi ya wale 19 hivyo ambao ni minority.

Nashauri swala la katiba lingoje mpaka 2025 baada ya mama kuingia awamu ingine na wabunge wa upinzani kuwa wengi bungeni hapo tutapata katiba nzuri.

Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Wabunge wa upinzani wakawe wengi bungeni ndiyo kunahusianaje na katiba?

Rasimu ikishskamilika inatakiwavipigiwe kura na wananchi full stop.
 
Bilashaka Tanzania inawezakuwa ni nchi yenye binadamu wengi wenye IQ ndogo duniani.

Bilakupepesa macho.
 
Hata Chadema wangekuwa madarakani wasingeweza kuendeleza mchakato wa katiba mpya. Kikwete mwenyewe alipoona anamalizia uongozi wake ndiyo akawaachia warithi wake katiba pendekezwa.
katiba mpya italetwa na wananchi wa kawaida.....
 
Katiba haikwepeki, mwendazake kanyofolewa ili kuopsha mchakato huu... katiba huru ndiyo msingi wa uongozi wa haki katika jamii..huwezi kujenga uchumi ukiwa na katiba inayoegemea upande mmoja never.

Sasa tunangoja wa kuupinga mchakato huu ili apate nyundo ya Muumba
 
Back
Top Bottom