Kudai katiba mpya katika mazingira ya sasa ni sawa na kuihujumu katiba mpya

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,495
2,043
Mchakato wa kudai katiba mpya ni mchakato muhimu sana, ambao kwa maoni na mawazo yangu ni muhimu ufanyike kukiwa na elimu kubwa sana ya uraia miongoni mwa wananchi.

Kwa bahati mbaya wanasiasa wanatuaminisha kitu ambacho hakiwezekani. Kwa namna katiba inavyodaiwa sasa ni kana Kwamba litakaa chopo la watu wa chama fulani, Kisha wataunda katiba Kisha wataileta kwa wananchi.

Upo ugumu kupata aina ya katiba ambayo wengi tunaitamani, kwani michakato mingi ya upatikanaji wa katiba mpya bado inahodhiwa na chama tawala. Ikiwa ni pamoja na kupata wajumbe wa bunge la katiba, Tume ya kusimamia upigaji kura, na uelewa wa wananchi wengi kuhusu katiba mpya.

Ushauri wangu ni kwamba wadau wote wanaopigania katiba mpya wajielekeze kuibua vipengele vya katiba vinavyokwaza maisha ya wananchi ya Kila siku, na vikwazo hivyo viwe ni vile vinavyo watatiza watu wote bila kujali itikadi za vyama vyao.
 
Mwenzetu, je umeisoma rasimu ya mzee Warioba na katiba pendekezwa. Kama ni hivyo, wapi paboreshwe ili kukidhi matamanio yako.
 
Mwenzetu, je umeisoma rasimu ya mzee Warioba na katiba pendekezwa. Kama ni hivyo, wapi paboreshwe ili kukidhi matamanio yako.
Mimi nawashauri wapigania katiba maana wanakuja na vitu ambavyo havieleweki kirahisi Kwa raia ambao ndio wafanya maamuzi
 
Back
Top Bottom