Kudai Haki Siyo Uchochezi: CUF

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi- CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ikiwa kuwaambia watu wasimamie na kudai haki zao ni uchochezi basi ataendelea kuchochea mara kwa mara na yuko tayari kwa lolote.
Akihutubia mamia ya wafuasi wa CUF, wakazi wa Mji Mkongwe, Zanzibar katika viwanja vya Vuga jana, Maalim Seif alisema wananchi wa Pemba wenyewe walipoona kuwa Tume ya Uchaguzi haiwatendei haki katika zoezi la uandikishaji katika daftari la wapigakura ndipo walipoamua kusimama kidete na kusema kuwa kama watu wanaostahili kupewa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi hawapewi, basi hakuna atakayeandikishwa.
"Kama watu wakisimama kidete kudai haki zao ndio kuchochea, basi mimi nitachochea, chochea, chochea…," alisisitiza Maalim Seif.
Alisema kama SMZ wasipotoa haki za wananchi, litakalotokea lolote serikali itabeba lawama. "Haki za watu watazitoa kwenye tundu za pua zao."
"Wananchi wenyewe walisema kama hawapewi vitambulisho vya uzanzibari hakuna atakayeandikishwa kwa kuwa jambo hilo limeingizwa katika sheria za uchaguzi isivyo halali kwamba ikiwa huna kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, huna haki ya kuandikishwa kupiga kura. Hayo ni makosa kwani ni kinyume cha Katiba. Katiba inasema mwenye haki ya kupiga kura Zanzibar ni Mzanzibari, mwenye akili, aliyetimia umri wa miaka 18. Sasa inakuwaje mtu mwenye umri wa miaka 70 ambaye amezaliwa, amekulia, amezaa na amejukuu Zanzibar aambiwe kuwa kama hana cheti cha kuzaliwa hapewi kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na haandikishwi katika daftari la kupiga kura?" Alihoji Maalim Seif.
Maalim Seif alisema watu kutoka Tanzania Bara wanapewa vitambulisho vya Uzanzibari Ukaazi lakini Wahadimu wa Tumbatu, Wahindi Wazanzibari wa karne kwa karne hawapewi vitambulisho, je hapo haki iko wapi?
Akitoa takwimu za idadi ya watu walioandikishwa katika majimbo matatu ya kisiwani Pemba amesema Konde wameandikishwa watu 6,444 (4218 hawajaandikishwa), Mgogoni 6,278 (3,650 hawakuandikishwa), Micheweni 7,512 (3,144 hawajaandikishwa).
Naye Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa sheria haitambui uandikishaji wa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na suala hilo hata halimo katika katiba.
Alisema anayechochea watu ni yule anayevunja Katiba na Sheria lakini inashangaza kuona kwamba anayeilinda Katiba ndiye anayeitwa mchochezi.
"Kurugenzi ya Vitambulisho inasema kuwa wanaoona wamekoseshwa haki yao ya kupata vitambulisho waende mahakamani, kamwe CUF haitakwenda mahakamani kwani mahakama yetu ni wananchi," alisema Hamad........

SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
 
Mwishowe haki itashinda tu.
HAKI SAWA KWA WOTE.
 
Yaani Seifu mwisho kabisa ,huyu jamaa hana uswahiba na mtu haswa awepo kazini,ni tofauti kabisa na viongozi wengine tuliowazoea, nasema ameamua kufanya siasa kikamilifu na inavyoonekana hamwonei mtu haya wala aibu ,wala mbele yake hakuna kitu muheshimiwa wala ,mzee awepo kazini huwa anasema yale ambayo yanaonekana wazi kabisa ni makosa kiutendaji ,hivyo ikiwa anehusika ni mkuu wa nchi au mwenyekiti wa chama katibu kata au katibu mtungi wote atawaelezaa makosa yao kama ni ujinga atawaita wajinga na kama ni ya kipumbavu atawaita wapumbavu.

Na hesabu za kuwaita watu majina hayo anazo kiasi ya kwamba wanaoitwa hivyo nao wakijaribu kufanya mahesabu wanajikuta kweli wamo kundini.Tunahitaji viongozi aina ya Seifu ili kumkwamua na kumtoa MTanzania katika chaka la mafisadi.
 
Back
Top Bottom