Kudahiliwa vyuo vikuu tafadhali hudhuria maonesho ya tcu- kutakuwa na udahili hapo hapo

MKL

Senior Member
Mar 2, 2012
126
77
Maonesho ya saba ya vyuo vikuu yatafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 mwezi Aprili mwaka 2012 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga Dar es Salaam. Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Mohamed Gharib Bilali. Maonesho yatakuwa yanafunguliwa saa tatu kamili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili jioni kila siku.
Hakuna kiingilio kwa watakaotembelea maonesho haya........
mliomaliza form six na mnatafuta vyuo hii ni nafasi pekee kumaliza kila kitu ndani ya dakika chache sana mlemle Diamond Jubilee
kwa roho saafi tuu tafadhali gongeaneni habari hii kwa washikaji wooooote

ASANTENI: Habari hii haihitaji chanzo tafadhali Niepusheni na swali hilo tafadhali.....
siku njema............
 
una maana gani unaposema udahili utafanyika hapo? kwani si kama kawaida watatumia olas??? sijakuelewa hapo mkuu.
 
Ni hiviiiii TCU wanashughulikia udahili wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu tuu, kwa mfumo unaoitwa "CENTRAL ADMMISSION SYSTEM KIFUPI CAS" wewe unachanganya na maombi ya mikopo ambayo ni kazi ya bodi ya mikopo HESLB ambao nao watakuwepo kwenye maonesho hayo pia kwa hiyo maonesho haya ni ya TCU sio ya bodi ya mikopo ingawa bodi ya mikopo nao ni washiriki wa maonesho haya. sasa kama bodi ya mokopo nao wataamua kuruhusu waombaji wafanye maombi yao hapo hapo hilo sina uhakika kwakweli.

nadhani umenipata au kama vipoi rusha tena swali ni wapi hujakaa sawa




una maana gani unaposema udahili utafanyika hapo? kwani si kama kawaida watatumia olas??? sijakuelewa hapo mkuu.
 
watu wa equivalent wanaotaka kuunga degree wanaruhusiwa pia mkuu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom