Kuchukua mkopo benki na kujengea nyumba ni jambo jema lakini hasara yake ni kubwa

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Mikopo tunayokopa benki hapa nchini Tanzania zina riba kubwa sana kitu ambacho hufanya watanzania wengi kutofaidika sana na mikopo hiyo. Kwani kuna benki hutoza riba zenye faida ya asilimia 18%-23%.

Watanzania tulio wengi tukishachukua mikopo hiyo hukimbilia kuninua uwanja na kuanza kujenga nyumba, kisha huishi maisha ya shida sana kwa kipindi cha miaka minne mpk mitano. Wapo wengine hukimbilia kununua gari ili waonekane hapa mjini lakini hata uwanja hawana, mikopo hiyo ya benk ina mambo sana.

Wazo la kukimbilia kujenga nyumba kwa kutumia mkopo ni kujitengenezea maisha ya dhiki sana kwani makato huwa makubwa na kufanya kila siku kukimbizana na madeni yasiyoisha. Ushauri wangu na maoni yangu kama unataka kujenga au kununua gari ni bora ujiwekee mkakati binafsi unaweza amua kila mwezi kujiwekea kiasi fulani ambacho unatumia kwaajiri ya ujenzi, utafanya hivyo bila riba wala hasara yeyote.

Mikopo ya benki ni yakuwekeza katika biashara na ili ziongeze kipato na biashara hiyo irudishe mkopo huo yenyewe bila we kuathiri mapato ya kazi yako.

Kuweka pesa kila mwezi au kila sikunkutokana na maingizo yako inawezekana, kikubwa ni uamuzi thabiti na kujiwekea malengo na kuhakikisha unayafikia malengo yako.

Huu ni ushauri na maoni yangu jinsi ninavyoona namna ya kutumia mkopo wa benk kwa faida, lakini hata kama mtu akajenga nyumba ya biashara ni sahihi lakini nyumba ya kuishi ni safi sana lakini kuna hasara kubwa ndani yake.
 
Umesema vema sana,,,na ushahidi nauona kwa watu kadhaa wanaonizunguka.. Ila ni vzr kukopa ukazalisha kuliko kukopa ukajenge,,, mm hua nakopa tena sana tu ila sikop kama sina hela,nikitaka kununua kitu labda cha 5m. Nahakikisha hiyo hela ninayo,then naenda kukopa ile ile 5m,baadae nanunua nachotaka then ile hela niliyonayo naiweka kwenye mzunguko inalipa deni,,sijawah kujuta kutumia njia hii
 
Wazo lako zuri lakini ktk uhalisia wachache wanaweza,biashara pia ni risk taking kama kununua gari.
Yaani kwa mtumishi aliyebanwa na mazingira hayamruhusu kufanya biashara hamna jinsi,lazima akope ili awe na nyumba. Kuwa na nyumba kutamsaidia asipange au kupangisha hiyo nyumba apate kodi. Lasivyo atastaafuu bado amepanga kama hakujenga.
Mkopo mbaya ni wa gari ya kutembelea hatari,kama umekopa naamini hata kuilipia bima comprehasive na mikopo ya gari imewaingiza loss vijana sana maintanance si mchezo.
Nimeongelea hasa watumishi. Kutunza fedha nayo ni kipaji,maana fedha ni shetani ikiingia inataka kutoka.
 
Nilikuwa napanga Nyumba nalipa 400000 kwa mezi,nimokopa nikajenga Nyumba nanimehamia sina shida kabisa uache uongo we we,kukopa kunasaidia sana tu
Inategemea,,,na kaz yako au unachofanya,cz mfanyakaz anaelipa kodi laki nne unadhan analipwa bei gan? Sababu ukipiga hesaba mwaka unalipa ml 4.8 kwa kodi tu sasa huwez shindwa kulipa deni kutokana na kipato chako ndugu
 
Wewe kweli unakula panya. Usisifie uwozo kama chakula chako. Mikopo inayotolewa na hizi bank zetu ndio inaumiza sana kwa riba kuwa kubwa lkn upande mwengine huwapa nafuu watu wengi kwa kuwapatia makaazi mazuri na kuondosha usumbufu wa kuhamia kila mitaa.
Ni kweli panya nakula mkuu. Wengi hujenga nyumba kisha kuziuza wapate mitaji mifano ipo mingi. Mtoa post kaandika vizuri tena mwishoni kasema waweza jenga nyumba ya biashara ikawa ina zalisha ni vema. Sasa kosa ni lipi hapo.
Huo ni ushauri siyo sheria.
 
Kwa yeyote mzoefu, atapingana kwa kiasi flani na ajenda hii.
Mtu umefanya kazi yenye kukuingizia kipato cha wastani na unajiwekea malengo, lakini hakuna ulichoambulia, bado unaishi pangoni, what do you expect?
Pata hela ya mkupuo jenga, hamia.
Madeni yana msimu yataisha na utabaki na njengo wako.
Kukopa na kufanya biashara yahitaji uzoefu pia, hilo silishauri kwa kuwa sina uzoefu nalo.
 
Ni kweli panya nakula mkuu. Wengi hujenga nyumba kisha kuziuza wapate mitaji mifano ipo mingi. Mtoa post kaandika vizuri tena mwishoni kasema waweza jenga nyumba ya biashara ikawa ina zalisha ni vema. Sasa kosa ni lipi hapo.
Huo ni ushauri siyo sheria.
Naheshimu mawazo yenu sana. Lkn upande wa pili haukutendewa haki katika mawazo.

Kwenye suala la kuuza hujawahi sikia mtu kaanzisha biashara (company)na ikaenda viziri halafu ukaona biashara anaiuza.
 
Back
Top Bottom