"kuchoma kadi au bendera ndiyo kukomaa kwa demokrasia"

Matango

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
515
225
hapa naomba wachambuzi wa siasa wanisaidie.
Mwanachama wa chama fulani anahama chama. Akienda chama kingine sherehe ni kuchoma kadi.

Mimi sio mwanasiasa lakini nikifikiri naona sherehe ingekuwa kwenda kuonana na viongozi wa chama kingine na kuwakabidhi, au kuweka kwenye ofisi kama maonyesho.

Wengine wanachoma hata bendera. Kumbuka kuna siku mwanachama yule yule atataka kurudi chama cha zamani. Je wenzetu huko nje wenye siasa za vyama vingi hufanya hivyo ?
 

alfazulu

JF-Expert Member
May 6, 2012
734
0
hakuna asiye mwanasiasa...hoja ni upo ktk level ipi ya uanasiasa. unapojadili hoja yoyote ya kitaifa au itikadi mfano mfumo wa afya, elimu, technology, miundo mbinu etc tayari umeshaingia ktk siasa kwani wellfare ya nchi hutokana na mwelekeo siasa ya nchi yenyewe, hvyo yategemea tu iwapo ni siasa bora au bora siasa. Back 2 ur topic...hv umesahau enzi zile wanafunzi wakihitimu dar 7 au form 4 walivyokuwa wakifanya fujo mashuleni, piga walimu piga wanafunzi, andika matusi ktk kuta na mbao madarasani, choma majengo ya shule....sasa ile haikukemewa ikaacha ikakomaa...ndo yakatokea yale ya mwanza mtu kushndwa ubunge akaondoa furniture hadi vitasa vya ofisi ya mbunge akaondoka navyo...hiyo ndiyo hali halis...tumewekeza ktk ushabiki kuliko ktk siasa bora. nasasa tunawekeza ktk kujengea watznia hisia za ukabila/udini na ukanda...tutapata majibu yake with time...tafakari chukua hatua. siasa hatakama twapingana mwsho wasiku tuangalie nchi...vyama ni nini bana?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom