G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,614
- 8,615
Heshima kwenu ndugu jamaa na marafiki,natumai MUNGU ni mwema kwetu kwa afya anayotupa na chakula cha kila siku.niko na hoja moja natamani kusikia pia kutoka kwenu..hivi ni kitu gani kinafanya mtu achoke kua mahala fulani pa kazi kiutafutaji na anatamani kwenda mahala pengine?nimekua nikisikia watu wengi wakisema Ah ofisi hii nimeshachoka bola nijiendee zangu ofisi fulani au ngoja nijiende zangu mtaani,nafikili mnanielewa kile nasema,binafsi hali hii imenitokea mala mbili sasa.mwaka 2003 nilikua nikifanya kazi mahala fulani kwa mtu kwa miaka sita,ikatokea tu ghafla nikachoka kuendelea kufanya kazi mahala hapo na nikaanza kutafuta kazi mahala pengine mpaka nikapata tena katika shirika fulani kubwa tu hapa nchini lisilo la kiserikali,hapa napo nimekaa nikifanya kazi toka mwaka 2009.kiukweli mahala hapa pamenifanya kupiga hatua ya maisha kwa kiwango fulani na siyo pabaya sana,tatizo tena limekuja ndani ya nafsi yangu naona kama nimechoka tena kua hapo na sasa natamani kuingia mtaani kufanya mambo yangu,lakini pamoja na kuwaza hayo sioni ntaanzia wapi coz kwa muda mwingi nikiwa ofc hii nimetumia pesa niliyokua naipata kwa kujenga nyumba ya makazi maana niko na familia,hivyo basi ukiondoa kua na nyumba kwa sasa na gari dogo la nyumbani sioni kitu kingine cha kunipa pesa zaidi ya akiba ya NSSF iliyo kama ten milion kwa sasa.lakini mpaka najikuta naandika hapa kiukweli moyo wangu unaniambia ondoka hapo nenda mahala pengine,nakua najiuliza what next na je hali hii huwatokea hata ninyi mnaosoma habari yangu hii?na kama ndiyo mmekua mkifikili nini juu ya kukabiliana na hali ya uchovu katika eneo moja la kazi,niseme ndiyo MUNGU ananiambia nenda huko kuna mafanikio au ni pepo mchafu anataka kunipoteza?mchango wenu wakuu kulingana na changamoto hii.Aksante