Kuchinja kuku wa kienyeji: kisu kisinolewe/kinolewe?...na kinolewe wakati gani?

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
Wapendwa kama mjuavyo, hatimaye majuzi nilimkamata yule kuku niliyekuwa nikimkimbiza kwa ajili ya kumfanya kitoweo na sasa yuko mikononi mwangu hapa. kuku mwenyewe nikimgeuza huku na huko namwona kanona kila idara. Lakini ishu iko kwenye kisu cha kuchinjia!

hiki kisu changu ni butu kwani huko nyuma kimechinja kuku wengi sana hivyo kinahitaji kunolewa kwa ajili ya huyu kuku kwani naona amenona sana. Sasa ninatatizwa na kitu kimoja hapa:

1. Ninoe kisu nikiwa nimemshikilia?au ataniponyoka na kukimbia tena? manake namwona bado ana nguvu za kukimbia.......
2. Nitafute kwanza kamba nimfunge ndo nikanoe kisu? Si nitachelewa kula jamani na njaa yote hii na kuku mwenyewe kanona hivi?
3. Nimchinje hivyohiivyo na kisu butu? Si nitamuumiza jamani na kumuongezea mateso tu kwa kumcheleweshea .......? watetezi wa haki za wanyama wataniacha kweli?

Sasa naomba ushauri wenu bandugu, nifanyeje?
 
Kuna wataalamu wapo tayari kuchinja 24/7. Ukiendelea kupoteza muda na kujingata ngata, utapata kuku kashachinjwa akiwa bado mikononi mwako. utabadi kula tu
 
Baba Chinja fasta kuna watu wana visu washanoa wanatembea navyo, tena vinakata pande zote mbili ohooooo
 
Wapendwa kama mjuavyo, hatimaye majuzi nilimkamata yule kuku niliyekuwa nikimkimbiza kwa ajili ya kumfanya kitoweo na sasa yuko mikononi mwangu hapa. kuku mwenyewe nikimgeuza huku na huko namwona kanona kila idara. Lakini ishu iko kwenye kisu cha kuchinjia!

hiki kisu changu ni butu kwani huko nyuma kimechinja kuku wengi sana hivyo kinahitaji kunolewa kwa ajili ya huyu kuku kwani naona amenona sana. Sasa ninatatizwa na kitu kimoja hapa:

1. Ninoe kisu nikiwa nimemshikilia?au ataniponyoka na kukimbia tena? manake namwona bado ana nguvu za kukimbia.......
2. Nitafute kwanza kamba nimfunge ndo nikanoe kisu? Si nitachelewa kula jamani na njaa yote hii na kuku mwenyewe kanona hivi?
3. Nimchinje hivyohiivyo na kisu butu? Si nitamuumiza jamani na kumuongezea mateso tu kwa kumcheleweshea .......? watetezi wa haki za wanyama wataniacha kweli?

Sasa naomba ushauri wenu bandugu, nifanyeje?

Weee! usijaribu kwani ukianza kukinoa na yale makali yakianza kuonekana
ni lazima atafuta upenyo wa kukimbia na hutomkamaata teena.
 
shika kisu chako kule kwenye ncha yake, fanana kama unakivuta toka kwenye ala yake, chinja hivyo hivyo ila angalia maana chaweza kuwa na kutu halafu ukasababisha tetenasi bure.
 
Lakini huyu kuku mwenyewe si yuko hapa ndani au ?? ..teteteteh..mfunge kamba tayari kwa kunoa kisu ukimaliza kunoa kisu endelea kwa raha zako ...ukitumia kisu butu AK shauri yako ..
 
Hapo akili kichwani mwako, lakini kumbuka, mambo kama, Kibudu,mwenye pupa hadiriki kula tamu.Thamini haki na uhai wa wengine,usichotaka kutendewa usimtendee mwingine.Hayo yakuongoze katika uamuzi wako,aidha awepo humu au kwenye banda la kuku.
 
Kiongozi, funga kamba kwa maneno mazuri ukavae salama Kondom upate kuchinja vizuri kuku asiumie na wala wewe usiumie
 
AK-47 kunani shem?? lete nikushikie ukimaliza kunoa kisu ntakupa kuku wako......
 
Huyu ni KUKU gani wajameni?
Mbona nahisi hili ni fumbo mezani
Kwanini mikononi na sio zizini?
Swali nauliza huyu KUKU gani?

Kidosho au mtetea?
Kimwana au jogoo?
Wa kisasa au kienyeji?
Swali nauliza huyu KUKU gani?

Mate yanakutoka au yanamwagika?
Kama kula peremende au kisusio?
Mikono umenawa, mezani umekaa
Swali nauliza huyu KUKU gani?
 
mmmmh kazi hipo leo,mkamateni huyo kuku achinjwe nyama tule wote,kwann akuponyoke?noa kisu kwanza then mkamate,si unajua mkulima hawezi kwenda shamba bila jembe?
 
mmmmh kazi hipo leo,mkamateni huyo kuku achinjwe nyama tule wote,kwann akuponyoke?noa kisu kwanza then mkamate,si unajua mkulima hawezi kwenda shamba bila jembe?
Mimi nilivyoelewa kuku ndio wewe LULU.au unataka kujila mwenyewe?
 
Duu hongera mkuu kwa kumkamata kuku wako..Unasema kisu chako ni butu kwa kuwa kilichinja kuku wengi huko nyuma,mimi nadhani kwa sasa kisu ndio kikali zaidi kwa kuwa kimechinja kuku wengi,umemsahau Darwin na law of use nad disuse?
 
Sauri yako we leta zako hizo za kutaka kunoa kisu, atakuponyoka. Na akikukimbia ndio humkamati tena, chinja faster na hicho kisu chako butu.
 
Huyu ni KUKU gani wajameni?
Mbona nahisi hili ni fumbo mezani
Kwanini mikononi na sio zizini?
Swali nauliza huyu KUKU gani?

Kidosho au mtetea?
Kimwana au jogoo?
Wa kisasa au kienyeji?
Swali nauliza huyu KUKU gani?

Mate yanakutoka au yanamwagika?
Kama kula peremende au kisusio?
Mikono umenawa, mezani umekaa
Swali nauliza huyu KUKU gani?

Hili hapa sio fumbo bali lugha ya mtaani
anazungumzia matumbo, usilichukulie maanani
ni kuku mwenye umbo, haenei kwenye sahani
nakujibu swali, huyu ni kuku mwenye umbo

kidosho wala mtetea, sio jibu la kutoa
usije ukamendea, mtama ukautoa
sio uchoyo natetea, hapa tushakutoa
nakujibu swali, huyu ni kuku mwenye umbo

mate yasikotoke, na tafadhali usiyamwage
kwenye mada hii utoke, nakuomba utuage
nenda kaokoke tuachie tumukarange
nakujibu swali, huyu ni kuku mwenye umbo
 
Mimi nilivyoelewa kuku ndio wewe LULU.au unataka kujila mwenyewe?

Jibu laanza kutoka ingawa kwa machale
Je a ni kweli LULU ndie KUKU?
Charity KUKU kujila mwenye?
Au LULU kujila mwenyewe?
Swali adimu kwenye kinza cha ndimu
 
Back
Top Bottom