Kuchimba Dawa Safarini!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuchimba Dawa Safarini!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Katavi, Nov 30, 2010.

 1. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini havijengwi vituo maalumu vyenye hadhi kwa ajili ya "kuchimba dawa" tunapokuwa safarini? Hawa wenye magari wameanzisha vituo rasmi kwa ajili ya kazi hiyo lakini vina upungufu kwa sababu ni porini na watu hawajisitiri vizuri, taabu inakuwa zaidi kwa akina dada na akina mama. Njia nyingine ndio kabisa mapori yenyewe wanaposimama kuna tishio la wanyama wakali kama simba na wengine. Bora njia nyingine angalau kuna ustaarabu wanasimama mahali kuliko na hoteli............
  Hili kwa kweli wahusika inabidi walitazame........:angry::angry:
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  yaaaaaahaaaaaaaaaaaaaaa ni kweli hilo neno maaana kuna siku nilikua naenda moro na abood likasimama sehemu ambayo hakuna kichaka kabisa halafu watu wachimbe dawa ilikua shida sana kwa akina dada na mama.
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Uchafuzi mkubwa wa mazingira for a proof notice maeneo haya mawili kama mfano, ukitoka morogoro kama waenda nyanda za juu kusini baada ya kutoka njia panda ya Mzumbe, kuna sehemu pale mpaka nyasi zimekauka iwe majira ya mvua au kiangazi. Pananuka si mchezo. Pia eneo moja kabla ya kuingia makambako, ukitoka mbeya, mnapoiacha makambazo kwa ku-drive after not more than ten minutes, hata kama mabasi kumi yamefuatana, lazima yote yatasimama eneo lile ili watu wachime dawa (wachafue mazingira) - funny thing is, they are also business centers, utakuta jamaa wanauza mahindi ya kuchoma, ndizi, sambusa etc
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kumbe kuna uchafuzi wa mazingira pia!...................kwa kweli hili ni tatizo kubwa linatakiwa litafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Sasa funga kazi hayo maeneo ya kuchimba dawa unakuta kuna watu wanauza nyama choma na vitafunio vinginevyo! Na abiria wanajinunulia kama kawa!!!
   
 6. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Inatisha lakini tutafanyaje. Inabidi wenye mabasi walazimishwe kujenga sehemu za watu kupumzikia wakiwa safarini. Inawezekana
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hii ni hali ya kushangaza sana, mabasi yote hulazimishwa kuingia stendi hata kama hakuna abiria anayeshuka na kupanda, mbaya zaidi standi kama ya Makambako haina vyoo vya kutosha kuhudumia mamia ya wasafiri wanaolazimishwa kuingia ndani ya standi hiyo. Jambo la kushangaza basi likiondoka standi kuelekea Iringa baada ya dakika 10 basi husimamishwa porini na abiria kutakiwa kwenda kuchimba dawa, eneo hilohilo biashara za vyakula mbalimbali huuzwa eneo hilohilo bila ya kujali afya za abiria.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hili ndilo linatakiwa lifanyike.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni advanture ,na kuna siku jamaa walimtukana dereva kwa kusimamish basi kwenye uwanja
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Pale eneo la makambako kuna choo cha kulipia lakini bado utakuta dereva anasimama eneo lisilo na choo na kuruhusu watu kuchimba dawa.

  Wanahitaji kupigwa fine woooooote wanochimba dawa porini. Na dereva apigwe fine kwa kila abiria aliyeshuka kuchimba dawa.
   
 11. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  sasa yakikushika ya kukushika utashika wapi?
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280

  mkuu hilo dili la konda na dreva wanakula chabo!!!!
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  njia ya kuja Yaeda kidogo tuna bahati, kuna vyoo sehemu mbalimbali tena maji na toilet paper vinapatikana....kwa wale waliowahi kutembelea huku wanaweza kuthibitisha hilo, kati ya makuyuni na mto wa mbu kuna vyoo, mto wa mbu na kibaoni manyara kuna vyoo.........na kuendelea.......raaaaaaaahaaaa mustarehe....tena ukitoka ****** unasogea pembeni kidogo unapiga picha mandhari ya eneo na kupata upepo mwanana.....swaaaaafi
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Inabidi tushauri iundwe timu ya wataalamu waje wajifunze huko ili sehemu zote za nchi hii ziwe na vyoo vyenye hadhi kama huko.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Nov 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Du!
   
 16. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  karibuni sana.....tutawafundisha wao waje tu
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wiki mbili zilizopita ITV walionyesha katika kipindi chao cha Ripoti Maalumu namna abiria wa Mbeya-Dar wanavyochimba dawa njiani........dah ilikuwa ni aibu!!!
   
Loading...