Kuchelewa kwa vitabu vya mtaala mpya, Mh Rais na Prof. Ndalichako wanalijua hili?

Chapota

Member
Oct 25, 2017
98
225
Mpaka sasa walimu wanafundisha kwa kutumia vitabu vya zamani katika mtaala mpya. Sijajua kama hili ndalichako analijua au ameamua kukaa kimya wakati wahanga wa mtaala huu wanafundishwa kwa vitabu vya zamani.

Pia sijajua kama daktari wa majipu anafahamu kwamba kwenye mpango wa vitabu vipya kuna jipu limeiva linahitaji daktari. Lakini pia sijafahamu kama mwenye nchi amekataza michango wakati watoto wake hawana vitabu vya mtaala mpya hasa wanafunzi wa darasa la nne.

Kama ndivyo wale wanaomjuza mzee wa kuzuia michango wamjuze na hili la vitabu vya darasa la nne. Ningekuwa na uwezo wa kuonana naye ningemwambia afanye mpango wa dharura vitabu vipatikane haraka sana.

Wanajf tusaidiane kumjuza huyu mzee watoto wanapata shida ya kusoma hakuna hata kitabu kimoja kipya kwa darasa la nne.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom