Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,767
Nionavyo hili limekuwa tatizo kwa Wizara inayohusika. Wanachelewa kutoa majina ya Shule na Vyuo wanakowapeleka wanafunzi wa Kidato cha Nne. Kuchelewa huku husababisha adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi hasa inapotokea watoto wao wamepelekwa katika shule au Vyuo vya mbali ukizingatia gharama za nauli, ada na matumizi.
Chukulia mfano wa Mwanafunzi anayetoka Kyaka kule Kagera, mpakani mwa Uganda na kupelekwa Mtwara, kusini, mpakani mwa Msumbiji, atahitaji gharama kubwa sana.
Kwa hali hiyo Wahusika wa Wizara wanaposubiri Hadi wiki za mwisho za mwezi wa sita ndipo watangaze shule na Vyuo, inakuwa si sawa. Ikumbukwe kuwa matokeo ya wanafunzi hawa yalitoka mwezi wa tatu, hivyo sioni sababu za msingi za uchelewevu huu wa makusudi.
Mhe. Waziri najua anapita humu, ni wajibu wake kuwahimiza wapanga shule na Vyuo watangaze mapema ili wazazi watayarishe gharama zinazotakiwa. Kujifungia Dar es Salaam na kufikiri wanafunzi wote watatoka Mbagala na kwenda Mikocheni si sahihi hata kidogo.