Kuchelewa kutangaza baraza la mawaziri nin maana yake?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Mimi naona huyu Mkwere aliomba dhamani bila kujiandaa, hakupanga nani atakuwa waziri Mkuu, nani atashika wizara fulani, n.k.
Nilidhani amejifunza kwa miaka mitano akiwa madarakani na nilitegemea safari hii, kila kitu kingekuwa kiko straight forward lakini mambo yanavyoonekana yatakuwa ni yaleyale, sitashangaa kama akija na baraza linalozidi 40 kama ambavyo Mwananchi na magazeti mengine yametabiri, tutegemee kuanzia 45 na kuendelea
 
.... ongeza basi na hizi...., MKE (namba X), Mke (namba Y), Mtoto (namba y), Mamkwe (mama wa Y),.... ,Nyumba ndogo (z, z+1,..., z+i,..., z+n), ongeza hapa
 
Nimemuuliza mtu mmoja aliye karibu na Ikulu, kaniambia sababu ya kuchelewa ni kuwa baraza la mawaziri litakuwa na sura nyingi mpya -- karibu 20 -- hivyo basi zoezi la vetting linalofanywa na usalama wa taifa (Tanzania Intelligence and Security Services) limekuwa refu.
Kwa kawaida, TISS huambiwa kuandaa faili za mawaziri watarajiwa zinazokuwa na details zao za undani ili kumsaidia Rais afanye uteuzi. Kwa vile Rais amesisitiza kuwa anataka mawaziri WAADILIFU, kazi ya vetting inayofanywa na TISS imekuwa na umuhimu wa pekee safari hii.

Mimi binafsi nadhani kuchelewa kutangazwa kwa cabinet ni hulka tu ya Rais wetu Mkwere. Huwa anasifika kwa tabia yake ya kuchelewa kufanya maamuzi magumu, kuchelewa appointments, etc. Zakia Meghji aliyempa ubunge juzi na kuandaa kumpa uwaziri ana uadilifu gani? Sote tunajua madudu aliyofanya akiwa waziri wa maliasili na utalii (Sheni wa Kigoma Hilltop na wengine walifanya ufisadi kwenye vitalu vya uwindaji). Akiwa waziri wa fedha alishindwa kushuhulikia sakata la EPA na kuishia kukiri kuwa alidanganywa na Gavana Ballali kuhusu malipo ya Kagoda. Lowassa wa Richmond naye anayefikiria kumrejesha?

Nasikia Kikwete kesho alitaka kwenda Libya sasa haendi tena. Badala yake yuko pamoja na Waziri Mkuu Pinda wakijadiliana kuhusu hao mawaziri WAADILIFU.

Hii ngoma imelala mpaka Jumatano!
 
Unawezaje kutegemea viongozi waadilifu wateuliwe na mtu ambaye hajui hata kufikiria kwa kutumia uwezo wake. Wapo wanasiasa wengi wanaomuongoza na bahati mbaya hata hao wana marafiki rudo wanaowinda kuingia kwenye udokoaji. Bunge la ccm nalo ndo hivyo tena.Hawapimi uwezo na ubora wa mwenyekiti wao na ndo maana wanampigia makofi kwa kila sentensi aliyosoma ktk hotuba. Hapo atajuaje kwamba anatakiwa arekebishe mambo?

Tutegemee uzembe wa kupita kipimo baraza lijalo.
 
Binafsi kuchelewa kutangaza Cabinet kwangu inanipa picha kwamba huyu Jamaa alikuwa hajijipanga,hana vision yoyote na kwaujumla hajui anataka kuifanyia nini Tanzania kama ambavyo alivyowahi kukiri hajui sababu za Tanzania kuwa masikini.Kikubwa anachokifanya saiv katika Ubongo wake nikuchakachua akili kuhakikisha Kwamba anatengeneza nafasi zakutosha kwa Watu wake ili waitafune nchi vizuri.
WATANZANIA TUFUNGE MKWIJI NA TUTEGEMEE MSOTO WAKUFA MTU KTK HII MIAKA MITANO NAAMINI ITAKUWA KAMA 100KUTOKANA NA UGUMU WAKE,IF WE SHALL PASS SAFE IS THE MATTER OF WAIT AND SEE BT WE MUST KEEP ON PRAYING.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Labda kwa mara kwanza anafuata ushauri na protocol zinavyotaka......awaache TISS ifanye kazi yake uswahiba pembeni this time
 
Jamani kwani tunaposema kuchelewa kutangaza tunamaanisha nini?
Kuchelewa from people's expectations? Au kwa mujibu wa katiba amechelewa?
Au kuchelewa kupi?
Katiba inasemaje kuhusu muda wa kutangazwa baraza?
 
Hivi JK wakati anahangaika na Tume yake kuchakachua kura za urais hakujipanga kuunda baraza la mawaziri? Kinachomfanya mpaka saa hizi hajaunda baraza ni kwamba hao mawaziri anawaumba? Kama ni kuwateua wale wapendwa wake tayari amewataja wa tatu na kama alitaka kuwataja wote ruksa. Au ameandaa mtihani wa kuwapatia wale anaowafikiria kuwa wanafaa hivyo anahitaji muda wa kusahisha pengine wengine wanarudia mtihani?

Ni shida gani anayopata katika kutafuta wale wa kupewa nafasi? mbona hawakuwa na shida kumpata spika? au anasubiri kesi ya Chenge itaendaje kule Uingereza? Asiwe na hofu, wabunge wa Chadema hawatapinga uamuzi wake na wala Watanzania asiwe na hofu nao maana ni wasahaulifu(lakini siku hizi wameanza kutunza kumbukumbu).

JK tunasubira baraza la mawaziri. Tupatie hata yule anayekushinikiza kwamba umpatie uwaziri katika ile wazara nyeti. Mambo ya uchaguzi yamepita usiwe na hofu kabisa tatizo limebakia kwenye Katiba. Umetangazwa na Tume wewe endelea na majukumu yako utupatie baraza. Usiwe na hofu tumeshatulia wewe huna tatizo wala Tume haipaswi kuwa na lawama kwa sababu hata kama ingekosea ikamtaja yeyote kuwa ameshinda hata ikikosea namna gani hakuna kosa katika utangazaji wa mshindi. NEC ndiyo mwisho wa kila kitu sisi wananchi tunajipanga bure kwenye foleni lakini Tume ndiye mwamuzi wa kura zetu.

Wewe tupatie tu Baraza la mawaziri. Tunaomba uwapeleke kwenye kozi ile ya Ngurudoto kama kawaida wapate maelekezo. Kadiri utakavyochelewa kulichagua baraza ndivyo watakavyochelewa kuwahi huko kwenye kozi.
 
Jamani ukiwa Mwizi ni lazima uzibe nyufa za ushahidi, hivi anasubiri baraka kutoka kwa mnajimu wake.
 
Rostam amechelewa kumpelekea majina mkuu wa kaya.

Kweli umenena, Rostam Aziz ndiye de facto president wa Tanzania. Yeye ndiye alimuweka Kikwete madarakani 2005. Yeye alisema atamtoa Sitta kama spika akafanikiwa. Yeye ndiye anayechagua mawaziri (Ngeleja. etc) na wabunge wa kuteuliwa na Rais (Jussa). Na yeye pia anachagua makatibu wakuu na wakuu wa taasisi nyeti za serikali kama Tanesco, Tanroads, etc. Hakika corruption Tanzania imefikia kwenye stage ya juu ya state capture kama NGOs zilivyowahi kusema.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!
 
KATUNI(323).jpg
attachment.php
 
atakuwa anaomba writting pad nyingine sasa, maana zile tatu za mwanzo zilichafuka saana, hivyo sasa hivi ndio anasubiri writing pad fresh a copy from those 3 drafts. sasa tatizo asije aka-copy vibaya, itabidi zoezi lianze upya.
 
Huu uchelewaji wa kutangazwa kwa baraza la mawaziri una maana gani? Kwanza hakuna kipya zaidi ya walewale wana mtandao ambao tumewazoea sasa kwanini mh. JK anachukua muda kulitangaza?
 
JK hajiamini hata kidogo, ndio sababu hakuna hata siku maalumu iliyotangazwa kuwa atatangaza baraza lake na hii ni wasiwasi juu ya timu yake ya maswahiba na ma shemeji juu ya wananchi watasema nini.
 
Hata ingekua wewe pale Magogoni bila ridhaa ya watu usingeweza kuogopa na kudondoka dondoka mara kibao kwa hofu ya kuiba cha watu na mipresha kupanda???

Huoni Bilal katumwa huku, Makamba kule na wengine wengi tu nchi za watu lakini serikali hizo zikawajibu kwamba tuwasaidie vipi wakati nchini kwenu mpaka sasa HAKUNA VITA??? Kumbu wasijue vita ya Mtanzania ya bila Vurugu, bila risasi ndio mbayo kuliko yote duniani!!!

JK Taifa linamtega ile mbaya, ngo kudondoke hata kimsumari uone...
 
Kimsingi mimi Rais wangu ni Dr. W.P. Slaa, mtu ambaye ni mzalendo mwenye kujali wanyonge, mpenda haki, na anipenda hii nchi na watu wake kwa dhati.

Tumuunge mkono na wabunge wake 48 aliowapata, maana huyu JK hana mpango na mtanzania wa kawaida kwake issue ya msingi ni kutetea ufisadi.
 
Back
Top Bottom