Kuchelewa kutangaza baraza la mawaziri nin maana yake?

Kuna jipya wala tusijidanganye, jamaa atateua mafisadi mpaka mbaki midomo wazi. wale ambao hukutamani waingie watakuwemo.sasa hilo si ndo litakuwa jipya? Kumbuka hii ndo lala salama ya jamaa wa mitandao....fadhila lazima ziendelee.......CCM hawana haya wewe!

Tatizo lenu ni kudhani nanyi mtateuliwa, sasa kimya kingi kinawanyima usingizi. Tulieni, kwani mna ubia na urais ???? Nawauliza, kazi ya urais ina ubia na mtu???? Fanyeni kazi zenu mwacheni na yeye afanye kazi yake. Tatizo siku hizi kila mtu mwanasiasa.
 
Mimi naona huyu Mkwere aliomba dhamani bila kujiandaa, hakupanga nani atakuwa waziri Mkuu, nani atashika wizara fulani, n.k.
Nilidhani amejifunza kwa miaka mitano akiwa madarakani na nilitegemea safari hii, kila kitu kingekuwa kiko straight forward lakini mambo yanavyoonekana yatakuwa ni yaleyale, sitashangaa kama akija na baraza linalozidi 40 kama ambavyo Mwananchi na magazeti mengine yametabiri, tutegemee kuanzia 45 na kuendelea

Looh, Wa-TZ kwa uzushi siwawezi, nani kakwambia hayo unayotuletea hapa???? Mara ooooh katiba inasemaje, KASOME..
 
Back
Top Bottom