Ushamtia mimba mtoto wa watu,jiandae kulea au kwenda gerezani!! Pole sana,ndo maisha lakiniWakuu Salaam!
Hapa home kuna issue tata kidogo! Kuna msichana ana umri wa miaka 18 na anakaribia miaka 19 hivi sasa! Ukimuona ana afya njema na haoneshi dalili yoyote ya upungufu wa kitu fulani mwilini! Sio tu kwamba anaonekana ana afya njema lakini amekuwa vizuri kwa sababu, usipomwangalia usoni na kugundua uso wake wa kitoto, unaweza kuamini amefikisha hata miaka 23 kwa jinsi alivyoenda hewani na mwili uliojengeka vema!!
Pamoja na yote hayo, huyu binti hadi sasa hajaanza kuingia hedhi!!
Ninachoomba kufahamu ni:
1. Je, hii inaweza kuwa ni hali ya kawaida pamoja na umri wote huo?
2. Kama si hali ya kawaida, hii hali inatokana na nini na tiba yake ni nini?!
Natanguliza shukrani zangu kwenu!