#COVID19 Kuchanja sasa kuwe lazima, hasa wafanyakazi serikalini. Chanja au achia ngazi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,314
24,177
Sasa inabidi Serikali ichukue uamuzi mgumu juu ya chanjo.

Wafanyakazi Serikalini lazima wachanje, au waachie ngazi kutazama afya zao.

Tutavaa barakoa hadi lini?

Tatizo kubwa ni hao wa Gwajima, wasiotaka kuchanja na ndio kwa kiasi kikubwa wanaeneza Covid katika jamii.

Ni jambo la kusikitisha vifo vya hivi karibuni familia ya Hanspoppe, kuna waliokataa kuchanja, mauti imewatembelea.

Imefika muda tusicheze na hili janga.

YANAYOJIRI
In just three weeks, six unvaccinated members of a Florida family died after contracting COVID-19.

After attending the funeral for 48-year-old family member Tyrone Moreland, 89-year-old grandmother Lillie Mae Dukes Moreland was hospitalized with the virus and died just 24 hours later, according to The Palm Beach Post.

Three more cousins died shortly after their grandmother, and the family's most recent loss was 44-year-old Trentarian Moreland, who died on Sunday.

UPDATE
Sasa kuchanja ni lazima kwa wafanya kazi serikalini.
 
We Chidu La acha unafiki asee, unataka kuaminisha hans amepigwa na Covid tuwe na hisia za hofu basi, hii tabia ya watu maarufu wakifariki mnasingizia corona, mbaya zaidi hampingi hiyo mikusanyiko kwa hao waliofariki kwa Covid.

😨UNAFIKI!
 
Sasa inabidi serikali ichukue uamuzi mgumu juu ya chanjo.
Wafanyakazi serikalini LAZIMA wachanje, au waachie ngazi kutazama afya zao.
Tutavaa barakoa hadi lini?
Wewe kuwa mkweli tu kwamba maisha mtaani yamekuwa magumu ikakupelekea kudhani watu wakifukuzwa serikalini utaajiriwa.

Kwa taarifa ni kwamba sio waajiriwa wa serikalini tu ndo hawajachanjwa,wapo watu wanauza mchicha hawajachanja, je hutanunua mchicha wao kisa hawajachanjwa?

Na ili uajiriwe ni lazima uwe na vigezo, hutaajiriwa kisa umechanjwa na kuna watu wamefukuzwa sababu ya kutochanjwa na wewe uliyechanjwa hata kama huna vigezo uajiriwe tu.
 
Uko sahihi
Nafikiri ana ajenda ya ajira
Ila amejificha kwenye chanjo
 
Sasa inabidi Serikali ichukue uamuzi mgumu juu ya chanjo.
Wafanyakazi Serikalini lazima wachanje, au waachie ngazi kutazama afya zao.
Tutavaa barakoa hadi lini?

Tatizo kubwa ni hao wa Gwajima, wasiotaka kuchanja na ndio kwa kiasi kikubwa wanaeneza Covid katika jamii.

Ni jambo la kusikitisha vifo vya hivi karibuni familia ya Hanspoppe, kuna waliokataa kuchanja, mauti imewatembelea.

Imefika muda tusicheze na hili janga.
Wafanyakazi ni asilimia chache sana ya watz!!! Kwann wafanyakazi wachanjwe kwa lazima?? Acha bangi mzee..... Kwaiyo wafanyakazi ndo wanakufanya uvae barakoa? Usivae barakoa
 
Sasa inabidi Serikali ichukue uamuzi mgumu juu ya chanjo.
Wafanyakazi Serikalini lazima wachanje, au waachie ngazi kutazama afya zao.
Tutavaa barakoa hadi lini?

Tatizo kubwa ni hao wa Gwajima, wasiotaka kuchanja na ndio kwa kiasi kikubwa wanaeneza Covid katika jamii.

Ni jambo la kusikitisha vifo vya hivi karibuni familia ya Hanspoppe, kuna waliokataa kuchanja, mauti imewatembelea.

Imefika muda tusicheze na hili janga.
Why watumishi wa umma pekee?

kwani Daladala si tunapanda wote?
 
Uko sahihi
Nafikiri ana ajenda ya ajira
Ila amejificha kwenye chanjo
Pia kuna waliochanjwa wengi wana hofu hawajui nini kitawapata hapo baadae, wanataka kushinikiza wote wachanjwe ili kama kuna madhara yasiwapate peke yao, hii ni roho mbaya na ya kichawi.

Ikumbukwe hii chanjo siyo ya kwanza zipo zizilizotangulia, Kwenye zilizotangulia, ukishampa taarifa jirani yako basi
unaendelea na maisha suala la ataenda kuchanjwa au la hatufuatilii, jiulize hii mbona wakishachanjwa wanataka na wewe uende hata kama ni kwa lazima?
 
Back
Top Bottom