Kuchangia mamilioni kwenye harusi wakati watoto wetu wanakaa chini bila madawati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuchangia mamilioni kwenye harusi wakati watoto wetu wanakaa chini bila madawati

Discussion in 'Jamii Photos' started by MTUMISHI WA WATU, May 9, 2012.

 1. M

  MTUMISHI WA WATU New Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naleta kwenu wana jamii, tusaidiane, kila siku, kila mwezi, tunachangia harusi, na nikirudi nyumbani mtoto kachafua nguo, kisa wanakaa chini, na michango ya harusi niliyochangia kwa mwezi naweza kutenegeneza dawati moja la mtoto wangu.kwa nini watanzania tusibadilike, ili na watoto wetu wafaidi pesa zetu badala ya kuzipeleka kwenye harusi na kuteketezwa kwa masaa machache tu!!!
   
 2. K

  Kaseisi Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anza wewe kubadirika, goma kutoa michango ya harusi
   
 3. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Nani kakulazimisha kuchangia harusi? wenzio tuliacha siku nyiiiiiiiiingiiiiii!
   
 4. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ah! Mkuu jamii ina taratibu zake jukumu la kununua madawati liko mikononi mwa serkali wakusanya kodi, sisi wananchi kuchangia ni utashi wetu tu lakini siyo jukumu wala wajibu wetu. Sasa tukisha lipa kodi ile change inayobaki tuna ruksa ya kuitumia tutakavyo na hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutupangia tuitumie kwa namna gani. Pia uchumi kwa kiasi kikubwa unajengwa na jinsi jamii inavyospend pesa, hiyo michango ya harusi huishia kununua vitu mbalimbali ikiwamo vyakula, nguo, miziki, mapambo, vipodozi, nk, nk, kwa hiyo biashara kama saruni, vinywaji baridi na moto, maduka, catering, kampuni za usafirishaji, wasanii wa miziki nk huduma zao hufaidika na michango ya harusi. Kuimarika kwa biashara mbali mbali kunasaidia upatikanaji wa ajira wa wananchi. Mkuu think big think wide!
   
Loading...