Kuchanganya rangi kwa kompyuta

Jane Lowassa

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,756
8,493
Wakuu, naomba kueleweshwa. Ukienda kwenye hardware wanakuambia tunachanganya rangi kwa kompyuta. Hii maana yake teknokojia ipoje?
 
Wakuu, naomba kueleweshwa. Ukienda kwenye hardware wanakuambia tunachanganya rangi kwa kompyuta. Hii maana yake teknokojia ipoje?
Jane soma hiyo uone kama utapata ulichouliza.... to be honest sijaisoma, cant make anya summary!

How Does a Computerized Paint Color Mixer Work?​

Hii nadhani kampuni za rangi kwa kuona kunachangamoto ya mawkala wakuuza rangi zao kuwa na kila aina za mwoneko wa rangi.

Wamewapa wauzaji mitambo ya kuchanganya rangi yoyote atakayochagua mteja kwenye catalog ya kampuni husika.

Muuzaji ananunua Base iliyo-park-iwa katika ujazo flani either Lita 4,10 or 20. Kwa kutumia mtambo ambao ni mdogo ulounganishwa na computer anaingiza formula ya chemicals ktk computer zitachuruzika ktk Base . then inatikiswa na machine ili ijichanganye itokee rangi husika
 
Uelewa wa rangi uko hivi; Rangi za msingi ni Nyekundu(Red), Kijani(Green) na Samawati(blue) yaani RGB.
 
Naendelea; Rangi zingine huitwa rangi sekondari(Secondary Colours). Hizi hupatikana kwa urahisi zaidi kwa kuchanganya rangi tatu za msingi. Hizi ni black, violet, magenta, cyan, purple na nyingine nyingi.
 
Sasa ukitaka rangi yoyote basi, rangi za msingi na sekondari huweza kukupa rangi unayotaka kwa kuchanganya katika uwiano maalum. Rangi tatu tu zinatosha kukupa rangi unayotaka.
 
Concept ya kuchanganya kwa kompyuta ni kwamba mashine hiyo husaidia kutaja uwiano(ratio ya rangi fulani ili kupata rangi ya mteja) wakijua basi uchanganyaji hufanyika kwa kuzingatia ratio. Ndio unapata damu ya mzee, ugoro, rangi ya udongo, kijivu, maziwa, bahari, maji, njano, machungwa, kijani kibichi, dhahabu, silver, kahawia etc.
 
Jane Lowassa Jane Lowassa umeshaanzisha duka la dawa Uyole? Au Mbeya kwa ujumla? Mwaka jana ulikuja kuomba ushauri hapa. Hukuleta mrejesho. Kama umeanzisha,lipia consultancy fee.
 
Wakuu, naomba kueleweshwa. Ukienda kwenye hardware wanakuambia tunachanganya rangi kwa kompyuta. Hii maana yake teknokojia ipoje?
Mkuu Chukulia mfano kampuni kama coca cola ina rangi yake nyekundu Dunia nzima inatumika hio hio hutakuta siku hata moja zinatofautiana.

Tanzania kuna Fundi maiko huko ulaya kuna John doe iweje wataalamu wote hawa waweze kumatch hizi rangi na zikatokea vizuri? Hapa ndio computer inafanya kazi. Kunakuwa na formula maalumu ambayo ukiitumia unapata rangi ile ile.

Kuna mdau ameelezea RGB hapo juu na Mimi nitairudia, huu ni mfumo wa kutumia rangi Nyekundu, kijani na Blue kupata rangi zote duniani, mfano ukiweka nyekundu 255, kijani 255 na bluu 255 unapata rangi nyeupe,
RGB-color-swatches-R-700x342.jpg

Hii RGB ni standard moja ila zipo standard nyingi na kwenye hardware vitu kama rangi za nyumba ama tiles kuna standard kama PMS na CYMK

Mfano hio CYMK inatumia rangi 4 cyan, Yellow, Magenta na black, ukichanganya hizi rangi unapata rangi yoyote unavyotaka.

CMYK-color-swatches-R-700x342.jpg

Hivyo kujibu swali mtu anaposema anachanganya rangi na computer anamaanisha ana uwezo wa kutoa rangi yoyote duniani kwa usahihi na sio kukisia kisia tu kama mafundi mtaani.
 
Asanteni sana wote kwa majibu yenye kujitosheleza. Nadhani hili ndiyo jukwaa lililojaa watu wenye uelewa mpana wa mambo, compared to majukwaa ya akina Bujibuji
 
Uelewa wa rangi uko hivi; Rangi za msingi ni Nyekundu(Red), Kijani(Green) na Samawati(blue) yaani RGB.

Mkuu hapo umeongelea primary colors za mwanga (Light) ndio RGB. lakini kwenye colored paint primary colors ni Red, Blue na Yellow. Ambapo pia kuna wakati hata nyeusi inahusika ingawa nyeusi haitambuliki kama rangi ila inaweza kuwepo kama ilivyo kwenye printer CMYK
 
Ashee! Mimi nimetoa general theory lkn. Practical yaweza kudeviate kidogo kulingana na lengo.
 
Mkuu Chukulia mfano kampuni kama coca cola ina rangi yake nyekundu Dunia nzima inatumika hio hio hutakuta siku hata moja zinatofautiana.

Tanzania kuna Fundi maiko huko ulaya kuna John doe iweje wataalamu wote hawa waweze kumatch hizi rangi na zikatokea vizuri? Hapa ndio computer inafanya kazi. Kunakuwa na formula maalumu ambayo ukiitumia unapata rangi ile ile.

Kuna mdau ameelezea RGB hapo juu na Mimi nitairudia, huu ni mfumo wa kutumia rangi Nyekundu, kijani na Blue kupata rangi zote duniani, mfano ukiweka nyekundu 255, kijani 255 na bluu 255 unapata rangi nyeupe,
RGB-color-swatches-R-700x342.jpg

Hii RGB ni standard moja ila zipo standard nyingi na kwenye hardware vitu kama rangi za nyumba ama tiles kuna standard kama PMS na CYMK

Mfano hio CYMK inatumia rangi 4 cyan, Yellow, Magenta na black, ukichanganya hizi rangi unapata rangi yoyote unavyotaka.

CMYK-color-swatches-R-700x342.jpg

Hivyo kujibu swali mtu anaposema anachanganya rangi na computer anamaanisha ana uwezo wa kutoa rangi yoyote duniani kwa usahihi na sio kukisia kisia tu kama mafundi mtaani.
nimependa, hizo namba kwa mfano R 255 ni nini inawakilishwa, haraka haraka nikajua ni kiasi cha hiyo rangi ila hapo chini kuna mchanganyiko una C63M0Y97 NA K0, hizo zero zina maana gan?
 
nimependa, hizo namba kwa mfano R 255 ni nini inawakilishwa, haraka haraka nikajua ni kiasi cha hiyo rangi ila hapo chini kuna mchanganyiko una C63M0Y97 NA K0, hizo zero zina maana gan?
0 ina maana hakuna kabisa kwenye RGB hii inakuwa ni rangi nyeusi color zote zikiwa zero.

Hizo code zinasomwa kwa mambo kama luminosity, hue na saturation, kuna formula zinaonesha kiasi gani hayo mambo matatu yapo. Luminosity ni kama mng'ao, saturation ni kama kiasi gani rangi imeenea na Hue sijui kiswahili chake sijui ndio tutumie neno ujazo?

Mfano mng'ao unakuwa kwenye scale ya 0 mpaka 1
1*HGWDGRJe5kzSMZouWvXP8g.png

Hivyo kupata scale yake unagawanya number ya kwenye rangi kwa 255

Kama ni 102 kuigawanya unapata 0.4 ina maana hio ndio scale yake,

Pia zipo formula za hue na saturation

Maelezo zaidi angalia hapa

Daah! Nakumbuka Physics Form Three miaka ilee tulisoma haya mambo ya kuchanganya rangi.
 
Back
Top Bottom