Kuchangamsha Bandari ya Mtwara ni zaidi ya kusafirishia korosho.

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
#TUJIKUMBUSHE NA NGOME YA VIJANA.

Ngome ya vijana tar 17 Oktoba tuliwahi zungumzia suala la serikali kutengua maamuzi ya kutumia Bandari ya Mtwara tuu kusafirisha korosho, tar 30 Oktoba 2021 ,Mh.Rais Samia kupitia naibu waziri Bashe walitengua maamuzi hayo ingawa tumechelewa kidogo kutokana na window entry ya msimo wa Korosho Tanzania kwenda mwishoni.

Tunatamani sana Bandari ya Mtwara ifanye kazi na kuchangamka ila kuchangamka kwa Bandari ya Mtwara hakupaswi kutegemea tuu variable/sababu moja ya kusafirisha korosho kwa Bandari hiyo.Kutegemea sababu hii moja athari yake ni kuongezeka kwa gharama za usafirishaji na hivyo kuathiri ununuzi wa korosho kupitia wafanyabiashara na hivyo wakulima kuathirika katika mjengeko wa bei.

Variable/sababu hii bado sio independent, sababu haiwezi kusimama yenyewe tuu ikafanya Bandari kufanya kazi na kuchangamka.Ila lazima tujue variable /sababu hii inategemea sababu/ variables zingine zaidi ili kuifanya Bandari kuchangamka.

Suala la korosho ni la kimsimu tuu kutegemea suala la kimsimu kuchangamsha Bandari haiwezi kuzaa matunda,lazima tutegemee shughuli ambazo zitakuwepo kwa mwaka mzima (Throughout the year ) ili Bandari kuchangamka.

Kwa namna hii suala la kusafirishia korosho Bandari ya Mtwara halitakuwa agizo kutoka Serikalini kama sababu /variables zingine zitafanyiwa kazi .

Lazima tukubali kwamba kuna wajibu wa Serikali haujafanyika ili kuifanya Bandari ya Mtwara kuchangamka . Na ndio maana Ngome ya vijana tulipinga maamuzi ya awali ya Serikali kutaka Bandari ya Mtwara kutumika,ile ilikuwa ni njia ya serikali kutaka kukwepa wajibu wao wa kuifanya Bandari ya Mtwara kuchangamka wakati wote.

Jambo kubwa ambalo serikali na mamlaka ya Bandari wanapaswa kufanya ni kuimarisha shughuli za kiuchumi , uwekezaji na biashara katika Mtwara Corridor ili kuvutia uwepo wa Meli za kutosha Mtwara . Uwepo wa Meli za kutosha Mtwara kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji, shughuli za kiuchumi na biashara kutafanya wafanyabiashara/wanunuzi wa Korosho bila kulazimishwa kusafirisha korosho zao kwa kutumia Bandari ya Mtwara sababu hakutakuwa na gharama kubwa za usafirishaji sababu ya uwepo wa Meli za kutosha Mtwara .

Sisi tunatamani kuona matumizi ya Bandari ya Mtwara kunufaishe makundi yote , kunufaishe wabeba mizigo wa Bandarini , mama Ntilie, kunufaishe Halmashauri kupitia mapato, kunufaishe wanunuzi na wafanyabiashara wa korosho kusafirisha korosho zao kwa wepesi,kunufaishe wakulima wa Korosho pamoja na makundi mengine.

Na hili linawezekana tuu pindi serikali na mamlaka ya Bandari wataamua kuimarisha shughuli za kiuchumi, uwekezaji na biashara katika Mtwara Corridor. Leo hii mizigo mingi ya malawi, Zambia,Msumbiji inapitia Bandari ya Dar es salaam kwanini ? ,Kwanini isipitii kwa Bandari ya Mtwara ? Changamoto nini ?

Kwanini Mikoa ya Lindi, Mtwara, Iringa, Ruvuma ,Njombe, Rukwa na Mbeya haifanywi mikoa ya kimkakati kuifanya Bandari ya Mtwara kuchangamka kwa mizigo inayokwenda au kutoka mikoa hiyo kutumia Bandari ya Mtwara?.

Serikali ina maslahi na Bandari ya Dar es salaam ndio maana inafanya Bandari ya Dar es salaam kuhodhi , Serikali inapaswa kuanza mikakati yake ya kuifanya Bandari ya Mtwara kuwa hub ya mikoa ya Kusini . Hakuna sababu inayofanya Bandari ya Mtwara kudumaa au kutochangamka.Kusini Kuna uchimbaji mkubwa wa madini,Makaa ya mawe , mradi wa chuma (Mchuchuma na Liganga), Gesi,pamoja na uzalishaji wa korosho wenyewe.

Serikali yenyewe haijajidhatiti katika kuimarisha miundombinu kama reli,barabara,kuchochea uwekezaji na shughuli za biashara.

Kuna wajibu haujatekelezwa na serikali kwa maendeleo ya Bandari ya Mtwara pamoja na watu wa kusini, Serikali isiwahujumu watu wa kusini watu wakusini wanapaswa kunufaika kutokana na rasilimali zao.


Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana-ACT wazalendo Taifa.

01/Novemba/2021.
 
Kwani boss wako lile shamba lake la mikorosho alishaliuza au bado?
 
Kuna graphite pale Lindi.....wale jamaa wako kwenye construction, serikali iweke rail line hata ya metergauge kusafirisha graphite kutoka mine site to Mtwara port... hiyo rail line ya Lindi iungwe na line kutoka Songea na makaa yawe exported hapo Mtwara port...

Serikali ijitahidi kuwe na uwekezaji mkubwa wa Makaa ya mawe kiasi cha kuexport..
Tuboost uzarishaji wa cement kwa viwanda vyote itoshereze matumizi ya ndani then turuhusu exportation via Mtwara na Tanga port....Cement + Clinker exportation kupitia Mtwara na Tanga port italeta tija kidogo...

tupige hesabu ya matumizi ya mafuta nyanda za juu kusini na kusini yenyewe then meli hiyo au hizo meli za mafuta ya huko zishushie mtwara na ubebaji uanzie hapo na storage iwe mtwara sio kila kitu dar tu....
 
Kuna graphite pale Lindi.....wale jamaa wako kwenye construction, serikali iweke rail line hata ya metergauge kusafirisha graphite kutoka mine site to Mtwara port... hiyo rail line ya Lindi iungwe na line kutoka Songea na makaa yawe exported hapo Mtwara port...

Serikali ijitahidi kuwe na uwekezaji mkubwa wa Makaa ya mawe kiasi cha kuexport..
Tuboost uzarishaji wa cement kwa viwanda vyote itoshereze matumizi ya ndani then turuhusu exportation via Mtwara na Tanga port....Cement + Clinker exportation kupitia Mtwara na Tanga port italeta tija kidogo...

tupige hesabu ya matumizi ya mafuta nyanda za juu kusini na kusini yenyewe then meli hiyo au hizo meli za mafuta ya huko zishushie mtwara na ubebaji uanzie hapo na storage iwe mtwara sio kila kitu dar tu....
Great !! Ahsante
 
Back
Top Bottom