Kuchangamkia fursa: WaTZ tuna matatizo!. Pongezi Rais Magufuli kuwa M/Kiti SADC, usiposaidia WaTZ kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tu!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,
Baada ya mkutano wa SADC, wageni wameondoka, sasa turejee kwenye maisha yetu ya kawaida ikiwemo kuendelea kuelezana ukweli sometimes ukweli mchungu kupitia hizi makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”. Makala ya leo kwanza ni kutoa pongezi kwa rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, naamini kwa uwezo wake, kama ali transform Tanzania kwa muda mfupi, kutoka nchi ya shamba la bibi, hadi kuwa nchi ya heshima na kupigiwa mfano, hivyo ndivyo atakavyo I transform SADC kuziwezesha nchi za SADC kuchangamkia fursa za SADC kwa nchi wanachama.

Hili ni bandiko la kuuleza ukweli mchungu kuwa katika suala zima la kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara, sisi Watanzania tunamatatizo!. Hivyo natoa pongezi zangu kwa rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti SADC, na kutoa wito kwake, kufuatia Watanzania kuwa ni watu wenye matatizo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi, asipo wasaidia Watanzania kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tuu wa fursa za kiuchumi kama ilivyo sasa kwenye fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Japo mimi sii mchumi, na wala sijui Watanzania tunamatatizo gani katika kuchangamkia fursa mbalimbali hali inayotufanya tubaki nyuma nyuma, lakini kwa vile nimeona tuna matatizo, jukumu langu kama mwana habari, linaishia katika kutoa taarifa tuu kuwa kwenye kuchangamkia fursa, Watanzania tuna matatizo, na Watanzania tukiwa na matatizo, inamaana Tanzania tuna tatizo. Hakuna kitu kizuri kama mtu kukubali udhaifu wako au matatizo yako, ukiisha kubali unamatatizo, huku kujikubali ndio hatua ya kwanza ya kukabiliana na matatizo yako, na mwishowe kuyapatia ufumbuzi wa kudumu. Katika hoja ya kuchangamkia fursa, lazima tujikubali kuwa sisi Watanzania, tuna matatizo, hivyo namuomba rais Magufuli katika uenyekiti wake wa SADC, aanze na charity which begins at home, kwa kuisaidia Tanzania na kuwasaidia Watanzania kuchangamkia fursa za SADC kisha azisaidie nchi nyingine zote za SADC kuchangamkia fursa za SADC bila kusahau fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimesema kwenye kuchangamkia fursa, sisi Watanzania tuna matatizo, kwa sababu Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa nyingi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini kama tumeshindwa kuzichangamkia fursa hizi kikamilifu kwa soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambalo liko next door, what are the chances kuchangamkia fursa za soko la SADC ambali liko mbali?, bila Watanzania kusaidiwa na serikali yetu kwa uhamasishaji kama uliofanyika kwenye kuuhamasisha huu mkutano wa SADC, na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania kuchangamkia soko la SADC, tutaendelea kuwa watazamaji kwenye regional trade, kama hali ilivyo sasa kwa mizigo mingi ikipitia bandari Dar es Salaam, halafu Watanzania tunaifuata huku inakokwenda kama Uganda.

Tanzania inaongoza kwa fursa za SADC na EAC kwa sababu tumepaka na nchi 8, katika ya hizi nchi nane, nchi 6 ni land locked countries, nchi nne ni za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, na nchi 4 ni za SADC, DRC, Msumbiji, Zambia na Malawi. Nchi zote hizo, zinaagiza bidhaa mbalimbali ambazo tunazo, lakini wanaagiza kutoka nchi za mbali, na kuzipitishia bandari zetu, barabara zetu, reli yetu na kuzipelekwa kwao, wakati sisi tungeweza kuchangamkia fursa hizo.

Ninaposema Watanzania tuna matatizo, kimataifa ni nchi ya Tanzania ndio tuna matatizo, kama watu wako wana matatizo, then nchi yako ina matatizo. Mfano kuna kulio kikubwa cha uharibifu wa mazingira kutokana na kukata miti ya kuni kwa nishati ya kupikia, na kuchoma mkaa, wakati tayari tumeishagundua gesi asili. Hata kabla ya ugunduzi wa gesi asili, Tanzania tuna viwanda vya kujaza gesi ya kupikia ya LPG kwenye mitungi na kutumia majumbani, huwezi amini nikiwaambia nendeni pale kwenye mpaka wa Namanga, mshuhudie malori ya gesi ya kupikia kutoka Tanzania, yanavyopeleka gesi Kenya. Hii maana yake mahitaji ya gesi Kenya ni makubwa kuliko uwezo wa Kenya kujitegemea, hivyo wananunua gesi nyingi kutoka Tanzania, huku sisi Watanzania wenyewe tukipikia kuni na mkaa!.

Hii inamaanisha wenzetu Wakenya wamehamasika zaidi kutumia gesi kuliko sisi, huku sisi tukiendelea kutumia kuni na mkaa na kuharibu mazingira yetu, wakati serikali yetu ikiimba nyimbo za utunzaji mazingira, utunzaji vyanzo vya maji kama utunzani misitu na upandani miti bila kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia. Moja ya sababu zinazowafanya Watanzania wa hali ya chini kushindwa kutumia gesi ni bei ya gesi na majiko ya gesi na mitungi ya gesi zenye vat, kama tungetoa msamaha wa kodi kwenye gesi ya kupikia na vifaa vya gesi, tungepata hasara ya kupungukiwa mapato lakini tungeokoa sana mazingira, hivyo ikifanyika a comparative analysis ya hasara ya kuondoa kodi kwenye gesi, na faida za kimazingira, ungekuta taifa linafaidika zaidi kuliko kuathirika.

Sasa tumegundua gesi asili na tunajenga mtambo wa kuchakata gesi, LNG pale Madimba, unaweza kukuta LNG yote inasafirishwa kupelekwa nje kwenda kutumiwa na wazungu wenye pesa, halafu sisi masikini wa Tanzania tukiendelea kutumia kuni na mkaa!. Hata mafuta ya Uganda yatakapitia bomba la mafuta pale Chongoleani Tanga, tangu kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda, Watanzania tungekuwa makini katika kuchangamkia fursa, ungekuta saa hizi tayari tunatengeneza refinery yetu ya mafuta kusubiria mafuta ya Uganda, ili tununue crude oil kutoka Uganda, tusafishe tutumie na ikibidi kuuza nje, tuachane na bulk procurement kununua mafuta nchi za nje, lakini amini usiamini, tunaweza kushuhudia mafuta ya Uganda yakipitia kwetu huku sisi tukiendelea kuagiza mafuta nje ya nchi.

Ukiangalia mahitaji ya soko la SADC na la EAC, utashuhudia bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya bara la Afrika na sisi kufaidika kama wasafirishaji tuu kupitia bandari, reli na barabara zetu, ndio maana azma ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kujenga Tanzania ya Viwanda, rais Magufuli ameona mbali, hii ni fursa, lakini ili hii fursa Tanzania ya Viwanda iweze kuleta manufaa ya kweli kwa taifa letu, ni kwa Watanzania kusaidiwa kuzibaini fursa za bidhaa zinazohitajika katika soko la EAC na SADC, tutengeneza viwanda vya bidhaa hizo zitoke Tanzania kama jinsi China ilivyo hub ya viwanda vya components kwa dunia nzima. Kwa vile Tanzania tunategemea kilimo, then Tanzania ya kweli ya viwanda ni Tanzania ya agro processing industries, kuwekeza kwenye kilimo kama ulivyo mradi wa ASDP II, ndio ulipaswa kuwa priority no. 1.

Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa n SADC baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti amezungumzia mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi na kusistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua na kutolea mfano wa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badala ya kukua. Mh Rais Magufuli kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kwa kushindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP ya nchi za SADC.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mugabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri, hivyo kama alivyotimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere kwa Tanzania kama kuhamia Dodoma na umeme wa Stigler, tunamuomba rais Magufuli aitimize ndoto ya waanzishi wa SADC kiuchumi.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua fursa zilizopo katika nchi mwanachama na kutolea mfano ziara yake ya mwezi May nchini Zimbabwe, alishangaa nchi hiyo kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha ya nafaka. Hivyo kwa soko la SADC na EAC, kuna mahitaji ya bidhaa nyingi ambazo nchi moja inazo na nchi nyingine haina, lakini bidhaa hizo zinaagizwa nje na zinaingia soko la EAC na SADC wakati sisi wenyewe kwa wenyewe tungeweza kuzalisha.

Rais Magufuli ameendelea kushangaa nchi za Afrika licha kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika ni masikini na inalalamika hali duni ya kiuchumi, amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba. Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli, hivyo sasa tunamuomba rais Magufuli baada ya kulitambua hili, autumie uenyekiti wake kuibadili hali hii.

Rais Magufuli ametolea mfano tunaagiza sukari, vyakula, mafuta katika nchi za mbali wakati baadhi ya mataifa ya SADC yanazo bidhaa hizo tena zinapatikana kwa bei nafuu, na kuahidi mwaka wake wa uongozi ameamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira..

“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipobadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Rais Magufuli.

Tumtakie kila la kheri rais Magufuli katika kuijenga SADC mpya kama anavyoijenga Tanzania mpya.

Viva Magufuli,

Viva Tanzania,

Aluta Continua.

Paskali
 
Hivi kuwa mwenyekiti wa SADC unakuwa na mamlaka kama unayo ya exercise nchini kwako?

Anaweza sema tu kuanzia kesho hakuna ushuru wa bidhaa flani. N.k
 
Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”. Makala ya leo kwanza ni kutoa pongezi kwa rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, naamini kwa uwezo wake, kama ali transform Tanzania kwa muda mfupi, kutoka nchi ya shamba la bibi, hadi kuwa nchi ya heshima na kupigiwa mfano, hivyo ndivyo atakavyo I transform SADC kuziwezesha nchi za SADC kuchangamkia fursa za SADC kwa nchi wanachama.

Hili ni bandiko la kuuleza ukweli mchungu kuwa katika suala zima la kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara, sisi Watanzania tunamatatizo!. Hivyo natoa pongezi zangu kwa rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti SADC, na kutoa wito kwake, kufuatia Watanzania kuwa ni watu wenye matatizo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi, asipo wasaidia Watanzania kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tuu wa fursa za kiuchumi kama ilivyo sasa kwenye fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Japo mimi sii mchumi, na wala sijui Watanzania tunamatatizo gani katika kuchangamkia fursa mbalimbali hali inayotufanya tubaki nyuma nyuma, lakini kwa vile nimeona tuna matatizo, jukumu langu kama mwana habari, linaishia katika kutoa taarifa tuu kuwa kwenye kuchangamkia fursa, Watanzania tuna matatizo, na Watanzania tukiwa na matatizo, inamaana Tanzania tuna tatizo. Hakuna kitu kizuri kama mtu kukubali udhaifu wako au matatizo yako, ukiisha kubali unamatatizo, huku kujikubali ndio hatua ya kwanza ya kukabiliana na matatizo yako, na mwishowe kuyapatia ufumbuzi wa kudumu. Katika hoja ya kuchangamkia fursa, lazima tujikubali kuwa sisi Watanzania, tuna matatizo, hivyo namuomba rais Magufuli katika uenyekiti wake wa SADC, aanze na charity which begins at home, kwa kuisaidia Tanzania na kuwasaidia Watanzania kuchangamkia fursa za SADC kisha azisaidie nchi nyingine zote za SADC kuchangamkia fursa za SADC bila kusahau fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimesema kwenye kuchangamkia fursa, sisi Watanzania tuna matatizo, kwa sababu Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa nyingi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini kama tumeshindwa kuzichangamkia fursa hizi kikamilifu kwa soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambalo liko next door, what are the chances kuchangamkia fursa za soko la SADC ambali liko mbali?, bila Watanzania kusaidiwa na serikali yetu kwa uhamasishaji kama uliofanyika kwenye kuuhamasisha mkutano, na kuweka mazingira wezeshe kwa Watanzania kuchangamkia soko la SADC, tutaendelea kuwa watazamaji kwenye regional trade, kama hali ilivyo sasa kwa mizigo mingi ikipitia bandari Dar es Salaam, halafu Watanzania tunaifuata Uganda.

Tanzania inaongoza kwa fursa za SADC na EAC kwa sababu tumepaka na nchi 8, katika ya hizi nchi nane, nchi nne ni za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, na nchi 4 ni za SADC, DRC, Msumbiji, Zambia na Malawi. Nchi zote hizo, zinaagiza bidhaa mbalimbali ambazo tunazo, lakini wanaagiza kutoka nchi za mbali, na kuzipitishia bandari zetu, barabara zetu, reli yetu na kuzipelekwa kwao, wakati sisi tungeweza kuchangamkia fursa hizo.

Ninaposema Watanzania tuna matatizo, kimataifa ni nchi ya Tanzania ndio tuna matatizo, kama watu wako wana matatizo, then nchi yako ina matatizo. Mfano kuna kulio kikubwa cha uharibifu wa mazingira kutokana na kukata kuni kwa nishati ya kupikia, na kuchoma mkaa, wakati tayari tumeishagundua gesi asili. Hata kabla ya ugunduzi wa gesi asili, Tanzania tuna viwanda vya kujaza gesi ya kupikia LPG mitungi na kutumia majumbani, huwezi amini nikiwaambia nendeni pale kwenye mpaka wa Namanga, mshihudie malori ya gesi ya kupikia kutoka Tanzania, yanavyopeleka gesi Kenya. Hii maana yake mahitaji ya gesi Kenya ni makubwa kuliko uwezo wa Kenya kujitegemea, hivyo wananunua gesi nyingi kutoka Tanzania.

Hii inamaanisha wenzetu Wakenya wamehamasika zaidi kutumia gesi kuliko sisi, huku sisi tukiendelea kutumia kuni na mkaa wakati serikali yetu ikiimba nyimbo za utunzaji mazngira, utunzani misitu na upandani miti bila kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia. Moja ya sababu zinazowafanya Watanzania wa hali ya chini ni bai ya majiko ya gesi na mitungi ya gesi, kama tungetoa msamaha wa kodi kwenye gesi ya kupikia na vifaa vya gesi, tungepata hasra ya kupungukiwa mapoto lakini tungeokoa sana mazingira, hivyo ikifanyika a comparison ya hasara ya kuondoa kodi kwenye gesi, na faidi za kimazingira, ungekuta taifa linafaidika zaidi kuliko kuathirika.

Sasa tumegundua gesi asili na tunajenga mtambo wa kuchakata gesi, LNG pale Madimba, unaweza kukuta LNG yote inasafirishwa kupelekwa nje kwenda kutumiwa na wazungu wenye pesa, halafu sisi masikini wa Tanzania tukiendelea kutumia kuni na mkaa!. Hata mafuta ya Uganda yatakapitia bomba la mafuta pale Chongoleani Tanga, tangu kusainiwa kwa kataba wa ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda, Watanzania tungekuwa makini katika kuchangamkia fursa, ungekuta saa hizi tunatengeneza refinery yetu ya mafuta ya Uganda, ili tununua crude oil kutoka Uganda, tusafishe tutumie na ikibidi kuuza nje, tuachane na bulk procurement kununua mafuta nchi za nje, lakini amini usiamini, tunaweza kushuhudia mafuta ya Uganda yakipitia kwetu huku sisi tukiendelea kuagiza mafuta nje ya nchi.

Ukiangalia mahitaji ya soko la SADC na la EAC, utashuhudia bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya bara la Afrika na sisi kufaidika kama wasafirishaji tuu kupitia bandari, reli na barabara zetu, ndio maana azima ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kujenga Tanzania ya Viwanda, rasi Magufuli ameona mbali, lakini ili hii Tanzania ya Viwanda iweze kuleta manufaa ya kweli kwa taifa letu, ni kwa Watanzania kusaidiwa kuzibaini fursa za bidhaa zinazohitajika katika soko la EAC na SADC, tutengeneza viwanda vya bidhaa hizo zitoke Tanzania kama jinsi China ilivyo hub ya viwanda vya components kwa dunia nzima.

Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli amekihutubia mkutano wa nchi za kusini mwa Afrika yaani SADC baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti amezungumzia mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi. Mh Rais amesistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua. Matharani amesema kwa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badala ya kukua. Mh Rais ambaye ndiye Mwenyekiti mpya wa SADC kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kuwa ndio tatizo. Amesema kuwa Secratarieti ndio wanafanya kazi za SADC za kila siku, lakini wameshindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP badala ya hivi ilivyo.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mgabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri, hivyo kama alivyotimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere kwa Tanzania kama kuhamia Dodoma na umeme wa Stigler, tunamuomba rais Magufuli aitimize ndoto ya waanzishi wa SADC kiuchumi.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua furusa zilizopo ktk nchi mwanachama. Amesema katika ziara yake ya mwezi May nchini Zimbabwe, alishangaa nchi hiyo kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha. Hivyo sasa sio nafaka tuu bali kuna bidhaa nyingi zinaingia soko la EAC na SADC kutoka nje, wakati sisi tungeweza kuzalisha.

Rais amesistiza wakati SADCC inabadirika na kuwa SADC ilitegemea kumaliza changamoto zote zilizokuwepo mwanzo, lakini uhalisia bado changamoto zipo. Ameshauri ni lazima sasa milango ya biashara ifunguliwe na kuondoa vikwazo vinavyoweza kuturudisha nyuma.

Dk. John Magufuli amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba. Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo, Rais Magufuli amesema mbali ya kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika inalalamika hali duni ya kiuchumi.

Rais Magufuli amesema Tunaagiza sukari, magari na mafuta katika nchi za mbali huku tukijua baadhi ya mataifa ya SADC yanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nafuu. Ndio maana katika mwaka wangu wa uongozi nimeamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira.

Vievile, fursa nyingi za kibiashara zinapelekwa katika mataifa ya mbali huku baadhi ya nchi zinazozalisha bidhaa nzuri ikiwemo magari na bidhaa nyingine za viwanda zikiachwa mbali ya kuwa na bidhaa bora na zilizo karibu.

Aidha, Rais Magufuli aliigeukia Sekretarieti ya SADC na kuitaka ieleze kwanini uchumi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo unashindwa kufikia viwango vya kukua. Kwanini kwa miaka 10 lengo la kuondokana na tatizo la kiuchumi halijafikiwa.

Awali Rais Magufuli akielezea changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo na kushindwa kufikia baadhi ya makubaliano, Rais Magufuli alisema changamoto ya kwanza ni vurugu za kisiasa, kutokamilika ahadi za kubadili uchumi na ukosefu wa taarifa za fursa katika nchi wanachama.

“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipibadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Rais Magufuli.

Mwenyekiti wa SADC, Dkt. John Pombe Magufuli akifunga mkutano huo, amesisitiza

kuwekeza kwenye miundombinu itakayowezesha kukua kwa uchumi katika ukanda wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wakuu wa nchi hizo walipitia hali ya uchumi katika ukanda wao ambapo uchumi wa nchi hizo ulishindwa kukua kama ulivyotarajiwa kwa asilimia saba na kushuka hadi asilimia 3.1, hivyo wamekubaliana kuwekeza kwenye miundombinu kwa kuwa ni mojawapo ya kikwazo cha kukua kwa uchumi kwenye bara la Afrika ikiwamo nchi za SADC.

Tumtakie kila la kheri rais Magufuli katika kuijenga SADC mpya kama anaijenga Tanzania mpya.

Viva Magufuli,

Viva Tanzania,

Aluta Continua.

Paskali
Ok.
 
Hivi nafasi ya kua chairman wa SADC mtu anadumu nayo kwa miaka mingapi?

Maana nataka kujua haya yote yaliyoainishwa na pasco ataweza kuyafanya kwa muda gani?
 
Bila Serikali kulazimisha kila mtu anayeuza chochote kutumia Mashine ya kodi ni kazi bure, hata kila hoteli au guest house zijae vipi lkn kama kwa kila kitanda kinacholaliwa hakikatwi kodi ni kazi bure, hata Kariakoo pajae vipi lkn bila ya kila kinachonunuliwa kukatwa kodi ni kazi bure, hata migahawa na restaurants zijae vipi lkn kama kila ya sahani ya chakula na kinywaji kinachouzwa havikatwi kodi ni kazi bure, hata dala dala na Mabasi, taxi zijae vipi lkn bila ya kila tiketi kukatwa kodi ni kazi bure, ...
 
Hata kumsifia Jiwe kuwa Chair wa SADC ni Fursa.
Unaweza kuukwaa u DC Mkuu
 
Hoja zako zinamashiko,ni fikirishi kwa mpenda maendeleo,
Kwakua ni ndefu na imelenga kuwafanya walalamikaji waache kulalamika ,watumie fursa ,tegemea kubezwa,wengi hupenda kusikia scandals,discussions za personality za watu nk,
Tunasafari ndefu sana,taifa lilibomoka
 
Nipende kusema tu kuchangamkia fursa unazotaka ni lazima watu wawe na mitaji ya kutosha ili kuwekeza. Serikali imeshindwa kuwajenga watu kushindana sababu ya elimu dhaifu ya ushindani. Serikali ijenge watu wenye mitaji kwa kuwawezesha ndani ya nchi kupunguza kodi ili biashara zirudi upya.
 
Wajenga viwanda na kuchangamkia fursa ni kina nani?

Je! Ni hawa wanaotekwa na kutupwa gymkana?

Je! Ni hawa wanaoitwa wapiga dili?

Ama ni hawa wanaotakiwa waishi kama mashetani?

Au wachangamkia fursa ni hawa wanaomaliza shule na kukaa nyumbani?

Je, Ni hawa wanaoombwa kuweka chereheni nne ziwe viwanda?.

Au unazungumzia wanaofungwa kwa uhujumu uchumi kisha wanasamehewa kisa DPP hana nia ya kuendelea na kesi?

Au wachangamkia fursa ni........

E bana eee acheni kucheka huku mnajua fika kuna misumali makalioni.
 
ukiona watu hawachangamkii fursa ujue kuna shida, na mara nyingi mazingira ya kuwekeza kwenye hizo fursa ni mabovu. bongo ukifanya biashara bila kukwepa kodi haufiki kokote, utakua unaifanyia kazi serikali, sasa si afadhari tuendelee kulala majumbani na wake zetu, taabu ya nini maisha mafupi haya.
 
Wanabodi,
Baada ya mkutano wa SADC, wageni wameondoka, sasa turejee kwenye maisha yetu ya kawaida ikiwemo kuendelea kuelezana ukweli sometimes ukweli mchungu kupitia hizi makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”. Makala ya leo kwanza ni kutoa pongezi kwa rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, naamini kwa uwezo wake, kama ali transform Tanzania kwa muda mfupi, kutoka nchi ya shamba la bibi, hadi kuwa nchi ya heshima na kupigiwa mfano, hivyo ndivyo atakavyo I transform SADC kuziwezesha nchi za SADC kuchangamkia fursa za SADC kwa nchi wanachama.

Hili ni bandiko la kuuleza ukweli mchungu kuwa katika suala zima la kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara, sisi Watanzania tunamatatizo!. Hivyo natoa pongezi zangu kwa rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti SADC, na kutoa wito kwake, kufuatia Watanzania kuwa ni watu wenye matatizo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi, asipo wasaidia Watanzania kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tuu wa fursa za kiuchumi kama ilivyo sasa kwenye fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Japo mimi sii mchumi, na wala sijui Watanzania tunamatatizo gani katika kuchangamkia fursa mbalimbali hali inayotufanya tubaki nyuma nyuma, lakini kwa vile nimeona tuna matatizo, jukumu langu kama mwana habari, linaishia katika kutoa taarifa tuu kuwa kwenye kuchangamkia fursa, Watanzania tuna matatizo, na Watanzania tukiwa na matatizo, inamaana Tanzania tuna tatizo. Hakuna kitu kizuri kama mtu kukubali udhaifu wako au matatizo yako, ukiisha kubali unamatatizo, huku kujikubali ndio hatua ya kwanza ya kukabiliana na matatizo yako, na mwishowe kuyapatia ufumbuzi wa kudumu. Katika hoja ya kuchangamkia fursa, lazima tujikubali kuwa sisi Watanzania, tuna matatizo, hivyo namuomba rais Magufuli katika uenyekiti wake wa SADC, aanze na charity which begins at home, kwa kuisaidia Tanzania na kuwasaidia Watanzania kuchangamkia fursa za SADC kisha azisaidie nchi nyingine zote za SADC kuchangamkia fursa za SADC bila kusahau fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimesema kwenye kuchangamkia fursa, sisi Watanzania tuna matatizo, kwa sababu Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa nyingi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini kama tumeshindwa kuzichangamkia fursa hizi kikamilifu kwa soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambalo liko next door, what are the chances kuchangamkia fursa za soko la SADC ambali liko mbali?, bila Watanzania kusaidiwa na serikali yetu kwa uhamasishaji kama uliofanyika kwenye kuuhamasisha huu mkutano wa SADC, na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania kuchangamkia soko la SADC, tutaendelea kuwa watazamaji kwenye regional trade, kama hali ilivyo sasa kwa mizigo mingi ikipitia bandari Dar es Salaam, halafu Watanzania tunaifuata huku inakokwenda kama Uganda.

Tanzania inaongoza kwa fursa za SADC na EAC kwa sababu tumepaka na nchi 8, katika ya hizi nchi nane, nchi 6 ni land locked countries, nchi nne ni za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, na nchi 4 ni za SADC, DRC, Msumbiji, Zambia na Malawi. Nchi zote hizo, zinaagiza bidhaa mbalimbali ambazo tunazo, lakini wanaagiza kutoka nchi za mbali, na kuzipitishia bandari zetu, barabara zetu, reli yetu na kuzipelekwa kwao, wakati sisi tungeweza kuchangamkia fursa hizo.

Ninaposema Watanzania tuna matatizo, kimataifa ni nchi ya Tanzania ndio tuna matatizo, kama watu wako wana matatizo, then nchi yako ina matatizo. Mfano kuna kulio kikubwa cha uharibifu wa mazingira kutokana na kukata miti ya kuni kwa nishati ya kupikia, na kuchoma mkaa, wakati tayari tumeishagundua gesi asili. Hata kabla ya ugunduzi wa gesi asili, Tanzania tuna viwanda vya kujaza gesi ya kupikia ya LPG kwenye mitungi na kutumia majumbani, huwezi amini nikiwaambia nendeni pale kwenye mpaka wa Namanga, mshuhudie malori ya gesi ya kupikia kutoka Tanzania, yanavyopeleka gesi Kenya. Hii maana yake mahitaji ya gesi Kenya ni makubwa kuliko uwezo wa Kenya kujitegemea, hivyo wananunua gesi nyingi kutoka Tanzania, huku sisi Watanzania wenyewe tukipikia kuni na mkaa!.

Hii inamaanisha wenzetu Wakenya wamehamasika zaidi kutumia gesi kuliko sisi, huku sisi tukiendelea kutumia kuni na mkaa na kuharibu mazingira yetu, wakati serikali yetu ikiimba nyimbo za utunzaji mazingira, utunzaji vyanzo vya maji kama utunzani misitu na upandani miti bila kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia. Moja ya sababu zinazowafanya Watanzania wa hali ya chini kushindwa kutumia gesi ni bei ya gesi na majiko ya gesi na mitungi ya gesi zenye vat, kama tungetoa msamaha wa kodi kwenye gesi ya kupikia na vifaa vya gesi, tungepata hasara ya kupungukiwa mapato lakini tungeokoa sana mazingira, hivyo ikifanyika a comparative analysis ya hasara ya kuondoa kodi kwenye gesi, na faida za kimazingira, ungekuta taifa linafaidika zaidi kuliko kuathirika.

Sasa tumegundua gesi asili na tunajenga mtambo wa kuchakata gesi, LNG pale Madimba, unaweza kukuta LNG yote inasafirishwa kupelekwa nje kwenda kutumiwa na wazungu wenye pesa, halafu sisi masikini wa Tanzania tukiendelea kutumia kuni na mkaa!. Hata mafuta ya Uganda yatakapitia bomba la mafuta pale Chongoleani Tanga, tangu kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda, Watanzania tungekuwa makini katika kuchangamkia fursa, ungekuta saa hizi tayari tunatengeneza refinery yetu ya mafuta kusubiria mafuta ya Uganda, ili tununue crude oil kutoka Uganda, tusafishe tutumie na ikibidi kuuza nje, tuachane na bulk procurement kununua mafuta nchi za nje, lakini amini usiamini, tunaweza kushuhudia mafuta ya Uganda yakipitia kwetu huku sisi tukiendelea kuagiza mafuta nje ya nchi.

Ukiangalia mahitaji ya soko la SADC na la EAC, utashuhudia bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya bara la Afrika na sisi kufaidika kama wasafirishaji tuu kupitia bandari, reli na barabara zetu, ndio maana azma ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kujenga Tanzania ya Viwanda, rais Magufuli ameona mbali, hii ni fursa, lakini ili hii fursa Tanzania ya Viwanda iweze kuleta manufaa ya kweli kwa taifa letu, ni kwa Watanzania kusaidiwa kuzibaini fursa za bidhaa zinazohitajika katika soko la EAC na SADC, tutengeneza viwanda vya bidhaa hizo zitoke Tanzania kama jinsi China ilivyo hub ya viwanda vya components kwa dunia nzima. Kwa vile Tanzania tunategemea kilimo, then Tanzania ya kweli ya viwanda ni Tanzania ya agro processing industries, kuwekeza kwenye kilimo kama ulivyo mradi wa ASDP II, ndio ulipaswa kuwa priority no. 1.

Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa n SADC baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti amezungumzia mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi na kusistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua na kutolea mfano wa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badala ya kukua. Mh Rais Magufuli kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kwa kushindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP ya nchi za SADC.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mugabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri, hivyo kama alivyotimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere kwa Tanzania kama kuhamia Dodoma na umeme wa Stigler, tunamuomba rais Magufuli aitimize ndoto ya waanzishi wa SADC kiuchumi.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua fursa zilizopo katika nchi mwanachama na kutolea mfano ziara yake ya mwezi May nchini Zimbabwe, alishangaa nchi hiyo kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha ya nafaka. Hivyo kwa soko la SADC na EAC, kuna mahitaji ya bidhaa nyingi ambazo nchi moja inazo na nchi nyingine haina, lakini bidhaa hizo zinaagizwa nje na zinaingia soko la EAC na SADC wakati sisi wenyewe kwa wenyewe tungeweza kuzalisha.

Rais Magufuli ameendelea kushangaa nchi za Afrika licha kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika ni masikini na inalalamika hali duni ya kiuchumi, amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba. Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli, hivyo sasa tunamuomba rais Magufuli baada ya kulitambua hili, autumie uenyekiti wake kuibadili hali hii.

Rais Magufuli ametolea mfano tunaagiza sukari, vyakula, mafuta katika nchi za mbali wakati baadhi ya mataifa ya SADC yanazo bidhaa hizo tena zinapatikana kwa bei nafuu, na kuahidi mwaka wake wa uongozi ameamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira..

“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipobadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Rais Magufuli.

Tumtakie kila la kheri rais Magufuli katika kuijenga SADC mpya kama anavyoijenga Tanzania mpya.

Viva Magufuli,

Viva Tanzania,

Aluta Continua.

Paskali
Hilo fursa unazozungumzia sijui ni zipi, Unaweza kwenda Zimbabwe kufanya biashara Zambia au Malawi , Jibu hakuna .South Africa na Botswana unaweza kufanya biashara lakini kupenyeza kwenye nchi zao ni vigumu,
 
Neno "Watanzania tuna matatizo" umelitaja zaidi ya mara kumi. Ni wazi hata huu uzi una matatizo.

Raisi analalamika chakula kununuliwa nje ya Afrika, Hivi ni nani yule aliyezuia chakula cha mahindi kuuzwa nje ya Tanzania?
 
Mimi nilillalamika Sana humu kwa Nini agenda ya gesi ya kupikia haijawa agenda kuu SADC kwenye kupambana na deforestation na climate change? Uzi uko humu jamii forums.Tanzania hatuko aggressive ku makert vyetu hiyo agenda ilitakiwa iwekwe na private sector foundandion ya Tanzania au bussiness council ya Tanzania au chamber of commerce ya Tanzania ,Wizara ya nishati au TPDC na kuitumbukiza .Niliumia Sana .Kenya gas inatumika Sana sababu kule ardhi imehodhiwa na matajiri utakata Kuni wapi? Ukisogea ardhi ya mtu.Hukati.Nakubaliana na wewe serikali ihamasishe utumiaji gesi kupikia after all watu wakihamasika serikali itavuna Kodi nyingi kwa watu kutumia gesi .Maafisa wa serikali huko SADC msiende tu na masuti na matai na vingereza vyenu bebeni tulivyonavyo ingizeni kwenye agenda tuuze.Agenda ya gesi ya kupikia ingizeni kwenye agenda za power and energy au kwenye agenda za climate change na deforestation.Ikieleweka Tanzania tutaonane benefit kea kuuza Sana soko la SADC.Wake up you government officials
 
Wanabodi,
Baada ya mkutano wa SADC, wageni wameondoka, sasa turejee kwenye maisha yetu ya kawaida ikiwemo kuendelea kuelezana ukweli sometimes ukweli mchungu kupitia hizi makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”. Makala ya leo kwanza ni kutoa pongezi kwa rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, naamini kwa uwezo wake, kama ali transform Tanzania kwa muda mfupi, kutoka nchi ya shamba la bibi, hadi kuwa nchi ya heshima na kupigiwa mfano, hivyo ndivyo atakavyo I transform SADC kuziwezesha nchi za SADC kuchangamkia fursa za SADC kwa nchi wanachama.

Hili ni bandiko la kuuleza ukweli mchungu kuwa katika suala zima la kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara, sisi Watanzania tunamatatizo!. Hivyo natoa pongezi zangu kwa rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti SADC, na kutoa wito kwake, kufuatia Watanzania kuwa ni watu wenye matatizo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi, asipo wasaidia Watanzania kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tuu wa fursa za kiuchumi kama ilivyo sasa kwenye fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Japo mimi sii mchumi, na wala sijui Watanzania tunamatatizo gani katika kuchangamkia fursa mbalimbali hali inayotufanya tubaki nyuma nyuma, lakini kwa vile nimeona tuna matatizo, jukumu langu kama mwana habari, linaishia katika kutoa taarifa tuu kuwa kwenye kuchangamkia fursa, Watanzania tuna matatizo, na Watanzania tukiwa na matatizo, inamaana Tanzania tuna tatizo. Hakuna kitu kizuri kama mtu kukubali udhaifu wako au matatizo yako, ukiisha kubali unamatatizo, huku kujikubali ndio hatua ya kwanza ya kukabiliana na matatizo yako, na mwishowe kuyapatia ufumbuzi wa kudumu. Katika hoja ya kuchangamkia fursa, lazima tujikubali kuwa sisi Watanzania, tuna matatizo, hivyo namuomba rais Magufuli katika uenyekiti wake wa SADC, aanze na charity which begins at home, kwa kuisaidia Tanzania na kuwasaidia Watanzania kuchangamkia fursa za SADC kisha azisaidie nchi nyingine zote za SADC kuchangamkia fursa za SADC bila kusahau fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimesema kwenye kuchangamkia fursa, sisi Watanzania tuna matatizo, kwa sababu Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa nyingi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini kama tumeshindwa kuzichangamkia fursa hizi kikamilifu kwa soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambalo liko next door, what are the chances kuchangamkia fursa za soko la SADC ambali liko mbali?, bila Watanzania kusaidiwa na serikali yetu kwa uhamasishaji kama uliofanyika kwenye kuuhamasisha huu mkutano wa SADC, na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania kuchangamkia soko la SADC, tutaendelea kuwa watazamaji kwenye regional trade, kama hali ilivyo sasa kwa mizigo mingi ikipitia bandari Dar es Salaam, halafu Watanzania tunaifuata huku inakokwenda kama Uganda.

Tanzania inaongoza kwa fursa za SADC na EAC kwa sababu tumepaka na nchi 8, katika ya hizi nchi nane, nchi 6 ni land locked countries, nchi nne ni za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, na nchi 4 ni za SADC, DRC, Msumbiji, Zambia na Malawi. Nchi zote hizo, zinaagiza bidhaa mbalimbali ambazo tunazo, lakini wanaagiza kutoka nchi za mbali, na kuzipitishia bandari zetu, barabara zetu, reli yetu na kuzipelekwa kwao, wakati sisi tungeweza kuchangamkia fursa hizo.

Ninaposema Watanzania tuna matatizo, kimataifa ni nchi ya Tanzania ndio tuna matatizo, kama watu wako wana matatizo, then nchi yako ina matatizo. Mfano kuna kulio kikubwa cha uharibifu wa mazingira kutokana na kukata miti ya kuni kwa nishati ya kupikia, na kuchoma mkaa, wakati tayari tumeishagundua gesi asili. Hata kabla ya ugunduzi wa gesi asili, Tanzania tuna viwanda vya kujaza gesi ya kupikia ya LPG kwenye mitungi na kutumia majumbani, huwezi amini nikiwaambia nendeni pale kwenye mpaka wa Namanga, mshuhudie malori ya gesi ya kupikia kutoka Tanzania, yanavyopeleka gesi Kenya. Hii maana yake mahitaji ya gesi Kenya ni makubwa kuliko uwezo wa Kenya kujitegemea, hivyo wananunua gesi nyingi kutoka Tanzania, huku sisi Watanzania wenyewe tukipikia kuni na mkaa!.

Hii inamaanisha wenzetu Wakenya wamehamasika zaidi kutumia gesi kuliko sisi, huku sisi tukiendelea kutumia kuni na mkaa na kuharibu mazingira yetu, wakati serikali yetu ikiimba nyimbo za utunzaji mazingira, utunzaji vyanzo vya maji kama utunzani misitu na upandani miti bila kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia. Moja ya sababu zinazowafanya Watanzania wa hali ya chini kushindwa kutumia gesi ni bei ya gesi na majiko ya gesi na mitungi ya gesi zenye vat, kama tungetoa msamaha wa kodi kwenye gesi ya kupikia na vifaa vya gesi, tungepata hasara ya kupungukiwa mapato lakini tungeokoa sana mazingira, hivyo ikifanyika a comparative analysis ya hasara ya kuondoa kodi kwenye gesi, na faida za kimazingira, ungekuta taifa linafaidika zaidi kuliko kuathirika.

Sasa tumegundua gesi asili na tunajenga mtambo wa kuchakata gesi, LNG pale Madimba, unaweza kukuta LNG yote inasafirishwa kupelekwa nje kwenda kutumiwa na wazungu wenye pesa, halafu sisi masikini wa Tanzania tukiendelea kutumia kuni na mkaa!. Hata mafuta ya Uganda yatakapitia bomba la mafuta pale Chongoleani Tanga, tangu kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda, Watanzania tungekuwa makini katika kuchangamkia fursa, ungekuta saa hizi tayari tunatengeneza refinery yetu ya mafuta kusubiria mafuta ya Uganda, ili tununue crude oil kutoka Uganda, tusafishe tutumie na ikibidi kuuza nje, tuachane na bulk procurement kununua mafuta nchi za nje, lakini amini usiamini, tunaweza kushuhudia mafuta ya Uganda yakipitia kwetu huku sisi tukiendelea kuagiza mafuta nje ya nchi.

Ukiangalia mahitaji ya soko la SADC na la EAC, utashuhudia bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya bara la Afrika na sisi kufaidika kama wasafirishaji tuu kupitia bandari, reli na barabara zetu, ndio maana azma ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kujenga Tanzania ya Viwanda, rais Magufuli ameona mbali, hii ni fursa, lakini ili hii fursa Tanzania ya Viwanda iweze kuleta manufaa ya kweli kwa taifa letu, ni kwa Watanzania kusaidiwa kuzibaini fursa za bidhaa zinazohitajika katika soko la EAC na SADC, tutengeneza viwanda vya bidhaa hizo zitoke Tanzania kama jinsi China ilivyo hub ya viwanda vya components kwa dunia nzima. Kwa vile Tanzania tunategemea kilimo, then Tanzania ya kweli ya viwanda ni Tanzania ya agro processing industries, kuwekeza kwenye kilimo kama ulivyo mradi wa ASDP II, ndio ulipaswa kuwa priority no. 1.

Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa n SADC baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti amezungumzia mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi na kusistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua na kutolea mfano wa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badala ya kukua. Mh Rais Magufuli kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kwa kushindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP ya nchi za SADC.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mugabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri, hivyo kama alivyotimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere kwa Tanzania kama kuhamia Dodoma na umeme wa Stigler, tunamuomba rais Magufuli aitimize ndoto ya waanzishi wa SADC kiuchumi.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua fursa zilizopo katika nchi mwanachama na kutolea mfano ziara yake ya mwezi May nchini Zimbabwe, alishangaa nchi hiyo kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha ya nafaka. Hivyo kwa soko la SADC na EAC, kuna mahitaji ya bidhaa nyingi ambazo nchi moja inazo na nchi nyingine haina, lakini bidhaa hizo zinaagizwa nje na zinaingia soko la EAC na SADC wakati sisi wenyewe kwa wenyewe tungeweza kuzalisha.

Rais Magufuli ameendelea kushangaa nchi za Afrika licha kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika ni masikini na inalalamika hali duni ya kiuchumi, amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba. Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli, hivyo sasa tunamuomba rais Magufuli baada ya kulitambua hili, autumie uenyekiti wake kuibadili hali hii.

Rais Magufuli ametolea mfano tunaagiza sukari, vyakula, mafuta katika nchi za mbali wakati baadhi ya mataifa ya SADC yanazo bidhaa hizo tena zinapatikana kwa bei nafuu, na kuahidi mwaka wake wa uongozi ameamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira..

“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipobadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Rais Magufuli.

Tumtakie kila la kheri rais Magufuli katika kuijenga SADC mpya kama anavyoijenga Tanzania mpya.

Viva Magufuli,

Viva Tanzania,

Aluta Continua.

Paskali
Mh P, umezunguka kwa bandiko refu.. Mwisho hujaainisha fursa ni zipi...Ungeenda moja kwa moja kwenye mada .
 
Ninaposoma mwandishi kama Pasco anasema "Pongezi Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa SADC ........,. " napata aina Fulani ya kigugumizi na kujiuliza jee Pasco anania gani? Kupotosha? Kukebehi? au naye hajui?
Nani kamchagua kuwa mwenyekiti wa SADC? Kwanini asiwe mkweli kuwa mwenyekiti ni Tanzania baada ya mzunguko kufika zamu yetu? Mbona Leo tunajua kuwa mwakani ni nchi Fulani iwe kwa rais aliyepo au mpya itakuwa tuu ilivyo?
Juzi nimemsikia DC mmoja akikiambia kikao kuwa juhudi za Rais Magufuli zimefanya achaguliwe Kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa SADC. Kweli DC anaweza kuwa na akili za namna hiyo?
Pengine hizi kebehi ambazo hata Pasco amekuwa mhanga wa kuzitoa itafika mahali Mwenyekiti wa CCM atagundua na kuwashukia kama mwewe wote wanao mfanya zumbukuku kwa kumpa sifa za uongo.
Angekuwa anabaki na cheo hicho tuu cha ccm nisingejali lakini ndio Rais wa TZ na hatupendi Rais wetu akebehiwe namna hii.
Pascal Mayalla acha kumsanifu Rais wetu namna hii.
 
Hilo fursa unazozungumzia sijui ni zipi, Unaweza kwenda Zimbabwe kufanya biashara Zambia au Malawi , Jibu hakuna .South Africa na Botswana unaweza kufanya biashara lakini kupenyeza kwenye nchi zao ni vigumu,
Zambia,Malawi unaota watanzania kibao wako kule wamejaa tele Wana Hadi Vituo vya mafuta .mikoa ya mipakani biashara zao nyingi kubwa ziko Zambia na Malawi hujui unachoandika.Zimbabwe Hadi mafuta ya alizeti yanauzwa kule .Malawi mfanya biashara mkubwa Ni bakhresa ndie huwakilisha Malawi Hadi maonyesho ya biashara ya kimataifa.Naona huna taarifa wewe.Yaani ulichoandika unakijua mwenyewe.Unaonyesha uko Giza unalojua mwenyewe.Nenda Mbeya tu pale mjini Hadi machinga wanafanya biashara Malawi na zambia .Nenda soko la SADC Lusaka asilimia 80 watanzania wachaga wakiongoza kwa uwingi.Nenda coperbelt Zambia uone muziki was watanzania,nenda pemba msumbiji uone
 
Paskali Tanzania ya neema wakati wa Uenyekiti wa SADC na baada ya Uenyekiti wa SADC wa JPM unawezekana kabisa kabisa kama serikali itakuwa mdau namba moja kushirikiana na Watanzania wengine wapya wenye uwezo wa kuanzisha uwekezaji mpya ambao soko lake ni la ndani na nje ya SADC.

Mambo mengine yanahitaji fedha, mengine government incentives na mengine government guarantee in term of equipment purchase na mkopo wa working capital towards execution ya mradi.

Mathalani jana umesainiwa mkataba wa billion Zaidi ya 400 kujenga barabara za Dodoma. Civil works business.
Nani anajenga barabara? huko ndiko fedha zinakwenda
Nani ana-supply kokoto. (Hapa serikali inaweza kutoa avenue Watanzania wapya waka-establish kampuni crushing machines kwa ajili ya barabara, SGR, uwanja wa ndege, uwanja wa mpira. Ukiwapa watu wapya vijana wetu wa engineering, marketing, accounts, legal, logistics hapo kuna watu wapya kufanya biashara na kupanua wigo wa ajira likewise new tax payers.

Si sawa aje mchina au mturuki yeye huyu huyo asage mawe yetu na achukue hela yetu. If necessary hao Watanzania wawe chini ya usimamizi wa jeshi ku-enhance discipline.
Money will begin to flow. Watu wakiwa na hela wata-spend kujenga nyumba, "kula bata"; so eventually hela inarudi tena serikalini interm of kodi ya spending.

Kama Waziri wa viwanda na biashara na waziri wa ujenzi haoni kwa jicho hili ili kuhakikisha kwa yale Watanzania wanayoweza kufanya ifanyika kila liwezekanalo wawe actors. Fedha ita-flow na kubaki ndani.

Such strategy not policy, strategy hubadilika tokana na wakati tokana na mahitaji kama timu ya mpira au vitani vile.

Biashara ni vita kama vita zingine. Tanzania lazima isimame na Watanzania kama business force yake ambayo lazima ishinde pale ambapo hela zinabaki ndani.

Mtu yeyote akipata nafasi soma kitabu cha kijasusi wa uchumi. Ni open book. Na wao muandishi ni jasusi ambae kaeleza namna ambavyo mataifa makubwa USA, Canada, Russia, China, Germany, France, Japan kila moja lina economic intelligence model.

Pitia hapa chini model za Ufaransa na Japan

1566291482604.png

1566291530683.png

Nimefanikiwa kusoma (open thesis) ya mwanafunzi mmoja wa masters ya uchumi USA.
Katika moja ya jambo kubwa kaweka wazi, kwa makampuni makubwa Ulaya na Marekani wanafanya sana tafiti za kukuza masoko ya biashara zao.

Moja ya jambo alilo-indicate ni kuwa 80% ni utafiti wa wazi (Overt findings) na 20% ni tafiti za kijasusi (covert findings)
Utafiti wa huyo jamaa umegundua 20% ya utafiti wa kijasusi unaingiza products za services zinazo-count 80% ya revenue za makampuni ya ulaya na USA. (Kumbukeni figisu ya Canada na USA kuhusu Huwaie mtaelewa wenzetu biashara ni vita ni ujasusi)

Let be back to point. Haihitaji rocket science ya high level ya intelligence ya kiuchumi. Ni right strategy on how to produce best products and services locally tupunguze imports na ku-maximize exports kwa soko la Tz, SADC na kwingineko.

The best way to predict the future is to create it...Njia pekee ya kukuza kipato cha Watanzania ni ku-create avenues Watanzania wawe actors.

Kama ambavyo watoto wanakopeshwa kusoma chou kikuu (yet hana hakika ya ajira na kulipa mkopo); kwa model sahihi zikifanyika tutatoboa na kulipa mikopo TIB au TADB.

Pitia hapa pia kuna ushauri nimetoa. Huwa inasemwa serikali haifanyi kazi kupitia mitandao ya kijamii japo inakamata wahalifu wa mitandaoni.
Na pia kuna ukurasa wa instram na twitter zinatupa feedback ya nini kimetokea serikalini, nani kapewa "shavu" na nani kaliwa kichwa.

Lets play as a team to solve issues on poverty and create wealth in our midst.

https://www.jamiiforums.com/threads...yake-kutengeneza-mabilionea-tanzania.1615838/

Natamani wakubwa wawe na insight haya yafanyike, at end of the day ujiko watapata wao
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom