Kuchagua mwenza: Pale mwanamke anapojikuta anaangukia kulamba GARASA…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
shutterstock_badpicker1.jpg

Linapokuja swala la mapenzi, wanawake ndio wanaokabiliwa na changamoto nyingi katika kuchagua mwenza hususan pale wanapokuwa wametokana na wanaume kadhaa ambao wameonyesha nia. Kutoka huko hakumaanishi kukutana kimwili bali hata kule kuwa na mitoko (dates) za mara kwa mara ambapo zote zinaonekana kuzaa matunda, hapo ndipo wanawake hujikuta wakikabiliwa na mtihani mzito wa kuchagua kwamba aolewe na yupi.

Nimeshawahi kuwasikia baadhi ya wanawake ambao niko nao karibu wakidai kwamba wanajuta kwa sababu uchaguzi wa wenza waliooana nao haukuwa sahihi kwa sababu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika ndoa zao tofauti na matarajio yao.

Je wewe ni mmoja wa wanawake wanaojutia uamuzi wa kuolewa na mwanaume uliye naye sasa?

Ukweli ni kwamba kuna idadi ya kutosha ya wanawake ambao wanajutia uamuzi wa kuolewa na wanaume walio nao leo. Wapo ambao wameshindwa na kujiondoa katika ndoa hizo, lakini wamejikuta tena wakiangukia kulamba garasa kwa maana ya kuolewa na wanaume hao hao wasio sahihi kwao mpaka wanajiuliza kama wana mkosi gani.

Lakini wapo ambao wamefaulu kujifunza kutokana na makosa na wakamudu kukubali matokeo na kubadili namna yao ya kufikiri kutoka upande wa hasi na kuweka fikra zao upande wa chanya, na hivyo kuleta mabadiliko makubwa katika uhusiano wao na kurejesha upendo. Hawa wamefanikiwa kuishi katika ndoa zao bila kujuta wala kuumiza hisia zao.

Wapo waliojitoa na kujipanga upya na kisha kwa umakini mkubwa kupata mwenzi aliye chaguo lao, wakiepuka kutorudia makosa waliyoyafanya awali, hawa mara nyingi sana huwa ni wale waliopata wasaa wa kutuliza akili na kufikiria kwa umakini na kupata jibu kwamba walikosea wapi. Wapo wanaopata msaada wa ushauri nasaha, lakini pia wapo wanaomudu kutuliza akili wakiwa peke yao na kupata suluhu muafaka.

Je mnadhani ni kwa nini linapokuja swala la kuchagua mwenza wapo baadhi ya wanawake ambao huangukia kupata mwanaume Garasa……

Mara nyingi wanawake wanaojikuta wakiangukia kulamba garasa ni wale wanaokabiliwa na matatizo yafuatayo:

1. Wanakuwa wamesongeka kutokana na kuvunjika moyo baada ya uhusiano wao wa awali kuvunjika katika mazingira ambayo hawakuyatarajia, hivyo hutafuta suluhu ya haraka ili kuziba pengo. Inapotokea kukutana na mwanaume mfujaji anayejua kujali hisia za wanawake mara nyingi hutokea kumuamini mwanaume huyo bila kukagua maeneo mengine ya tabia, na kwa sababu bado akili yake imefungwa hujikuta amelamba garasa bila kujijua na hata akijua inakuwa ni too late. Hapo ndipo atajiuliza maswali mengi. Je kitoka katika uhusiano huo jamii itamuaonaje? Je itamuona hajatulia? Je itamuona ni Malaya au ana matatizo ya kutomudu kulinda uhusiano? (Kumbuka uhusiano wowote ukivunjika jamii huelekeza lawama kwa mwanamke)

2. Kutojiamini na kusubiri kukamilishwa na wengine

3. Utegemezi wa kihisia

4. Kuogopa kukosea

5. Kuogopa kusikiliza machale yao (Intuition). Kwa kawaida sisi binadamu tuna machale. Kwa mfano kama mwanamke anakua na uhusiano na mwanaume ambaye siyo husband material, ipo sauti ndani mwao huwaambia kwamba watafanya makosa kuolewa na mwanaume fulani…. Lakini hutokea kudharau sauti hiyo ambayo mara nyingi hujirudia mara kwa mara. Sauti hii sisi huiita machale, na mara nyingi sisi tumekuwa hatusikilizi machale yetu, hudharau na mwisho wa siku tunajikuta tumeangukia mahali pabaya au tumeumia.

6. Malezi ya wazazi nayo huchangia kuwafanya wanawake wengi kuangukia kulamba garasa katika kuchagua mwenza. Hebu fikiria mzazi au wazazi wanaotukuza watu wenye fedha na kusifia wanawake walioolewa na wanaume wenye fedha. Kama anafanya hivyo mbele ya watoto wake wa kike,hapo somo linakuwa limetimia kwamba mwanaume wa maana ni yule mwenye fedha tu, na hapo ndipo unapoweza kumuona mwanamke anangukia kwa mwanaume mwenye fedha lakini mnyanyasaji na mzinzi kupita kiasi lakini yumo tu haoni wala hasikii…

7. Makundi, hii nayo ni shule nyingine ambayo huwakabili wanawake wengi kuangukia kulamba garasa wanapochagua mwenza, mafunzo ya makundi bila kuchanganya na zako huwaponza wanawake wengi......
 
nafikiri hiyo namba tano tunatakiwa kujifunza zaidi. basi tu wanawake tunajifanyaga viziwi sometimes. ila hata ukiramba garasa sio mbaya ni changamoto tu. maisha hayapo mteremko kama tunavyoyadhania, hiyo ni changamoto pia.
 
hapo sio machale kwa sisi wapendwa tu nasema roho ya ndani NIMEPASTE HAPA:
5. Kuogopa kusikiliza machale yao (Intuition). Kwa kawaida sisi binadamu tuna machale. Kwa mfano kama mwanamke anakua na uhusiano na mwanaume ambaye siyo husband material, ipo sauti ndani mwao huwaambia kwamba watafanya makosa kuolewa na mwanaume fulani…. Lakini hutokea kudharau sauti hiyo ambayo mara nyingi hujirudia mara kwa mara. Sauti hii sisi huiita machale, na mara nyingi sisi tumekuwa hatusikilizi machale yetu, hudharau na mwisho wa siku tunajikuta tumeangukia mahali pabaya au tumeumia.
 
nafikiri hiyo namba tano tunatakiwa kujifunza zaidi. basi tu wanawake tunajifanyaga viziwi sometimes. ila hata ukiramba garasa sio mbaya ni changamoto tu. maisha hayapo mteremko kama tunavyoyadhania, hiyo ni changamoto pia.
Mwanangu Husninyo nimezungumzia jambo hili la changamoto za ndoa katika kipengele hiki....

Lakini wapo ambao wamefaulu kujifunza kutokana na makosa na wakamudu kukubali matokeo na kubadili namna yao ya kufikiri kutoka upande wa hasi na kuweka fikra zao upande wa chanya, na hivyo kuleta mabadiliko makubwa katika uhusiano wao na kurejesha upendo. Hawa wamefanikiwa kuishi katika ndoa zao bila kujuta wala kuumiza hisia zao.
 
Last edited by a moderator:
lingine wawe wana approach(tongoza) basi vinginevyo sina uhakika kama katika wale wote wanaokuja kwao kuonyesha nia (date nao) ni chaguo lao
 
Mmmh!
Wanaume ni wajanja sana pindi wakimdoea mtu!
Fake moral!
Fake smile!
Fake wisdom! And other fake habits hutufanya kuwaingiza kingi ke wengi!
...
There is no ANY components that is sufficience to make woman aamini kama anapendwa kweli!!!
.
Ukizingatia watu tunatofautiana sana!
Kwa mfano me wenye ukarimu, ni ngumu sana kwa ke kuproof penzi la hawa watu, and almost me wote wakarimu ndio hupendwa sana na ke na ndio wasaliti wakubwa wa mapenzi!
...
Also ke wengi huwakataa me wanaostahili kutokana na style yao ya kutongoza! Yap, me wengi ambao ni husband material hawawezi/hawajui kutongoza! Sasa ke wengi huwachukulia hawa watu kama wanaushamba na ulimbukeni!
Thus why hujikuta wakinasa kwa me wenye swaga kali ambazo ni fake!
...
Nikubaliane na wewe Mtambuzi kuhusu suala la kumsoma mwenzio nje ndani! But remember hii task sio ndogo!
 
lingine wawe wana approach(tongoza) basi vinginevyo sina uhakika kama katika wale wote wanaokuja kwao kuonyesha nia (date nao) ni chaguo lao

Kabisa mkuu wanawake wanabweteka xana katika hili akimpenda m2 anajishaua 2 hasemi mwisho wa siku anachukuliwa na mwingine. Learn girls! Learn women! Fight for what you need.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom