Kuchagua mke au mume..Je ni sahihi wazazi kushiriki??

socket

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
305
431
Ni matumaini yangu mu wazima nyote.
Hiki ni kisa cha ukweli na kinaniweka njia panda. Huyu ndugu yangu wa kiume alikuwa na mpenzi wake ila baada ya wazazi (Mama) kumuona huyu Binti hawakuridhika naye japo sisi kama vijana na muhusika mwenyewe yaan kaka tuliona Bnt yuko poa,

Wazazi walimshauri kuwa huyu sio mke na asifunge naye ndoa ila baada ya muda wakafunga ndoa. Sasa juzi baada ya kuishi kama mwaka na nusu wakaachana kutokana na tabia za Binti.

Najua vijana wengi mmepita hii stage na wengine tunapitia ila tushauriane wakati ukifika, je ni vyema kuwashirikisha wazazi ilihali muda huo utakuwa na huyo mrembo??

Lakini pia mabinti msiwe mnatuangusha maana mwanzo mnanyenyekea mno mpaka tunawaamini
Nawasilisha
 
Ndiyo wazazi unatakiwa uwashirikishe wakimkataa mtu wako hayo ni matatizo yao. Pia wewe usipodumu kwenye ndoa yako hayo ni matatizo yako si yao.
 
Kumshirikisha wazazi ni jambo sahihi ila ikitokea wakakataa na ili hali ushafanyanae mambo mengi ikiwemo na zinaa. Huwa unakuwa mtihani mkubwa sana kwa sababu ulimwamini na alikuamini japo kuna kasoro unaweza kuwa unaziona ukadhani ni ndogo ila wazazi wakaziona zina mashiko katika maisha ya kila siku
Kwa mfano unakuta binti hapendi kujishughulisha na vikazi vidgo vidgo vya nyumbani hapo huwa inakuwa changamoto kubwa sana
 
Tatizo mtu ukishazama kwenye penzi hata ukiambiwa baya kuhusu mpenzi bila kujali ni kweli au sio kweli, utahisi wanamuonea tu!

Pia, vijana huwa tunawashirikisha wazazi katika hatua za mwisho kabisa, mambo mengi huwa tumeshayamaliza sisi kabla ya kuwa shirikisha, hivyo inakuwa vigumu kupokea ushauri kutoka kwa wazazi maana hata kushirikishwa kwa kwako huwa inakuwa ni sawa na kupewa taarifa tu! na wanakuwa hawana mwaya wa kukosoa jambo na likafanyiwa kazi.. zaidi zaidi utawaona wanamchukia tu baby wako..!

Binafsi naona ni sahihi kuwa shirikisha wazazi wako tena mapema sana kabla things get too serious..! Ila ukisubiri penzi likolee hadi uwe kipofu. Ukiwashirikisha ni sawa na kuwapa tu taarifa kuwa unataka kuoa.
 
Kama kuna jambo tunalokosea vijana wa .com ni kutotambua mchango wa wazazi ktk maandalizi ya kumchagua mke. Binafsi nasema wazazi ni muhimu mnoo
 
Mimi akinipenda mume wangu tu inatosha.
Na hao wazazi nablock kabisa hawanisaidii chochote....


Sio maneno yangu, huwa nayaona tu mitandaoni.
 
Sometimes yes sometimes not, amini husiamini muda mwingine wazazi wanakuingiza chaka na hii imemtokea kaka yangu.
 
Wazazi wana nafasi yao kwenye kukupa ushauri na maono yao...

Ingawa siyo kila kitu unaweza fuata... Za kuambiwa unachanganya na za kwako kidogo...
 
Wazazi wanashiriki kwenye kutambulishwa tu, mambo mengine mtajijua wenyewe, kwani anayeoa mzazi?

Inabidi utumie akili ujiongeze kama unayefunga naye ndoa ni mtu anakufaa, chochote kikienda wrong, u~handle it yourself. Wazazi wangemchagulia huyo jamaa alafu binti akasumbua je? Lawama zote si angezirudisha kwa wazazi? Mtu yeyote yule anabadilika, ukiona wife hazipandi weka pembeni vuta mwingine, ila pia siyo guarantee kua mpya atatulia siku zote, watu hawatabiriki.

Ndoa kitu kingine aisee, tunaona watu wana tabia njema sana, alafu wakishavalishwa pete wanabadilika ghafla. Bachelor club zamu yetu bado.
 
Back
Top Bottom