Kuboronga Kwa Kilimanjaro Star Mashindano Ya CECAFA, niliwahi Kuandika Kuhusu Kocha Minja

Huu ni mtihani wa kwanza wa Rais wa TFF, Wales Karia. Aache mambo ya kubebana, hii awamu ya tano anaweza asibaki salama.
 


Mpango wa uhakika wa kuongeza viwango vya michezo ni kwenye elimu.

Kama tulivyogundua mapungufu kwenye vifaa vya shule maabara wakati wa kikwete, vyumba vya madarasa na madawati mpaka uwezo wa kulipia awamu hii ya tano,

step inayofuata iwe michezo mashuleni na afya ya watoto ikiwemo vyakula mashuleni. Namna ya kugharamiwa haya mambo lazima itafutwe.

Raisi ametangaza ongezeko la wanafunzi na maendeleo mengine katika miaka 56 ya Uhuru wa Tz Bara.

Ukiangalia takwimu siyo kwa kutaka kulaumu awamu zilizopita, kuna mabadiliko ya mfumo wa kijamii na uchumi ambao kiasi fulani umechangia kushuka kiwango cha michezo nchini ukiihusisha elimu na sera zake.

Miaka 1960, shule zilikuwa chache, tulicheza vizuri michezo mingi kwa kuwa uwekezaji na mfumo wa utawala wa elimu ulikuwa mzuri. Quality ya michezo ilikuwa nzuri ingawa quantity ilikuwa ndogo.

Miaka ya sabini, tulipanua elimu, quantity iliongezeka, lakini hazina ya wachezaji waliokuwa chipukizi miaka ya 1960 ndiyo walikuwa nyota miaka ya sabini, wakakutana na kupanuka kwa elimu(quantity) na unafuu elimu bure, tukaenda fainali AFCON 1980.

Baada ya 1980 tuliathirika na vita ya Uganda, elimu ya kujitegemea na kubana matumizi, wanafunzi walitumia muda mwingi kwenye kazi za kujitegemea, program za michezo zilishuka ajili ya pesa kupungua, pia wanafunzi waliepuka michezo ajili ya challenge za masomo.

Miaka ya 1990 ikakosa flow ya vipaji toka mashuleni,

miaka 2000 ikawa mbaya zaidi kwani hata michezo inaelekea ilipunguzwa au zuiliwa mashuleni hivyo 2010 nayo ilikosa flow ya chipukizi.

Sasa hivi kuna wafadhili wengi na umaskini umepungua kidogo.

Itafutwe namna ya ku source vyanzo vipya na channel tena fedha kwenda mashuleni ila vyanzo mbadala kama wafadhili n.k vitafutwe ili miaka kuanzia 5 mpaka 10 tena ijayo tuone mazao ya miaka baada ya uhuru waliotupeleka fainali mwaka 1980 na medali kwenye Olympiki.

Mikakati hasa mpango wa miaka 5 wa maendeleo uonyeshe malengo hayo kwa wizara za Elimu na ile ya habari, sanaa na michezo.
 
Back
Top Bottom